Confirmed: No DECI Refunds | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Confirmed: No DECI Refunds

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kang, May 9, 2009.

 1. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Source: The Guardian
   
 2. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Watu wengine bwana wanasoma magazeti eti confirmed please try to get info from the selected comittee the u come with your story otherwise be calm brother

  FYI DECI wana hela za kutosha kurudishia wateja wake its matter of procedure and gov order(wajiridhishe) sio mambo ya kukurupuka

  News ndio hiyo
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kama mna hela za kutosha si mzirudishe!! Wezi wakubwa nyie!!
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama wana pesa kurudisha mbegu zote....sidhani
   
 5. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  DECI na Malingumu zilitoka wapi? Na je watu hawakujiuliza faida kubwa iliyokuwa inatolewa na makampuni hayo ilikuwa inatoka wapi?

  Ni jambo la kushangaza kuona kuna kampuni nyingi zinazoshughulika na upandaji mbegu (pesa) kama DECI. Jana nilisikia kwenye vyombo vya habari watu kibao wakilia na Malingumu. Je kama wenye kampuni hawana chochote cha kuwalipa waliokuwa wanachama itakuwaje? Inabidi uchunguzi ufanyike hii inaonyesha kuna makampuni mengi mengine kama DECI na Malingumu. Nina imani baada ya muda tutasikia kilio kingine cha watu kutopata mbegu zao walizopanda. Hii inaonyeha kwamba wanachama wanapanda mbegu lakini hawavuni, wanafaidika wenye kampuni hizo uchwara. Tumwombw MUNGU alinusuru taifa letu.
   
 6. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuna nyingine nimesikia radion wakizungumzia asubui clouds ipo Tabata nayewe imefungwa
   
 7. B

  Bata Senior Member

  #7
  May 13, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  inaitwa tumaini
   
 8. R

  Rwey Senior Member

  #8
  May 13, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hizi pyramid scheme zinasababisha watu kutofikiri ktk kufanya production jobs. Zaidi inasababisha mfumuko wa bei (inflations), since lots of money zinawekwa mahali bila kuwa na effective circulation, vile vile zinakuwa under low security (risk). Kwa vile inaonekana kama wanaoendesha hizo sheme hawatumii hizo fedha kugenerate faida zaidi.
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Deci na Tumaini ni wale wale,wizi mtupu.
   
 10. a

  artist Member

  #10
  May 19, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii imechapishwa KULIKONI la leo...  RIPOTI MAALUM...


  Jeetu Patel, Subash, Chavda
  ni pembetatu ya majonzi


  *Walitumia staili ya DECI kuifukarisha nchi
  *Serikali ikatikisika na kuchapa noti mpya
  *Shilingi ikashuka, bei za bidhaa zikapanda
  *Watanzania sasa wahoji tuhuma, si rangi yao


  MWANDISHI WETU
  Dar es Salaam


  MWAKA 1994, kiasi cha miaka 15 iliyopita, mfanyabiashara V.G Chavda na kundi la washirika wake Jeetu Patel na Subash Patel, ambao pembetatu yao ya majonzi KULIKONI linaifichua leo, waliweza 'kupanda' milioni 2.5 tu na 'kujivunia' mamilioni kutoka Serikali ya Tanzania, katika kisa cha ufisadi wa aina yake unaoweza kufananishwa na sakata la DECI lakini mkasa wenye majonzi na machozi kwa Watanzania.


  [FONT=Times New Roman, serif]Watanzania wote wanakumbuka jinsi miaka ya 1990 uchumi wa Taifa ulivyoanguka-shilingi ikashuka thamani na bei za bidhaa zikawa juu lakini sasa imefichuka sababu mojawapo ya hali hiyo ni matendo ya wanamtandao wa pembetatu hii ya wafanyabiashara na sasa wafadhili wa wanasiasa wetu-Jeetu Patel, Subash Patel na V.G Chavda.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Sakata hilo na mkasa wenye majonzi kwa Tanzania linaweza kuelezwa vyema kuanzia miaka ya 1970 pale Chavda, raia wa India na mhitimu wa shahada ya pili kutoka Chuo Kikuu cha Massachusets, Marekani alipoingia nchini, kwa lengo adhimu-kujaribu bahati yake katika nchi hii ya amani.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Chavda ambaye baadaye aliachana na kazi yake ya utaalamu wa uhandisi na kuanza shughuli zake binafsi huku akiombewa kibali kwa nguvu za Ikulu kwa kuelezwa kuwa atakuwa akifanya “kazi nzito nzito za Serikali na mashirika ya umma,” baadaye alijisifu kuwa pamoja na kuingia nchini akiwa kama ombaomba, elimu yake na kusafiri sana kwake 'duniani' kulimpa uwezo wa kuyaona mambo ambayo wengi hawakuweza kuyaona.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Moja ya vipawa alivyojaliwa vya kuona mambo kikajifunua kupitia mpango wa Serikali wa Kuyabadilisha Madeni (Debt Conversion Program), DCP, ambapo Chavda akiwa mwasisi wa nadharia hiyo ya kiuchumi iliyopingwa na wachumi wengi wa Benki ya Dunia na IMF, aliishawishi Serikali ya Tanzania kuyauza madeni yake kwa wawekezaji wa ndani na nje ili wawekeze katika sekta ambazo zingezalisha na kuuza nje ili kuliongezea Taifa mapato ya fedha za kigeni.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Lakini ni ushauri huo kutoka kwa msomi huyo wa Massachusets, kama ilivyokuja kutokea katika sakata la EPA mwaka 2005 (ambapo nako ushauri wa mchumi mmoja mahiri ulizua balaa lote), nako mwaka 1993 Serikali ya Tanzania ilipojikuta ikiuzamisha zaidi uchumi wa nchi hii uliokuwa tayari katikati ya matatizo mambo yalianza kama hivyo.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Haikujulikana kama Chavda, Jeetu Patel na Subash Patel walifahamiana kabla ya kukutana Dar es Salaam au la, lakini kilicho dhahiri mpaka sasa na ambacho Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi iliyochunguza sakata hilo mwaka 1994, ikiwa chini ya aliyekuwa mbunge wa Rorya, Edward Ayombe Ayila, watatu hao waliielekeza Serikali ya Tanzania katika mchezo wa DECI-kupanda na kuvuna, bila yenyewe kujijua.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Alianza Chavda kwa 'kupanda' mbegu zake katika kile Kamati hiyo ilichobaini kuwa ni kiasi kidogo cha milioni 2.5/- tu akinunua moja ya madeni hayo na kuasisi mzunguko mkubwa wa aina ya DECI ambapo baadaye jumla ya kampuni 82 (nyingi mpaka sasa wamiliki wake hawajafahamika) nazo 'zikapanda' kiasi cha bilioni 3 tu na kujivunia Serikalini zaidi ya bilioni 50/- ambazo Serikali ililazimika kuzilipa kwa kuchapisha noti mpya hali iliyougharimu uchumi wa Taifa![/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Akieleza kuwa fedha hizo angezitumia kuwekeza kwenye miradi ya kilimo kwenye mashamba ya mkonge kupitia kampuni zake za alizozisajili haraka haraka za Tanfarms Ltd, Makinyumbi Estates Ltd, Centrepoint Investments Ltd na Arusha Farms, Chavda kwanza alianza 'kupanda' kwa kuyanunua mashamba hayo kutoka Serikalini kwa jumla ya milioni 15/- tu (ambazo zililipwa kwa awamu saba) vikiwemo vyote vilivyokuwa ndani ya mashamba hayo zikiwemo mashine mbalimbali na majengo![/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Kisha baada ya kuyanunua kwa bei hiyo chee, Serikali ikamlipa Chavda fidia ya milioni 100/- kwa kupitisha tu baadhi ya nguzo za umeme na barabara katika kijisehemu tu cha mashamba hayo.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Baada ya kumiliki mashamba hayo ndipo 'upandaji' na 'uvunaji' ukaanza rasmi, akianza kwa kuchota 916,755,147.60/- mwaka 1990 kutoka Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini wakati huo (CRDB) ikiwa ni mkopo kwa ajili ya kununulia mitambo tu ya kuwekeza katika mashamba hayo. Mkopo ambao hadi Chavda anatimuliwa nchini mwaka 1994 haukuwa umelipwa hata senti![/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Kutoka mkopo huo, Chavda akaingia katika DCP (fedha ambazo kwa sasa ndio zimewekwa katika akaunti ya EPA) ambako ikichukuliwa yeye ndiye aliyeasisi mkakati huo kupitia kwa mwanasheria wake Nimrodi Mkono, alinunua deni la milioni 2.5/- tu na kuingiziwa jumla ya milioni 661/- ambazo tofauti na masharti ya malipo hayo-kuwekeza kwenye kuboresha kilimo cha mkonge kwa kupanda mazao mapya na kuyahudumia hadi yatakapouzwa nje ya nchi na kulipatia Taifa fedha za kigeni, lakini badala yake Chavda akaingia katika pembetatu ya aina yake na washirika wake, Subash Patel na Jeetu Patel.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Badala ya kuwekeza katika mashamba ya mkonge Chavda akawalipa Subash na Jeetu malipo tata kwa madai kuwa “walimpa huduma mbalimbali” ambazo hata hivyo ushahidi wao haujapatikana mpaka sasa.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Kwa mfano Subash ambaye naye baadaye 'akapanda' moja kwa moja kwenye mpango huo na kuvuna jumla ya bilioni 6. 98/- (kupitia kampuni zake za Deco Arts, Hotel Sea Cliff, M.M Motors na M.M Garage) ambazo haijajulikana alizifanyia nini, bado alinufaika kutoka fedha alizolipwa 'kaka' yake (Chavda) kwa kuingiziwa malipo tata ya jumla ya 515,995,375/- kati ya milioni 661/- alizolipwa Chavda.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Naye Jeetu Patel kupitia kampuni zake za Azania, Agricultural Enterprises, Liberty Leather Shoe Ltd, Azania Eximco na kadhalika, alithibitisha kupokea 82,295,000/- vyote vikithibitika kuwa ni uongo kwa mujibu wa wachunguzi wa Serikali.[/FONT]

  [FONT=Times New Roman, serif]Malipo hayo ingawa Chavda alidai kuwa ni ya vifaa na utaalamu ambao Subash na Jeetu walizipa kampuni zake za mkonge, wote watatu walishindwa kuonesha ushahidi mbele ya kamati hiyo ya Bunge walipotakiwa kuthibitisha kwa nyaraka “huduma” au “biashara” waliyoifanya na badala yake wakaikacha Kamati hiyo kwa visingizio vya kisheria katika barua zao mbili ambazo mfululizo wa maelezo ya kutotaka kuhojiwa ulikuwa ukifanana kama vile umeandikwa kutoka ofisi moja na mtu mmoja.[/FONT]


  “[FONT=Times New Roman, serif]Subash Patel na Jeetu Patel wamejipatia jumla ya 661,274,660/-. Fedha hizi wamezipata bure bila kutoa huduma yoyote. Wala hawakuzilipia fedha hizo kodi ya mapato. V.G Chavda ameifanya Tanzania kama ni shamba lake la kuchuma. Watanzania ni vibarua wake. Ama kweli wajinga ndio waliwao...,” imehitimisha sehemu ya ripoti hiyo ya Apiyo ikimnukuu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo Augustine Lyatonga Mremba ambaye naye alilivalia njuga sakata hilo na kufanya uchunguzi wake uliobaini makubwa.[/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]KULIKONI limebaini kuwa kupitia mpango huo wa Chavda uliozinufaisha kampuni 82 nyingi zikiwa wamiliki wake hawajulikani, Serikali ilitikisika mno hali iliyosababisha athari kubwa katika uchumi wa Taifa ambao ulielezwa hivi kwa maneno ya Kamati yenyewe:[/FONT]
  “[FONT=Times New Roman, serif]Kwa kipindi hicho cha miaka miwili na nusu ambacho programu hiyo iliendeshwa jumla ya kampuni 82 zilipata vibali vya kununua madeni yenye thamani ya jumla ya bilioni 3.038/- nazo zikalipwa na serikali Bilioni 50.877/- sawa na asilimia 18.02% ya bajeti ya matumizi ya kawaida.[/FONT]


  “[FONT=Times New Roman, serif]Hii ina maana kuwa Serikali ililazimika kuchapisha fedha kiasi cha Tshs. Bilioni 48 kufidia pengo! Inakadiriwa kuwa hadi Serikali ilipoamua kusimamisha programu ya DCP, Juni 30, 1993, madeni hayo yalishaliathiri Taifa kwa kuongeza mfumuko wa bei kwa asilimia 15 huku madeni hayo yakiwafaidisha wafanyabiashara wachache.” [/FONT]


  [FONT=Times New Roman, serif]Kwa ufisadi wa aina hii KULIKONI linahoji Watanzania wanapodai utajiri wa Taifa lao uliopokwa kwa mbinu ambazo zinajirudia kila baada ya muda, watalaumiwa kwa ubaguzi wa rangi?[/FONT]
   
 11. M

  Mr II Senior Member

  #11
  May 19, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Asante kwa makala hii. Kinachotokea hapa TZ hakitofautiani sana na yanayotokea Kenya, Uganda na nchi zingine za Afrika. kuna mtu mmoja wiki mbili zilizo pita alitoa ulinganishi wa kashfa hizo za ufisadi zilivyotokea Kenya na TZ. Hivyo tujue hawa jamma kila unapowagusa kwa madhambi ya ufisadi watakwambia wewe mbaguzi wa rangi au unataka kugombanisha watu au unataka kuleta vita. Ni kwa bahati mbaya huu mchezo unafanya na hawa jamma ambao ni wahindi wakishilikia na viongozi wetu wasio na uchungu na nchi yetu. Hapa tunapiga vita ufisadi na si uhindi au weusi. Ni bahati mbaya sana kwamba hawa jamma ni wajanja sana, wao ili kuhakikisha watakuwa salama kila nchi walipo huwa karibu sana na tabaka tawala na pia hufadhili vyama vya siasa hasa vilivyo madarakani. Ndio maana utashangaa utakapo waambia kuhusu tuhuma hizo usishangae kiongozi furani toka serikalini au chama tawala hutokeza kuwatetea. Ufisadi upo nchi zote duniani. Tunachotofautiana kati ya nchi kama TZ na nchi zilizo endelea ni ule utashi wa kisiasa na ali ya kupigana nao kwa moyo mmoja (Political will and commitment to fight corruption) wenzetu hawana mchezo na hilo.Suala la Kampuni ambayo wakurugenzi hawajulikani ni kichekesho. Katika nchi zilizo endelea wapo makini huwezi fungua kampuni bila vitambulisho kamili. Hatuwezi walaumu sana BRELA kwa hili kwani mpaka leo nchi hii hatuna National ID labda zoezi la ID likikamilika watakuwa makini. Nomba tuendelee na mapambano mpaka wajue TZ sio shamba la bibi tena.
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Artist Sant sana kwa hoja kali
  Nimeisoma naona hasira zimenipanda na ungeona ninavyotaipu hapa we acha tu.

  Kama ushahidi wa kimazingira uko wazi hivi, dola inangoja nini kuchukua hatua?
   
 13. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #13
  May 19, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna thread ilishawahi kutumwa hapa JP kwamba wahindi ni mafisadi iila kuna baadhi ya watu wakiipinga kwa nguvu zao zote,hawa watu ndio waliosababisha leo hii watanzania tunaishi maisha magumu,sasa nachoomba mwakani hakuna kumpa ubunge muhindi yoyote
   
 14. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,840
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  kumbe nchi ilishaporwa siku nyingi... hapo kuna Rais, Serikali, UWT na wananchi wote wamekubali kuliwa sasa tufanyeje? inatakiwa tubaki kimya...
   
 15. S

  Sauti ya Simba Member

  #15
  May 19, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya revelations kama hizi serikali inasemaje? Inawezekanaje wahalifu wa aina hii wakawa bado wapo uraiani as if nothing happened? Mie nakumbuka kwa uchungu sana jinsi nchi yetu ilivyoyumba miaka hiyo. kumbe ni kutokana na hawa wahindi! nadhani hii sasa imetosha! iwapo serikali haitawakamata mafisadi hawa, nguvu ya wananchi itatumika.
   
 16. m

  mnozya JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Imekaa ofisini imetulia inangoja wananchi watafute ushahidi halafu wapelekewe NA OLE WAKO LION NA TARIK AZIZI WAKUSIKIE.
   
 17. H

  Hongasuta Member

  #17
  May 19, 2009
  Joined: Sep 10, 2006
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina shaka Sophia Simba na George Mkuchika wamesoma hii na sana wamemuelewa Reginald Mengi alipozungumzia 'mafisadi papa'. Hapa hatuzungumzii wahindi bali mafisadi! Jamani Watz tutaendelea kuwachekea mafisadi hawa mpaka lini? Hivi tumekuwa mataahira kiasi hiki? Tunapaswa kuamka na kusema 'sasa imetosha'!
   
 18. H

  Hongasuta Member

  #18
  May 19, 2009
  Joined: Sep 10, 2006
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru sana kwa taarifa kama hizi kwani ndio zinatufumbua macho. Labda zitasaidia pia kuwabadilisha watawala wetu ambao wanaonekana kuwakumbatia mafisadi.
   
 19. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mafisadi na vibaraka wao wasome na kutafakari habari hii,na wanaotaka tufunge midomo wasome alama za nyakati.
   
 20. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kwani Wahindi wanagombea Ubunge kulinda utajiri wao.Wabaki kufanya biashara halali na wawekeze si kupangisha tuu.
   
Loading...