Congress waiomba Uongozi wa Trump kuiwekea vikwazo Venezuela haraka iwezekanavyo

mcomunisti halisi

Senior Member
Jan 17, 2017
103
328
Makubaliano baina ya wanasheria wa chama cha Republican na Democrat wanamtaka Rais Donald Trump awawekee vikwazo Venezuela haraka iwezekanavyo kutokana na ukiukwaji wa haki za binaadamu zinazondelea nchini humo na mafungamano ya serikali ya Venezuela na mashirika ya kigaidi.

Sen.Bob Menendez wa chama cha Democrat na Sen.Ileana Ros-Lehtinen wa chama cha Rep walituma maombi white house wachukue hatua wiki hii kuwawekea vikwazo serikali ya Venezuela na kuwawekea vikwazo maofisa wa serikali ya Venezuela akiwemo makamu wa rais wa Venezuela Tareck El Aissami ambaye anadhaniwa kuwa ana mafungamano na makundi ya kigaidi yenye msimamo mkali.

Mwanzoni mwa mwaka huu serikali ya kibepari ya USA wamekuwa wakiikosoa serikali ya kijamaa ya Nicolas Maduro kwa kumchagua El Aissami katika moja ya nyadhifa ya juu kabisa nchini humo,serikali ya kibepari ya USA inadai ya kwamba El Aissami ana mafungamano na makundi tofauti ya kigaidi na yenye msimamo mkali.

USA inadai ya kwamba mataifa ambayo siyo aminifu kama Iran yanafungamana na mataifa mengine ambayo yanachuki na nchi za magharibi kama Venezuela katika kuendeleza nguvu ya kuidhoofisha USA.Baadhi ya Wataalamu wanadai ya kwamba wafuasi wa kikundi cha Iran cha Hezboullah na makundi mengine yameonekana yakiingia amerika ya kusini

''Tunaandika maombi haya kwa Uongozi wako ichukue hatua ya haraka kuwawekea vikwazo viongozi wa utawala ambao wanasababisha ukiukwaji wa haki za binaadamu ,ukandamizaji wa haki za binaadamu na ufisadi ambao unaendelea Venezuela-''barua hiyo ilisoma hivyo

''zaidi ya yote ni hatua ya Maduro kumchagua Tareck El Aissami kuwa makamu wake wa rais ambaye huenda akawa rais ajaye wa Venezuela ,jambo hili linastua sana sababu El Aissami anahusishwa na makundi ya kigaidi na makundi ya madawa ya kulevya

''pia tunaguswa na utawala wa Maduro unavyoendelea kutesa watu wasio na hatia nchini Venezuela.

''USA inabidi ichukue hatua za nguvu dhidi ya Venezuela ili kuitenga uongozi wa Maduro na kuichakaza serikali ya Maduro mpaka atakapoachia madaraka.

''Muunganiko kati ya ufisadi,ulanguzi wa madawa ya kulevya na ushawishi wa mashirika ya kigaidi ndani ya Venezuela na shughuli zote hizi hufanywa na El Assaimi

El Aissami pia anashutumiwa kwa kugawa passport kwa wafuasi wa Hamas na Hezboullah nchini humo,

Serikali ya kijamaa ya venezuela kwa kipindi kirefu imekuwa kwenye mgogoro na serikali ya kibepari ya USA,Rais aliyepita Hugo Chavez alikuwa kwenye ugomvi wa muda mrefu na USA na kupelekea nchi yake kuwekewa vikwazo vya kila aina,mrithi wake wa sasa Nicolas Maduro ameendeleza falsafa na mfumo aliouacha mtangulizi wake.Venezuela inaendeshwa na Chama cha United Socialist Party of Venezuela hivyo mlengo wao upo tofauti na matakwa ya USA jambo linalochochea chuki na uhasama baina ya nchi mbili hizi .




Nchi za Amerika ya kusini zenye mlengo wa ujamaa kama Bolivia,Venezuela na Cuba zimekuwa kwenye uhasama na mgogoro wa muda mrefu na USA.Pia Rais wa nchi ya Nicaraguana ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Socialist Sandinista National liberation front Daniel Ortega amekuwa akichukiwa na USA.




tarek.jpg
Tareck Zaidan El Aissami makamu wa rais wa Venezuela ambaye anatuhumiwa kuwa na ukaribu na Iran na mashirika yanayopigwa vita kama Hezboullah
 
Uzuri america si kama makonda hiyo inasemekana ana mafungamano ujue ni ukweli huyo mtu washamchunguza
 
Back
Top Bottom