Consolata na Maria ; Pacha walioungana na kufariki dunia watazikwa ndani ya jeneza moja au watatenganishwa ?

Dk Faith Kundy aliyekuwa akiwahudumia pacha Maria na Consolata katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa ameeleza jinsi Consolata alivyofariki dunia kati ya dakika 10 hadi 15 baada ya mwenzake kufariki.

“Wakati tunampa Maria huduma ya kwanza na namna alivyokuwa anatapatapa, Consolata alianza kuhisi hali hiyo ndio maana alikuwa akinisukuma na kusema tuache, tuache, tuache na nilikuwa nawaambia pumua... pumua... pumua... niliwasisitiza hivyo,” amesema Dk Kundy.

Ameeleza kuwa katika kuungana kwao kuna viungo vilivyokuwa pamoja.

“Anaweza kula Consolata na Maria akasema ameshiba na hata suala la maumivu ataanza kulalamika Consolata na baada ya muda mfupi Maria analalamika,” amesema.
Daktari huyo ameeleza kuwa tangu walipowapokea pacha hao kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hawakuwa kwenye hali nzuri kwa sababu Maria alikuwa akitumia oksijeni kupumua.

“Kwa hiyo walikuwa chini ya uangalizi na tulikuwa tunaangalia hali zao na kama kuna tatizo basi tunawasaidia,” amesema.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Museleta Nyakiroto alipoulizwa kuhusu iwapo mmoja angeendelea kuwa hai kwa muda mrefu, amesema pacha hao walikuwa na mshipa mmoja mkubwa wa damu uliokuwa ukiwasaidia wote wawili.

Dk Nyakiloto aliwaeleza waandishi wa habari Jumamosi, Juni 2 kuwa pacha hao walifariki dunia wakipatiwa matibabu katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU).

“Tangu wafikishwe hospitalini hatukuwahi kuona wakibadilika kiafya kiasi kile. Jana (juzi) hali yao ilikuwa tofauti sana. Maria ndiye alianza kufariki na baada ya dakika 10 alifuata Consolata,” alisema
kulikua na uwezekano wa m1 kufa na mwinginekubaki hai??
kama m1 alipatwa na ugonjwa wa moyo lazima na mwingine aupate?
 
Dk Faith sisi tunakufa,” hiyo ndio ilikuwa kauli ya mwisho ya Consolata Mwakikuti wakati pacha mwenzake, Maria akiwa katika hali ya umauti.

Dk Faith Kundy ndiye aliyekuwa akiwahudumia pacha hao katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa mpaka dakika ya mwisho walipofariki dunia juzi usiku.

Akizungumza na Mwananchi jana Jumapili, Juni 3 daktari huyo alisimulia hali ilivyokuwa katika dakika za mwisho za uhai wa pacha hao na kueleza kuwa baada ya kuona hali ya mwenzake imebadilika, Consolata alianza kumsukuma (Dk Faith) akimtaka aache kuwapatia matibabu, akieleza kuwa alikuwa katika maumivu makali na tayari alishakata tamaa.

Awali, Dk Faith alisema juzi saa kumi na moja jioni alipigiwa simu kuwa hali ya pacha hao imebadilika.

“Nilikimbia hadi wodini kwa ajili ya kuwaona na kuwahudumia. Nilipofika niliwaona wauguzi na madaktari wengine wakiendelea kutoa huduma ya kwanza hivyo niliungana nao kwa ajili ya kuokoa uhai wao,” alisema.

“Kuna dawa niliwapatia ambazo huwa zinamsaidia mtu anapokuwa anakosa hewa, Maria alikuwa ameanza kubadilika kabisa na kwa wakati huo hakuwa na ufahamu. Ilikuwa hata ukimuita haitiki wala kuonyesha kama anasikia.”

Dk Faith alisema wakati huo mfumo wa upumuaji wa Maria ulikuwa chini kabisa hivyo baada ya huduma hiyo, alirejea kwenye hali yake ya kawaida.

“Hapo Maria alifungua macho, ukimuita anaitika na akawa na hali nzuri baada ya huduma,” alisema.

Aliendelea kusimulia kuwa baada ya hali zao kuwa vizuri aliendelea kuwahudumia wagonjwa wengine hadi saa moja jioni alipoitwa tena na kuambiwa hali za pacha hao zimebadilika.

“Nilipoenda kwa mara ya pili, Maria alikuwa kwenye hali mbaya kama ile ya kwanza na safari hii hakuweza kupona. Ilikuwa kama saa mbili usiku sikumbuki vizuri dakika ila ndio muda ambao Maria alitutoka,” alisema.

Daktari huyo alisema Maria akiwa kwenye umauti, Consolata pia alianza kutetemeka na kulalamika maumivu makali mwili mzima.

“Alikuwa anaona kama hamsikii ‘ham-feel’ mwenzake na akawa ananisukuma huku akiniita kwa jina’ ‘Dk Faith sisi tunakufa’ aliniambia akisisitiza niwaache. Maria hakuweza kuongea chochote dakika za mwisho na wakati huo Consolata anasema hivyo Maria alikuwa tayari ameshafariki.”
 
Eehh Mola wangu jamani!
Ni mateso makali sana walahi uwiii ehhh!
Rip watoto wazuri jamani!
 
kulikua na uwezekano wa m1 kufa na mwinginekubaki hai??
kama m1 alipatwa na ugonjwa wa moyo lazima na mwingine aupate?
Madaktari waje wajibu swali hili maana nilikuwa nawaza the same
 
Na wamezaliwa wengine Leo kagera wameungana, kama maria na conso,,ngoja nilete picha
 
Waliozaliwa Leo
 

Attachments

  • Screenshot_2018-06-04-22-35-50.png
    Screenshot_2018-06-04-22-35-50.png
    99.8 KB · Views: 38
Back
Top Bottom