tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,240
- 4,466
Juzi wafanyabiashara jijini Mwanza wamelalamika kwamba biashara zinafungwa kwa sababu makadirio ya kodi ni makubwa kuzidi uhalisia.
Leo nilikuwa Kariakoo, nimewasikia wafanyabiashara fulani wakimjadili mfanyabishara mmoja waliyemuita Iwawa (naamini sikosei jina). Wanadai katika vikao vya wafanyabiashara wa Mbeya na TRA mwaka jana, Iwawa aliwalaumu TRA Mbeya kuwabambikia kodi wafanyabiashara wazawa wa Mbeya kama wanakomoa kwa sababu hawana machungu na biashara zao, na kwamba hiyo ni sababu kubwa ya wafanyabiashara wengi wenye asili ya huko kutowekeza biashara zao kwenye mji wa Mbeya. Inadaiwa ndani ya wiki kadhaa baada ya hicho kikao Iwawa alipelekewa madai ya kodi yanayozidi milioni mia sita (600,000,000/=).
Inawezekana ni tetesi tu, lakini kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusiana na makadirio ya kodi kwa baadhi ya miji, huku wafanyabiashara wa kabila fulani wakidaiwa kutosumbuliwa sana na haya makadirio.
Huwezi shughulikia tetesi zote, lakini tetesi kama hizi zinapaswa kuchunguzwa kwa ustawi wa Taifa.