Inakuwaje unapokuwa na mume mjeuri ambaye hataki kutoa matumizi ndani ya nyumba kisa tu sababu umemzoeza kutomwomba pesa mara kwa mara sasa anadhani you can manage yourself all household expenses, na si kwamba hana pesa ana kipato kizuri tu kuzidi mkewe. Eti sababu mkewe ana kazi yeye anasema household expenses atoe mwanamke yeye atafanya other things which by the way hazipo coz hajengi, hajanunua gari wala hana mtoto wa kumsomesha coz mtoto bado ni mdogo sana, pia si kwamba anategemewa na familia yake coz wazazi wote wana kazi na wanajiweza. Hata mavazi na mapambo mkewe hujitegemea na hata most of the things ndani ya nyumba vimenunuliwa na mkewe, yani hata mtoto jamaa hata nguo moja hajawahi kununua. Sasa kwenye kasheshe kama hii ambayo kimsingi inamsumbua huyu mwanamke hajui afanye nini kwenye hali kama hii coz jamaa ni expert wa ubishi inakuwaje? Wataalamu hii ni aina gani ya tabia? Or is it right for him to do that? Najua cost sharing ni sawa kabisa, lakini inakuwaje pale mwanamke anapoachiwa afanye kila kila kitu wakati mumewe hakuna anachofanya wala hasemi kama anasave pesa ni kwa ajili ya plani gani? Je ndoa inaweza kushamiri kwenye mazingira ya aina hii ambayo kuna hard feelings kwa mtu anayedhani its not fair at all? jE solution ni nini kwenye hali kama hii? Hali hii inapelekea hata mapenzi kupungua coz wanawake pia wanaongoza kwa kupenda kuona wanajaliwa na wako protected, does it mean mtu wa aina hii hana mapenzi kwa mkewe? ni selfish au mnyonyaji, au nini, its realy confusing jamani, please help