Congrats Zitto Kabwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Congrats Zitto Kabwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Oct 14, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Invisible,
  Mkuu hata sielewi mahusiano ya kichwa cha habari na maelezo uloyatoa hapa..Sioni uhusiano wa Zitto na habari hii ikiwa wananchi wenyewe wa Kigoma hawatahusika zaidi ktk mjadala huu. Ni wao wanaofahamu uwakilishi wa Zitto kama mbunge wao na kaweza yepi.
  Binafsi Zitto namtazama kama mbunge wangu wa Upinzani hivyo sifa zake zinatokana na uwakilishi wake wa hoja za upinzani ndivyo navitazama zaidi mathlan swala la Buzwagi, na mikataba feki lakini anapokuja kupendekeza tena mkataba feki mwingine inaondoa nguvu kubwa ya sifa alovuta wakati wa Buzwagi. Kwa sababu hata mkataba wa Buzwagi ungetuwezesha kuvuta japo kidogo hizo asilimia 3 na zikapunguza matatizo yetu, pia wakazi wa Buzwagi ambao wanahitaji sana huduma za Shule, Zahanati, Maji safi na Umeme wangeweza kupata japo kiduchu..Barrick wangeweza kuondoa tatizo hilo la wakazi wa Buzwagi nikitumia mtazamo wake ktk swala la Dowans..
   
 3. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  labda zitto ni mbunge wa "tanzania yote"

  btw ... nani kaendesha hii poll?
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Tunaweza kupata report nzima? Maana naona hizo charts peke yake zinaweza zisiseme mengi.

  Pamoja na hayo Hongera kwa Zitto na Wabunge wenzake walioonyeshwa kwenye chart, angalau wananchi wanaona michango yao.
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mkandara,

  Nimeambatanisha doc nzima. Well, ni vema kuangalia "Page 36" maana image haionekani vema then utajua naongelea nini.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Invisible,
  Mkuu, shukran nimekupata sasa hizo asilimia 25 ndio sifa ya mbunge washuhuri wa Kitanzania?..kaazi kweli kweli!. Hizo 25% ya wananchi kukubali uwakilishi wa mtu ni failure kwa Mbunge, mtu kama Zitto anatakiwa kujipima yeye mwenyewe anakubalika vipi na sii kutazama walioko nyuma yake..
  Kifupi mkuu wangu ukiwa ktk mtihani uka score asilimia 25% kweli unastahili kupongezwa au ndio kusema shule hiyo haifai kabisa!...mtu wa kwanza kwa aslimia 25% basi hiyo sii shule tena mwondoe mwanao asisome hapo..
  Tunachojifunza hapa ni kwamba Bunge letu halkina wabunge kabisa, wananchi hawana imani nalo kabisa iwe mtu kwa mtu.
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkandara,

  Pamoja na kwamba wananchi wa Kigoma Kaskazini wanaweza wasihusike kutoa maoni yao kwenye huu mjadala, bado ninaona siyo vibaya jamii ikijua ama kusoma report kama hizi just kutufahamisha kwamba wabunge gani wanaowajibika kwa wananchi wao na nchi yao.

  Lakini nina tatizo moja kwenye hizo charts, sijajua waliohojiwa ni watanzania wote nchi nzima ama ilikuwaje? Kama ni survey ya nchi nzima then interpretation ya charts inatakiwa ifanywe with caution.

  Tunaweza kupima utendaji wa Mbunge kwa njia mbili. Moja, je, wapiga kura wake (jimboni) wana maoni gani kuhusu Mbunge wao. Kuna vipengele vinaongelea ushiriki wa Mbunge kwenye shughuli za maendeleo, sasa kama respondent ni mkazi wa Dar au Mwanza atajuaje yaliyo kwenye ground huko Kigoma Kaskazini ama Same kwa Mama Kilango au Kyela kwa Dr. Mwakyembe? Kwa hiyo charts hizi zingetoa picha halisi kama tungejua Jimboni kwa mbunge husika wananchi wanasemaje? Na hapo inabidi kuwa makini kwamba waliohojiwa ni wa chama gani? Maana wengine ni wakereketwa, hata Mbunge afanye mambo mazuri kiasi gani bado wataona hajafanya kitu kwa kuwa ni si Mbunge wa kutoka chama chao.

  Ngazi ya pili ni at a National Level, ambapo sasa akina Mkandara na Keil wanaweza kutoa maoni yao kwamba kwa jinsi tunavyomuona Bungeni akitoa hoja ama kuibana serikali tunaona kwamba anafaa sana. Ingawa kwenye hili kundi maoni yetu hayawezi kuwa na maana sana kwa kuwa sisi sio wapiga kura wa Mbunge husika. Kwa hiyo mimi nikisema Zitto anafaa kurudi Bungeni kwenye uchaguzi wa mwakani, ni utashi wangu lakini siwezi kuchangia chochote kwenye kumrudisha Bungeni. Ningekuwa ni mkazi wa Kigoma Kaskazini, kura yangu moja ina mchango mkubwa sana kumrudisha Bwana Zitto mjengoni na pia hata nikiongea na vijana wenzangu Jimboni ninaweza kuwa-influence wakaona mazuri ya Zitto na wao wakaongezea kura zao.

  Ndiyo maana nikamuomba Invisible kama anaweza kutuwekea report yote ili tusome na kuona sample ilipatikana vipi. Tusije tukawamwagia pongezi sisi wakazi wa Dar lakini kwenye majimbo yao kuko hoi bin taaban na wapiga kura wao hawataki hata kuwaona.
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 9. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwanza nimpongeze Zito, pamoja na weote walioonekana katika hiyo watatu wanaomfuatia.

  Lakini hapa ndipo panapokuwa na matitizo katika design ya utafiti kama huu. Swali, unapolielekeza kutafuta mbunge aliyefanya vyema, halafun ndani yake unchanganya na mawaziri, ni lazima utapata matokeo yanayoegemea upande mmoja (biased). Waziri anawakilisha serikali, na mara nyingi wananchi inawawia vigumu kupima watu hawa 2 katika mizani moja. Ingekuwa ni waziri yupi aliyekonga nyoyo za wananchi, na ni mbunge yupi aliyekonga nyoyo za watu. Vingenevyo ni kutowaweka mawaziri katika mizani wanayostahili.

  Jambo jingine, katika hizo kurasa 2 haijaelezwa kuwa watu waliohojiwa walipatikana kwa utaratibu upi, ambayo nayo kitakwimu inaweza kuwa na matatizo kufanya tathmini wakilishi.
   
 10. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,042
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Purely UDAKU.
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kama sio mauzauza.
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Kwenye utafiti kama huu, ni watu wachache tu, sio rahisi uwahusishe watanzania wote, ama sivyo itakuwa uchaguz wa rais.

  Pili hii haina ubishi wala hailazimishi kila mtu akubaliane nao.

  So, wote mnaopinga, aidha mfanye zenu, kuna mtu anasema bunge la Tanzania halina wabunge kabisa!!!! yet anasema , mbunge Zito ni wa Kigoma!!!!

  Kuna ubishi ambao hauna msingi , ili mradi kuonekana unabisha,
   
 13. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  bado sijaelewa hapa
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kuna tatizo gani akiwa mbunge wa TZ yote
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  well said mkuu.Mbona REDET wanaposema JK ni rais bora kabisaaaa toka tanzania ipate uhuru kwani ilihusisha watanzania wote?thinkimng ya miafrika iko biased and one sided sana..
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Waberoya,
  Mkuu punguza jazba hii kitu haikukaa sawa kabisa. Hata Redet wana afadhari mara 10 ya kitu hii maanake hatuwezi kumpongeza Zitto kwa sababu tu yeye ni wa kwanza na amepata kura asilimia 25 yaani kati ya watu 100 ni 24 tu waliompitisha. haya ni matusi makubwa kwa kiongozi huyo.
  Na ukitazama mwisho wa hizo kura utaona kisanduku kinachosema DKNone chenye asilimia 24..nikichukulia pengine ndio kusema Hakuna mbora which includes Zitto mwenyewe..hii ni dalilimbaya sana kwa wabunge wetu, labda iwe haina maana hiyo.
  Kisha tazama maswali yaliyoulizwa basi, ni vitu ambavyo vinatokana na magazeti yaani sifa ambazo tunaweza kumpa mbunge ni zile tulizozisikia toka magazetini zikilenga umaarufu wa mtu..Wangesema hivyo basi kuwa hapa tunatazama umaarufu wa mtu na sii swala la kuchaguliwa ama kufanya mazuri bungeni wakati hatufahamu kabisa nani kafanya nini bungeni zaidi ya scandals za utawala huu..
  Hata hao REDET hutoa takwimu za Umaarufu wa Kikwete na kwa sababu yeye ni rais wa Tanzania nzima binafsi napokea takwimu zao kama somo hata kama kuna makosa ya utekelezaji wake. Labda nikufahamishe kidogo nilichoelewa mimi upate kuona wapi nazungumzia..
  Kwanza, sifa za mbunge kulingana na point walizo score.. Ya kwanza ambayo imepata kura nyingi inasema nini?..I am not keen on the issue or the name of the minister! hii wamevote kwa asilimia 19...ipo juu kabisa ya kura zote na sijui kuna ubora gani wa kiongozi yeyote zaidi ya kutupoteza kabisa..ya pili inayofuata inasema He fights for the poor!- kivipi mkuu wangu and who are the poor! Je, ni Wananchi, Walalahoi au wanatafuta mbunge mwenye mtazamo wa siasa za Kijamaa kugawana umaskini.
  Hilo tuachane nalo twende mbele zaidi..

  Shuka chini ktk hesabu ya Wabunge wanaotegemewa kurudi bungeni utakuta ni asilimia 42 swali la kwanza linasema - Careless in his work, hapo wame vote kwa asilimia 22 juu ya kila kipengele cha uchaguzi wa wabunge hao watakao rudi bungeni. Mimi mkuu wangu sielewi hapa wanaposema Careless on his work, wana maana gani kiasi kwamba iwe sifa ya kwanza kumrudisha mbunge..laa sivyo ni ashirio tosha kwamba hatuna wabunge wa maana (the are all negligent) kwa asilimia hiyo 19, hii sio sifa hata kidogo..

  Hata hivyo naomba darasa mkuu wangu ikiwa mimi ndio sikuelewa... karibu
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hiyo page iko wapi mbona siioni zaidi ya hapo juu bwana invisible ?
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hakuna tatizo tunamkubali kuliko hao tulionao
   
 19. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkandara,
  Inawezekana unapoint lakini unashindwa kuchallenge hiyo ripoti kwa hoja kama zilivyotumika humo. Kumbuka kuwa huu ni utafiti na wala siyo hisia za mtu, kwa hiyo basi ninakushauri go back na kuchambua vianzilishi, viashiria nk vya utafiti ili ujenge hoja zenye nguvu. Kukataa utafiti bila ya kufanya utafiti sidhani kama ni sahihi.
   
 20. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  wakuu sijaelewa hapa nini kinaendelea CONGRATS ZITTO KABWE for what??????/ !!!!!!!!
   
Loading...