connection ya uuzaji viungo vya watu, na siku za mwisho wa dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

connection ya uuzaji viungo vya watu, na siku za mwisho wa dunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwana wa Mungu, Nov 14, 2008.

 1. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  siku hizi, sio kitu kigeni kuona viungo vya binadamu vinauzwa kwa waganga kwa hela nyingi. walianza watu wenye vipara, waliwindwa kishenzi. ikaja kuchuna ngozi za watu na kuziuza kwa hela nyingi. ikaja kukata matiti ya akina mama na kuyauza kwa hela nyingi(hasa kule mbeya). ikaja kukata sehemu za siri na kuziuza kwa hela nyingi. ikaja kukata kiungo chochote na kukiuza kwa hela nyingi. sasahivi imekuja kukata viungo vya albino na kuviuza. kwa watu ambao wanasali dini ninasali mimi, wanaweza wakakubaliana na mimi kuwa, siku hizi ni siku za mwisho. watu wanapenda pesa kuliko Mungu, na wako tayari kufanya chochote kile ili tu wapate pesa hata kama ni kinyume na maagizo ya Mungu. wengi tunajua kuwa, kutakuja kipindi cha mpinga kristo, ambaye atakuja kuendeleza sana mambo kama haya. hivyo, hii ni dalili tu ya huyu mnyama, kwani bado hajafunguliwa kikamilifu, akijafunguliwa baada ya watakatifu kunyakuliwa,ndo wote waliobaki watabapa adha za namna hii nyingi. mpinga kristo atakuwepo kwa muda ambao sio mreefu sana, na akijua kuwa anao wakati mchache, atafanya mambo mengi ya kutisha ili akamilishe mambo yake. huu ni unabii upo kwenye biblia.

  blessed are they who trust in the Jesus today, na sio hivyo tu, bali wale watakaovumilia hadi mwisho. for they will reap what they saw now.

  watu wako tayari kuua mtu kwasababu tu ya uwaziri, kupata duka kubwa,urais,ubunge,milioni za pesa au gari,cheo n.k. ubinadamu unazidi kupungua. ni dalili za kukaribia ule mwisho,pale ambapo mpinga kristo atafanya sana mambo kama haya. wengi tunajua kuwa, kuna mji mmoja unaoitwa Hila kule Iraq, ambao umetabiriwa kuwa itakuwa ndo centre ya maasi, na viungo vya watu vitakuwa vinauzwa kule. kuna mengi ya kuongelea kuhusu jambo hili, with evidence, lakini kwa hapa, naomba kuwataadharisha enyi wasomaji wenzangu wote, kuwa, mwisho umekaribia. kila mwenye akili aamua sasa kuuacha uovu na kuifuata njia ya Mungu wa kweli. asate.
   
 2. h

  hallanus Member

  #2
  Nov 15, 2008
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa tahadhari uliyotoa kwa wasomaji. Ni nani wa kupona tusipojali
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I believe in existence of God and I fear him Most and second to Him I fear him who fears Him not but about the last day Nah!
  Sounds superstitious to me!
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Inategemea unayajua mambo haya kwa upeo gani. Kama wewe unaona hili ni jipya inabidi usome zaidi historia ya dunia. Haya mambo ya kuuza viungo vya binadamu yametokea sana kwenye sehemu nyingine za dunia. Huko kunakoitwa kukaribia mwisho wa dunia unakokusema wewe is not a story mwisho ulishakaribia siku nyingi, lakini sio kwa kuua albino. Inategemea upeo wako wa akili na kufikiri ukoje. Kuna watu kama wewe walituambia kuwa mwaka 2000 ni mwisho wa dunia, sasa hivi wanafunika sura zao chini kama mbuni. Unaweza kushangaa kuwa wewe mwenyewe unakufa dunia inabaki. Kuna uwezekano miwsho wako wewe ukawa umekaribia lakini sio mwisho wa dunia. Sijui kama nimeeleweka.
   
Loading...