CONFIRMED: January Makamba kugombea Bumbuli

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
313
7
January makamba yupo soni, lushoto, jimbo la bumbuli (linaloshikiriwa na shelukindo) leo hii akijinadi kwa wapiga kura.

January ambaye alishaanza kujitangaza jimboni humo kwa kumwaga pesa na pikipiki za kampeni leo aliwasubiri watu wa soni wamalize kuswali ili apate nafasi ya kusalimia, lakini kitendo hicho kilichukiwa na wengi na wengi kuondoka bila kutaka kumsikiliza.

Jioni hii anaenda kutembelea shule mpya ya waislamu ambapo mwanzo alichangia shilingi laki moja ya ujenzi.

Safari ya january imekumbwa na vikwazo vingi kwani amekuwa akipata mapokezi mabovu moja ni vijana kukataa vifaa vya michezo kama jezi na kumuambia hawahitaji.....

Mapokezi haya mabaya ya January ambaye anasema ametumwa na rais kuchukua jimbo hilo, yanasababishwa na chuki waliyokuwa nayo wananchi dhidi ya baba yake mzee Makamba ambaye mara ya kwanza naye alitimuliwa na wananchi alipojaribu kumnadi kijana wake....

Wengi wamekuwa wakisema January hajulikani na si mwenyeji wa eneo hilo japo baba yake ni mkazi na alishawahi kugombea jimbo hilo zaidi ya mara 2 na kushindwa.

Wadau wanasema january atatumia jeri ya pesa, wakati wananchi wanasema hawadanganyiki tena......

Mzee Shelukindo nae amekuwa akizomewa kila anapokwenda jimboni, wananchi wamemuambia basi kwa kuwa kwenye kampeni za 2005 yeye na mke wake waliomba na kuahidi ingeuwa ni awamu ya mwisho hatagombea tena pamoja na kutofanya lolote jimboni humo.......

Naona wana-JF wameshaanza kujitokeza..... Tumuunge mkono January!?

Ningefurahi kupata uchambuzi yakinifu kutoka kwa wazoefu hapa jamvini.....
 
Januari Makamba ni Mtanzania kama Mtanzania mwingine yeyote na ana haki zake za kikatiba kugombea nafasi yeyote. Kuweka kichwa kuwa mtoto wa makamba una nia mbaya. Sema tu Januari Makamba.

Tusinyime watu haki zao za kikatiba kwa kuwa tu wamezaliwa na fulani. Akifanya rafu tutadeal naye, lakini kuna ubaya gani yeye kugombea? Baba yake aligombea mwaka 1995 na akanyimwa kura za maoni za CCM huko Bumbuli. Naye pia kama hana mikakati itakuwa hivyohivyo
 
Like father like son. Ni mzee Makamba mwenyewe aliyewahi kusema eti watoto wa viongozi ndio wanastahili kuchukua uongozi na kwamba kama baba yako ni mfagizi au kinyozi basi na wewe mtoto utaishia kuwa mfagizi au kinyozi.

Endapo tunaamini mtoto hurithi toka kwa baba, then huyu January pia hana sifa za uongozi kama ilivyo kwa baba yake. Na kama baba aliwahi kushindwa kwenye jimbo hilo hilo, sasa mtoto atawezaje? It's pure logic.
 
ninachopingana nacho mimi sio january na watu wengine kugombea, ningependeza vizazi vikipishana kiuongozi! Sio makamba in power then another makamba is vying. Leo tuna kikwete Rais, basi mtoto naye - watoto nao, kaka, mdogo, mke naye. hiyo ni siasa na inaheshima yake inahitaji mtu aliye jituma sio anayefuata baba anilinde! kama mtoto anaubavu asubiri baba amalize kipindi then njoo kama mwanasiasa.

huo ni woga wa siasa na ndo kisa cha ufisadi na vigugumizi vya kutoa maamuzi, kwa vile kila mtu amebebwa na aliye mbeba ndo fisadi. what do u expect?

heshima naitoa kwa moderator
 
.....Hakuna ubaya wowote kwa yeye kujitangaza, hata kama anataka kuwa mbunge ni sawa wampe ubunge kama ni sifa anazo.
Tusisilalamike hapa kwa kuwa ni mtoto wa Makamba, hata wewe unaweza kwenda kwenu kugombea ubunge kama sifa unazo.
 
Like father like son. Ni mzee Makamba mwenyewe aliyewahi kusema eti watoto wa viongozi ndio wanastahili kuchukua uongozi na kwamba kama baba yako ni mfagizi au kinyozi basi na wewe mtoto utaishia kuwa mfagizi au kinyozi.

Endapo tunaamini mtoto hurithi toka kwa baba, then huyu January pia hana sifa za uongozi kama ilivyo kwa baba yake. Na kama baba aliwahi kushindwa kwenye jimbo hilo hilo, sasa mtoto atawezaje? It's pure logic.

Tumjadili Januari kama mtu anayejitegemea,Hatutokuwa tunamtendea haki Januari kama tutakuwa tunamuhusisha na kauli za Baba yake (Mzee Yusuph).Januari ana haki kikatiba kugombea Ubunge!Tumpe ushirikiano kama mwenzetu baada ya kumkatisha tamaa.
 
..kwenye mahojiano yake na Blog ya Mohamed Dewji alitoa "hint" kwamba ana mipango ya kugombea ubunge.

..labda JK ana mipango ya kumteua January kuwa Waziri ukizingatia ile ahadi yake kwamba ana mipango ya kuongeza vijana ktk cabinet yake.

..kwa upande wangu, ningependa kuona kijana msomi kama huyu akiwa ni back bencher wa CCM ili atoe changamoto kwa serikali goigoi ya CCM.
 
Mleta habari umeingiza ushabiki mwingi mwishoe umemhukumu kuwa hafai.

Tuwaachie wananchi wa Bumbuli wachague wamtakae Januari apimwe kama Januari na si vinginevyo
 
Like father like son. Ni mzee Makamba mwenyewe aliyewahi kusema eti watoto wa viongozi ndio wanastahili kuchukua uongozi na kwamba kama baba yako ni mfagizi au kinyozi basi na wewe mtoto utaishia kuwa mfagizi au kinyozi.

Endapo tunaamini mtoto hurithi toka kwa baba, then huyu January pia hana sifa za uongozi kama ilivyo kwa baba yake. Na kama baba aliwahi kushindwa kwenye jimbo hilo hilo, sasa mtoto atawezaje? It's pure logic.

NO NO NO NO NO NO. Huu hauwezi kuwa uchambuzi makini. Tusianze majungu hapa JF. Leteni facts. Mtoa mada anasema je! tumuunge mkono January Makamba. hapo ndipo naanza kuona kupotoka kwa mawazo. Kwani sisi wote wana JF tupo katika jimbo hilo, au sote tuna msimamo sawa wa kutazama mambo? Hapana, hapo sikubaliani!!

January Makamba, kwanza ana umri gani? Je! Ni chini ya miaka 18?. Kama si chini ya miaka 18, ni mtu mzima sasa. Baba yake kuwa Katibu Mkuu wa CCM haimaanishi kwamba anayoyafanya baba yake, Mzee Makamba, na January atayafanya. No No No wapendwa!!. Ila kama ameanza kutoa rushwa na mambo mengine machafu, hapo kweli wananchi wamchuje!. Lakini, tusifike mahali tukaanza kusema watoto wa viongozi waliopo nao ni wabaya, hata kama baba zao wame prove failure!!.

Nadhani, nimwonye January , kama kweli ameanza huo uchafu, ulioelezwa na mtoa mada, basi, atajichafulia bure. Watanzania wengi tumevua miwani, tunaona vyema. Lakini kama ni majungu, asonge mbele, apeleke changamoto.
 
..kwenye mahojiano yake na Blog ya Mohamed Dewji alitoa "hint" kwamba ana mipango ya kugombea ubunge.

..labda JK ana mipango ya kumteua January kuwa Waziri ukizingatia ile ahadi yake kwamba ana mipango ya kuongeza vijana ktk cabinet yake.

..kwa upande wangu, ningependa kuona kijana msomi kama huyu akiwa ni back bencher wa CCM ili atoe changamoto kwa serikali goigoi ya CCM.

Foreign Minister in the making...........
 
Tumjadili Januari kama mtu anayejitegemea,Hatutokuwa tunamtendea haki Januari kama tutakuwa tunamuhusisha na kauli za Baba yake (Mzee Yusuph).Januari ana haki kikatiba kugombea Ubunge!Tumpe ushirikiano kama mwenzetu baada ya kumkatisha tamaa.
Mara nyingi watu waliopanda kazini kutumia migongo ya baba au ndugu zao hawaoni ufisadi wa kisiasa unaofanywa na viongozi wa CCM kuwaprop watoto wao ili baadae wawalinde na uvundo watakaouacha. January Makamba anataka kutumia ukaribu wa baba yake kwa Rais[ ambao ndio umempatia kazi Ikulu] kama ndio nguzo yake ya kupatia Ubunge pamoja na support ya mafisadi papa[ through watu kama GT] ; hii ni weakness on his part or you could call it political opportunism ambayo watu wasiokuwa na SPINE ndio wanaitumia. If January is man enough na dada yake woman enough wangoje baba yaoa ondoke CCM halafu waingie ulingoni kutafuta Ubunge tuone kama watafua dafu!!
 
WAKUU HESHIMA MBELE.

Mh. Makamba alishawahi kusema "MTOTO ALIYEZALIWA KATIKA NYUMBA YA JIZI LAZIMA ATAKUWA JIZI TU HATA AJIFINYANGEFINYANGE". Nadhani alipokuwa anayasema haya hakujua kwamba ipo siku itafika, mmoja kati ya wanawe atajikuta akiutaka uongozi. Kwa maana hiyo, pamoja na kwamba Januari ana haki ya kikatiba kugombea aina yoyote ya uongozi, lakini hatufai kwa sababu alizozisema baba yake. Sina haja ya kueleza sifa na aina ya uongozi aliokuwa nao baba yake kwani kila Mtanzania anamjua na ndiyo maana tulumkataa kwenye kura za maoni mara mbili alipokuja kutuomba ili awe mbunge wa kuchaguliwa jimboni kwetu.

Bahati nzuri sana tukiwa wadogo niliwahi kuisha nao hawa watu mjini Tanga, wakati baba yake akiwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini. Unavyo waona hivyo ndivyo walivyo na ndivyo watakavyo kuwa.

Bumbuli tunasema hatumtaki kama tulivyo mkataa baba yake, vinginevyo angojee vya kupewa kama dingi.
 
January makamba yupo soni, lushoto, jimbo la bumbuli (linaloshikiriwa na shelukindo) leo hii akijinadi kwa wapiga kura.
January ambaye alishaanza kujitangaza jimboni humo kwa kumwaga pesa na pikipiki za kampeni leo aliwasubiri watu wa soni wamalize kuswali ili apate nafasi ya kusalimia, lakini kitendo hicho kilichukiwa na wengi na wengi kuondoka bila kutaka kumsikiliza.
Jioni hii anaenda kutembelea shule mpya ya waislamu ambapo mwanzo alichangia shilingi laki moja ya ujenzi.

Safari ya january imekumbwa na vikwazo vingi kwani amekuwa akipata mapokezi mabovu moja ni vijana kukataa vifaa vya michezo kama jezi na kumuambia hawahitaji.....

Mapokezi haya mabaya ya january ambaye anasema ametumwa na raisi kuchukua jimbo hilo, yanasababishwa na chuki waliyokuwa nayo wananchi dhidi ya baba yake mzee makamba ambaye mara ya kwanza naye alitimuliwa na wananchi alipojaribu kumnadi kijana wake....

Wengi wamekuwa wakisema january hajulikani na si mwenyeji wa eneo hilo japo baba yake ni mkazi na alishawahi kugombea jimbo hilo zaidi ya mara 2 na kushindwa.

Wadau wanasema january atatumia jeri ya pesa, wakati wananchi wanasema hawadanganyiki tena......

Mzee shelukind nae amekuwa akizomewa kila anapokwenda jimboni, wananchi wamemuambia basi kwa kuwa kwenye kampeni za 2005 yeye na mke wae waliomba na kuahidi ingeuwa ni awamu ya mwisho hatagombea tena pamoja na kutofanya lolote jimboni humo.......

Naona wanajf wameshaanza kujitokeza.....je tumuunge mkono january???

Ningefurahi kupata uchambuzi yakinifu kutoka kwa wazoefu hapa janvini.....
safii watu wanapata mwamko sasa! wanathani watawanunua kila wananchi siku zote!
 
Tumpe ushirikiano kama mwenzetu baada ya kumkatisha tamaa.

Unajua wewe Mwawado mchemfu sana wewe. Sasa huyo Januari amekuwa "mwenzetu"? Ni "mwenzetu" kivipi? Wewe ni bendera fuata upepo kama avatar yako. Upo upo tu..
 
WAKUU HESHIMA MBELE.

Mh. Makamba alishawahi kusema "MTOTO ALIYEZALIWA KATIKA NYUMBA YA JIZI LAZIMA ATAKUWA JIZI TU HATA AJIFINYANGEFINYANGE". Nadhani alipokuwa anayasema haya hakujua kwamba ipo siku itafika, mmoja kati ya wanawe atajikuta akiutaka uongozi. Kwa maana hiyo, pamoja na kwamba Januari ana haki ya kikatiba kugombea aina yoyote ya uongozi, lakini hatufai kwa sababu alizozisema baba yake. Sina haja ya kueleza sifa na aina ya uongozi aliokuwa nao baba yake kwani kila Mtanzania anamjua na ndiyo maana tulumkataa kwenye kura za maoni mara mbili alipokuja kutuomba ili awe mbunge wa kuchaguliwa jimboni kwetu.

Bahati nzuri sana tukiwa wadogo niliwahi kuisha nao hawa watu mjini Tanga, wakati baba yake akiwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini. Unavyo waona hivyo ndivyo walivyo na ndivyo watakavyo kuwa.

Bumbuli tunasema hatumtaki kama tulivyo mkataa baba yake, vinginevyo angojee vya kupewa kama dingi.

Leteni uozo wake hapa udadavuliwe! Close family member kaleta vitu!
 
.....Hakuna ubaya wowote kwa yeye kujitangaza, hata kama anataka kuwa mbunge ni sawa wampe ubunge kama ni sifa anazo.
Tusisilalamike hapa kwa kuwa ni mtoto wa Makamba, hata wewe unaweza kwenda kwenu kugombea ubunge kama sifa unazo.

Dear Pretty, politics is not as innocent as you look (based ur picture i see)! Umeona kuwa chipukizi kumekuwa na malalamiko ya rushwa?- hoa watoto wametoa wapi mafungu ya kumwaga? wanayajua hata thamani za hayo mafungu? umeona kuwa ni watoto wa vigogo tu? hadi sheikh anaingilia kati, mtu akigusa tu fomu, to hell! tufike mahala tukubaliane kuwa kama unakubalika, usimpe baba wakati mgumu, mwache apite kipindi chake, tumia muda huo kujifunza then at your own time join the game kivyako uonyeshe misuli yako kisiasa.
 
.....Hakuna ubaya wowote kwa yeye kujitangaza, hata kama anataka kuwa mbunge ni sawa wampe ubunge kama ni sifa anazo.
Tusisilalamike hapa kwa kuwa ni mtoto wa Makamba, hata wewe unaweza kwenda kwenu kugombea ubunge kama sifa unazo.

Tatizo la msingi ambalo aliye post hii thread ameliona ni rafu anazocheza huyo January,kipindi chote alikuwa wapi adi leo ndo aende kutoa takrima!!inaingia akilini kweli hii.
Kama anataka ubunge asubiri wakati muafaka ndo aanze hizo rough zake.
hizi tabia za kutaka kuleta utawala wa kifalme hazitakiwi kabisa..hongera kwa watu wa bumbuli kwa kushtukia janja ya Makamba na mwanae..msichague mtu eti kisa baba yake ana ushawishi ktk serikali..huu nu ujinga na upuuzi..juzi tumeona uchaguzi wa madogo wa CCM ulivyokuwa..watoto wa viongozi eti ndo wameshinda...
Labda CCM ijitangaze kuwa ni chama cha ki ukoo ukoo tutakielewa,lakin kama wao wanatuhubiria kuhusu ubaguzi ilhal wao wanataka kuleta undugu undugu katika chaguzi ni sawa na kutuona watanzania ni wapumbaf..
January kama anataka ubunge asubiri wakati muafaka na aende kwa sera za atawafanyia nini wananchi wa bumbuli na sie et kuwaambia katumwa na Rais kuchukua jimbo...hilo jimbo sio la Rais..ni la wana bumbuli.
 
Acheni longolongo...Inaelekea january ni tishio sana maana akitaka kufanya kitu lazima watuw atake kumpinga kamavipi na wewe basi nenda kagombee kwenye jimbo lenu kani kuna mtu aliyekatazwa...waachieni wananchi wa Bumbuli huko Soni hii issue siyo kukaa na kumdiscuss Next generation leader!!...

Inamaana leo FMES akitoka akasema anagombe jimbo la chamwino mtamkataa kwa sababu ni mtoto wa Malecela?....
 
.....Hakuna ubaya wowote kwa yeye kujitangaza, hata kama anataka kuwa mbunge ni sawa wampe ubunge kama ni sifa anazo.
Tusisilalamike hapa kwa kuwa ni mtoto wa Makamba, hata wewe unaweza kwenda kwenu kugombea ubunge kama sifa unazo.

loh pretty
huu uhaini kabisa;wangapi waanze kupita na kutangaza raisi kawatuma
rais anawezaje kumtuma mtu akagombee ubunge;je kwa akili huu ni muda wa kufanya kampeni??kama wananchi wanaliona hili wako sawa
sikuhizi watanzania wachache ni wadanganyika
 
Acheni longolongo...Inaelekea january ni tishio sana maana akitaka kufanya kitu lazima watuw atake kumpinga kamavipi na wewe basi nenda kagombee kwenye jimbo lenu kani kuna mtu aliyekatazwa...waachieni wananchi wa Bumbuli huko Soni hii issue siyo kukaa na kumdiscuss Next generation leader!!...

Inamaana leo FMES akitoka akasema anagombe jimbo la chamwino mtamkataa kwa sababu ni mtoto wa Malecela?....

Ndio FMES akija kugombea jimbo la Mvumi ambako Malecela aliwahikukataliwa[ kama Makamba alivyokataliwa Bumbuli] na akatanguliza kugawa hela za EPA kutoka kwa mafisadi papa ; kwavile wananchi sikuhizi hawadanganyiki watamkataa baada ya kuvila vijisenti vyake.!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom