Congo: Watu wengine tisa wauawa baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha Wilayani Beni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,862
Watu wenye silaha, wamewauwa watu tisa, katika mauaji ya hivi karibuni kutokea katika Wilaya ya Beni, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kuendelea kuzua wasiwasi miongoni mwa raia kuhusu usalama wao.

Ripoti zinasema kuwa, watu hao waliuawa kwa kukatwa mapanga katika kijiji cha Manzati, Kilomita 25 kutoka mji wa Eringeti katika wilaya hiyo.

Mwakilishi wa Gavana katika eneo hilo, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo yaliyotokea Jumatano asubuhi.

“Kijiji cha Manzati kilishambuliwa na watu wenye silaha, nyakati za asububi na watu wameuawa na wengine kuamua kuondoka,” alisema.

Hali hii imezua wasiwasi mkubwa, na watu zaidi ya 200 wamekimbilia katika mji wa Eringeti kwa hofu kuwa wanaweza kushambuliwa tena.

“Nimeamua kukimbia baada ya kushuhudia mauaji, moyo wangu umechoka sana, watu wengi wamekimbia,” alisema mmoja wa watu walioamua kukimbia.

Mashirika ya kiraia, yanasema kuwa, watu zaidi ya 40,000 wameyakimbia makwao kutokana na ukosefu wa usalama unaoendelea kushuhudiwa katika wilaya hiyo.

Tangu mwezi Oktoba mwaka 2019, mamia ya raia wamepoteza maisha, huku waasi wa ADF Nalu wakishtumiwa kuhusika na ukosefu wa usalama.

Licha ya serikali kupitia jeshi la FARDC kutangaza kushirikiana na lile la Umoja wa Mataifa MONUSCO kupambana na waasi hao, mauaji yameendelea kushuhudiwa.
 
Serikali inayoshindwa kulinda raia wake ni serikali dhaifu.
Hivi Congo si wapo na civil war miaka na miaka? Au huwa ni vita gani Proved ?
Wanajeshi wa Tz nasikia wanalinda amani huko chini ya UN, yaelekea nchi imefeli kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom