Congo DRC yawasilisha ombi la kujiunga jumuiya ya Africa Mashariki.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
4,675
2,000
Habari JF siasa.

Rais wa Congo DRC Felix Tshekedi aliye ziarani nchini Kenya ametumia fursa hiyo kuomba kujumuishwa taifa lake ktk jumuiya ya Africa mashariki inayozidi kupanuka kwa kasi.

Alitoa ombi hilo ktk ikulu ya Nairobi ktk dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais mwenyeji Uhuru Kenyatta.


Alidai Congo DRC inahitaji kujumuishwa ktk ushirikiano huu kuliko kipindi chochote ktk historia ya taifa hilo kubwa barani Africa lenye raslimali nyingi.

Ombi la Congo DRC linakuja ktk kipindi kifupi baada ya Somalia nayo kuwasilisha ombi kama hili.

Source: BBC
 

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
4,675
2,000
Kabla ya kuwakubalia hao ni vyema vikawepo vipengele vya nchi wanachama waanzilishi kuwa na nguvu ya kuwadhibiti hao wanachama wapya vinginevyo ipo siku maadui zetu hasa sisi Tanzania kwa kutumiwa na vibaraka wakatusumbua na kutukwamisha ndani ya jumuia na pia nchi moja isipohudhuria mkutano basi kusikwamishe nchi nyingine kuendelea na mkutano na kufanya maamuzi fulani kama ilivyotokea juzi kati mkutano ulishindwa kufanyika kwa sababu ya Burundi kushindwa kutuma mwakilishi
Hili nalo neno
 

Gidbang

JF-Expert Member
Jun 1, 2014
3,517
2,000
Kuikaribisha DR Congo ni Sawa na kumkaribisha Ngamia kwenye Hema, hii Jumuiya ya Africa mashariki mpka sasa inataka kua kimbilio la Madictator.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa maana ya kuuchumi ni eneo la kimkakato sana kongo ina raia zaidi ya 70m wanahitaji nafaka kwa sana na wana hela za madini na tunawez kuweka soko kunwa la madini wat Africa
 

Zambotti

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,667
2,000
Yaani wangekuwa wanajiunga tu then kila mtu na lake sawa. Lakini hawa wenzetu kwenye nchi zao wana matatizo mengi kiasi watataka msaada kutoka kwenye makubaliano ya umoja.

Asa pata picha huku M23 kule Al-shabab then hao wahanga wawe wanataka msaada, sijui tunaanzia wapi mungu wangu
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,925
2,000
Mimi nafurahia sana nchi hizi kama Somalia, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda kuwemo kwenye jumuia hii ya Afrika Mashariki, kwa sababu moja kuu: Itatusaidia sana sisi Tanzania kuepuka ulaghai, hasa wa Kenya.

Sijui kama nitaeleweka kwa bandiko hili. Maana yake ni kwamba sidhani kuwa kutakuwepo na Jumuia imara, itakayowezesha hadi pawe na shirikisho pakiwemo na wanachama kama hao. Hilo litahitaji muujiza!
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,925
2,000
Hivi hii jumuia haizingatii geographical location?
Inazingatia. DRC ni jirani na Rwanda, Uganda, Burundi, Tanzania, yaani wana'share' mpaka na wanachama wengine wa Jumuia. Hilo ni takwa moja muhimu zaidi.
Tunaweza hata kuwahimiza jirani zetu Zambia, Malawi, Mozambique nao wajiunge.
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,800
2,000
Kwani AU imekufa?! Kuna faida gani za kuwa ndani ya EA community?! Sisi ni member tunafaidikaje ni East Africa community
 

kimswilia

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
1,020
2,000
Habari JF siasa.

Rais wa Congo DRC Felix Tshekedi aliye ziarani nchini Kenya ametumia fursa hiyo kuomba kujumuishwa taifa lake ktk jumuiya ya Africa mashariki inayozidi kupanuka kwa kasi.

Alitoa ombi hilo ktk ikulu ya Nairobi ktk dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais mwenyeji Uhuru Kenyatta.


Alidai Congo DRC inahitaji kujumuishwa ktk ushirikiano huu kuliko kipindi chochote ktk historia ya taifa hilo kubwa barani Africa lenye raslimali nyingi.

Ombi la Congo DRC linakuja ktk kipindi kifupi baada ya Somalia nayo kuwasilisha ombi kama hili.

Source: BBC
2020 baada Lissu kuingia ikulu tutajiondoa kwenye umoja huo wa kizushi kama Wingereza na mpango wake wa Brexit
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom