Elections 2010 CONFIRMED: Dk. Nchimbi Ashinda Songea

PEDE

Member
Nov 2, 2010
30
0
Baada ya kucheleweshwa kwa muda mrefu kutolewa kwa matokeo ya ubunge jimbo la Songea mjini,hatimaye Dk.Nchimbi atangazwa.
Sina uhakika kama kura hazikuchakachuliwa kama sehemu nyingine.
 
Huwa anajisikia sana Nchimbi na kujiona ana hati miliki ya kuongoza Songea wakati hakuna cha maana lichofanya uko
 
Asante kwa taarifa yako, lakini habari za kuaminika ni kwamba, matokeo yamechakachuliwa sana. Aliyekuwa mshindi ni wa CHADEMA, ila si unajua URANIUM iko huko? Kuna order kwamba hata Jimbo moja lisichukuliwe na upinzani.
 
Kuna mwisho wake,huu ni mwanzo na URANIUM itatufaidisha wote huko mbeleni labda waivune ktk miaka mitano hii iishe.
 
Ulivyotaja uranium umenikumbusha machungu ya jinsi rasilimali za nchi zinavyokwepuliwa na wajanja wachache
 
Huyu anaitwa emanuel nchimbi na sio dr emanuel nchimbi,hana u dr,msanii tu.kachakachua matokeo ndio maana wakaz wa songea mjin wamemuambia wewe sio mbunge wetu kwa kuwa hata madiwan wa kata zote za mjin ni wachadema.
 
Ivi inaingia akilini watu wachague Mbunge CCM alafu kata CHADEMA naona ata hesabu zinawashinda wazee wa kuchakachua
 
Baada ya kucheleweshwa kwa muda mrefu kutolewa kwa matokeo ya ubunge jimbo la Songea mjini,hatimaye Dk.Nchimbi atangazwa.
Sina uhakika kama kura hazikuchakachuliwa kama sehemu nyingine.

Watu kama wewe PEDE ndio mnadhalilisha taaluma za watu; huyu unaemwita "DR" hana heshima hiyo na wewe nadhani mpaka sasa unajua hivyo kwani amechakachua vyeti vyake vya elimu, hivyo nawe kuendelea kumwita hivyo unajidhalilisha kwani itaonekana kama ni mtu wa kujipendekeza, hiyo ikiwa sio sifa nzuri!!
 
Kama ameweza kuchakachua elimu yake ,hawezi kushindwa kuchakachua matokeo ya kura. Hawa ndio Historia itawahukumu na Vijukuu vyao vitachapa makaburi yao
 
Ivi inaingia akilini watu wachague Mbunge CCM alafu kata CHADEMA naona ata hesabu zinawashinda wazee wa kuchakachua

Kama haiingii akilini, Muulize Batilda kule Arusha.

Kimsingi kama mgombea anakubalika kwenye kata yenye wapiga kura wengi, na wakaenda kupiga kura; matokeo ya namna hii kutokea si ajabu.
 
Kama ameweza kuchakachua Elimu yake,hashindwi kuchakachua matokeo ya kura. Historia itamshtaki na wajukuu zake watachapa bakora kaburi lake
 
Watu kama wewe PEDE ndio mnadhalilisha taaluma za watu; huyu unaemwita "DR" hana heshima hiyo na wewe nadhani mpaka sasa unajua hivyo kwani amechakachua vyeti vyake vya elimu, hivyo nawe kuendelea kumwita hivyo unajidhalilisha kwani itaonekana kama ni mtu wa kujipendekeza, hiyo ikiwa sio sifa nzuri!!

Ni Dr wa kuchakachua
 
Inawezekana ni U'Dr' wa kuchakachua kweli!
Ukifika mahala ukakuta mtu anaitwa "Maliyatabu" utajikuta tu unamwita jina hilo na ukiambiwa na wenyeji kuwa hilo sio ljina ake halisia unabadilisha.
Nami nabadilisha;ni Bwana.NCHIMBI na sio Dk.Nchimbi.
 
KATIKA FANI YA UGANGA WA BINADAMU NA WA KIENYEJI KUNA MADAKTARI PIA,NA HATA KUNA MADAKTARI WA FALSAFA WA HESHIMA.HUYE EMANUEL ALIPATA Phd COMMONWEALTH OPEN UNIVERSITY AMBAYO NI DEGREE MILL.HATA WEWE UKITAKA BOYA LA DEGREE UKIWALIPA DOLA KADHAA WATAKUPATIA HIYO.SWAHIBA WAO NI DIODORUS KAMALA,MWINGINE MAKONGORO MAHANGA, MWINGINE PROSPER HONEST NGOWI NA WASANII WENGINE.LA AUBU HAO HAO WEZI WA ELIMU NDIYO WANAMTANDAO NDIYO WASHAURI WA JAKAYA MRISHO KIKWETE,HALAFU UNIAMBIE ETI NCHI ISIYUMBEYUMBE KAMA MLEVI YEYOTE WA POMBE YA MNAZI-AKA TEMBO?
 
Mgombea wa Chadema, Mhe. Mbogoro, anashauriwa apinge haya matokeo Mahakamani. Yeye ni mwanasheria na anajua inaruhusiwa kuchallenge huu uchakachuaji. Itasaidia sana ku-set precedence iwapo hizi mbinu za CCM zitaanikwa na kupigwa marufuku kisheria.
 
Back
Top Bottom