Congo, Brazaville: Chama Kikuu cha upinzani kususia Uchaguzi wa Machi 21

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya Congo kimesema kitasusia uchaguzi uliopangwa kufanyika Machi 21. Kwenye uchaguzi huo Rais Denis Sassou Nguesso aliyepo madarakani kwa miongo kadhaa anawania kuchaguliwa tena.

Nguesso mwenye umri wa miaka 77 ameshikilia madaraka kwa miaka 36 sasa na hivyo kuwa mmoja wa viongozi waliodumu kwa muda mrefu madarakani ulimwenguni.

Katibu wa kwanza wa chama cha upinzani cha Pan-African Union for Social Democracy (UPADS) Pascal Tsaty Mabiala amesema kufanyika kwa uchaguzi huo wa urais isiwe sababu ya kuligawanya taifa kama ilivyokuwa zamani na hivyo chama chake kimeamua kutoshiriki katika uchaguzi huo.

Chama hicho cha UPADS cha aliyekuwa rais wa zamani Pascal Lissouba ndicho pekee cha upinzani chenye uwakilishi bungeni. Congo Brazaville imo kwenye mgogoro mkubwa wa kiuchumi uliosababishwa na kushuka kwa bei ya mafuta, deni la muda mrefu pamoja na athari za janga la corona.
 
Huku nako tulitakiwa kufanya hivyo lakini wahuni wachache wakalazimisha kuingia kwenye uchaguzi kichwakichwa wakijua wataukwaa ubunge kiulaini kama enzi za JK
 
Sasa mtu yuko madarakani kwa karibu miongo minne eti bado unaingia naye kwenye uchaguzi halafu mtu mwenyewe ni mweusi kwa rangi, hapo kweli una akili?

Vyombo vyote vinavyohusika na huo wanaouita uchaguzi ni vya kwake na hata hivyo vyombo pia vinaamini kuwa yeye ndiye amewaajiri na sio umma, sasa hapo kuna uchaguzi gani.
 
Back
Top Bottom