MtazamoWangu
JF-Expert Member
- Apr 25, 2009
- 313
- 7
January makamba yupo soni, lushoto, jimbo la bumbuli (linaloshikiriwa na shelukindo) leo hii akijinadi kwa wapiga kura.
January ambaye alishaanza kujitangaza jimboni humo kwa kumwaga pesa na pikipiki za kampeni leo aliwasubiri watu wa soni wamalize kuswali ili apate nafasi ya kusalimia, lakini kitendo hicho kilichukiwa na wengi na wengi kuondoka bila kutaka kumsikiliza.
Jioni hii anaenda kutembelea shule mpya ya waislamu ambapo mwanzo alichangia shilingi laki moja ya ujenzi.
Safari ya january imekumbwa na vikwazo vingi kwani amekuwa akipata mapokezi mabovu moja ni vijana kukataa vifaa vya michezo kama jezi na kumuambia hawahitaji.....
Mapokezi haya mabaya ya January ambaye anasema ametumwa na rais kuchukua jimbo hilo, yanasababishwa na chuki waliyokuwa nayo wananchi dhidi ya baba yake mzee Makamba ambaye mara ya kwanza naye alitimuliwa na wananchi alipojaribu kumnadi kijana wake....
Wengi wamekuwa wakisema January hajulikani na si mwenyeji wa eneo hilo japo baba yake ni mkazi na alishawahi kugombea jimbo hilo zaidi ya mara 2 na kushindwa.
Wadau wanasema january atatumia jeri ya pesa, wakati wananchi wanasema hawadanganyiki tena......
Mzee Shelukindo nae amekuwa akizomewa kila anapokwenda jimboni, wananchi wamemuambia basi kwa kuwa kwenye kampeni za 2005 yeye na mke wake waliomba na kuahidi ingeuwa ni awamu ya mwisho hatagombea tena pamoja na kutofanya lolote jimboni humo.......
Naona wana-JF wameshaanza kujitokeza..... Tumuunge mkono January!?
Ningefurahi kupata uchambuzi yakinifu kutoka kwa wazoefu hapa jamvini.....