Elections 2010 CONFIRMED: Lissu atangazwa mshindi rasmi!

Ibra Mo

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
793
101
Source: Dorice Meghji
TBC1 Reporter


Tundu Lissu kapata kura 13,787 na Mgombea wa CCM -12,161

These are the bestiest results for me kwa ambao hawamjui huyu Jamaa wataiona shughuli yake Dodoma.
 
Tundu Lissu ni kama wabunge wote wa CCM sasa hapa jamani bunge limekaa sawa kabisaaaaaaaa. Mafisadi mavi debe sasa hivi. Uspika tunauchukua pia.
 
baada ya kubana saaaaaaana hatimaye Chi Chi em wameachia na mpiganaji namba moja na mrithi wa Dr. Slaa bungeni anatinga rasmi mjengoni. Nahisi sasa hivi wizara na idara mbalimbali serikalini zinaweka sawa mafaili yao because we voted in quality instead of quantity!
 
...kwa hiyo enzi hizo ulikuwa unaweza kushinda hata kura zisitoshe? Maana unadai hii mara ya pili kushinda. Vipi Mzee wa LEAT, Mwanasheria kweli wewe?

Ndugu yangu kusema kuwa kura hazikutosha ina maana kwamba hakushinda. Sasa mbona unazungumza kwa jaziba. Uanasheria wangu hauna mashaka yoyote labda tu unaweza ukatafuta jina langu kwenye google itakusaidia kunijua mimi ni nani. Sitaki nikufanyia kazi ya utafiti kwani nilitegemea ungechunguza kwanza kabla ya kusema.
 
Huyu jamaa ishu za EPA, Kiwira, Richmonduli, Tundu la choo@ Tsh 700 mil, Matumizi ofisi ya Spika, Ulaji mkubwa wa fedha za Bush nk vipo kichwani, walwahi Majambazi yana kazi!
 
Hizo ndo quality tunazozitaka bungeni na sio Quantity za magabachori kama Rostam Azizi, dewiji na wasinziaji wengine bungeni
 
Yule mbunge wa ccm - Nyalandu wa Singida kaskazini ni tapeli amekuwa akiwadanganya wananchi tangu miaka 10 iliyopita lakini nashangaa wanaendelea kumchagua! Wananchi wa hilo jimbo wanadhihirisha umbumbumbu wao, acha iendelee kula kwao.
 
E ee! Bwana eeh!
Wacha utani mbele ya kazi. Hivi hii ni kweli au vipi?!?!:clap2:
Naona kama Gabriel kanitonya kwamba nisiwe na hofu nikifa sit yangu iko reserved kule peponi??

Naona ndugu Mikataba ya Madini akiwa katika Machela kuelekea chumba cha Upasuaji huku Tabibu mkuu wa Kansa inayomsumbua ndugu Mikataba, Surgeon Lissu akiwa tayari kavalia rasmi mavazi ya Suggery Room tayari wkati wowote kuondoa kansa yote ndani ya ndugu Mikataba ambayo imekuwa ikimsumbua kwa miaka kadhaa sasa.


Kwa mbali nawaona JK,Karamagi,Lowassa na waraba viatu wao wakiteta vichwa wamejiinamia kila mmoja mkono mmoja umeshika kidevu na mwingine ukiwa kifuani sijui wanauhusiano wa karibu na Ndugu Mikataba ya Madini???
Japo mara ya mwisho nilipoangalia Biography ya ndugu Mikataba, Ndugu Mikataba Ya Madini hana ndugu yeyote wa karibu zaidi ya Ndugu Umma na Ndugu Jamhuri ambao muda wote wamekuwa wakisema hawana tatizo kabisa na ndugu Mikataba kufanyiwa Suggery.
 
lisu nimjuae mimi na watz wenye uelewa wa kizalendo ni mbadla tosha wa slaa,slaa mzee wetu sasa chanja mbuga na operesheni sangara hadi 2015,
 
yeah mkuu hii ameitoa Dr slaa wa ukweli kwenye link yake facebook. Huyu bwana thithiemu wasingependa kumuona bungeni but itawabidi wakubaliane na matakwa ya wananchi. Ni slaa mwingine mjengoni!
 
mOJA ya habari njema kuzisikia..tusubirie vibweka wakati wa kuapishwa tu!!
 
mbona ni tangu mchana!! hebu fuatilia thread nyingine ndo mtaridhika..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom