Congo DRC: Marekani yashinikiza Rais Joseph Kabila asigombee tena kwenye uchaguzi ujao.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Marekani imemshinikiza Rais wa Congo DRC Joseph Kabila kutangaza kuwa hatogombea tena katika uchaguzi ujao wa Disemba 23.

Hatua hiyo ya Marekani imekuja baada ya mataifa ya Ufaransa na Uingereza kufanya hivyo siku zilizopita.

Wiki iliyopita Kabila alitarajiwa kuwa angetangaza Bungeni nia yake ya kuwania urais wa kuiongoza Congo kwa muhula mwingine tena lakini ameacha watu wakihisi juu ya nia yake.

#My take hii ndiyo dawa kwa madikteta wote barani Afrika wanaozifanya nchi kama mali zao binafsi.
 
Last edited:
Safi, aachie wengine, DRC iko ovyo sana na huyu kalio hataki kutoka tu miaka yote, watu tumekua jamaa yupo tu kama Rais na hakuna chochote cha maana kwenye kinchi kimasikini balaa.Nchi za kiafrika ovyo sana, mambumbumbu wengi.
 
Marekani imemshinikiza Rais wa Congo DRC Joseph Kabila kutangaza kuwa hatogombea tena katika uchaguzi ujao wa Disemba 23.

Hatua hiyo ya Marekani imekuja baada ya mataifa ya Ufaransa na Uingereza kufanya hivyo siku zilizopita.

Wiki iliyopita Kabila alitarajiwa kuwa angetangaza Bungeni nia yake ya kuwania urais wa kuiongoza Congo kwa muhula mwingine tena lakini ameacha watu wakihisi juu ya nia yake.

#My take hii ndiyo dawa kwa madikteta wote barani Afrika wanaozifanya nchi kama mali zao binafsi.
Mbona hao marekani hawamtoi Museveni????????
 
Wamarekani hawaitazami Tz kwa kuwa bado wananufaika nayo,siku Yohana akizingua tu kidogo lamza wamtengenezee zengwe!
 
Back
Top Bottom