Confession: The hurting truth -- natamani kurudi kwenye ushirikina

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,720
Niliachana kabisa na mambo yote ya kishirikina miezi kadhaa iliyopita, na kuthibitisha hilo niliweka uzi rasmi hapa JF na kumrudia Mola wangu mazima. Na kuna hili ambao sikuwahi kulisema hapa lakini wale ambao niliwaumiza na roho ikaniongoza tusawazishe nilifanya hivyo. Na nikapata amani kubwa moyoni

Naamini nanyi ni mashuhuda wa hili kwakuwa nilipunguza mada za ushirikina kwa asilimia 80 ama 90 hivi. Na kila nilichomiliki chenye viashiria na viasili vya ushirikina ama niligawa au niliviharibu na kuviteketeza kwa moto kwa mikono yangu mwenyewe. Nilihakikisha naishi maisha ya ukamilifu na usafi wa kiroho

LAKINI wapendwa shetani ana nguvu sana sana. Unapokuwa umevaa koti jeupe la mshika dini na asiyependa mambo ya ulozo lakini ndani u mchafu kupitiliza wala sheatani hawezi kukusumbua kabisa lakini once unapomkataa kwa roho na kweli. VITA HUANZIA HAPO! atakujia na washirika wengine SABA kuhakikisha wanakurudisha kwenye himaya yao.

Juzi kati nilikuwa maeneo ya mikwambe Kigamboni kibada mpaka saa tatu usiku hivi wakati naondoka nikagundua kuna watu walikuwa wameniungia body na nilienda nao mpaka Tuangoma halafu wakapotea kusikojulikana

Tangu hapo nimejiwa na msisimko wa ajabu kabisa. Msisimko wa kutafuta zile nguvu za giza tena. Najitambua kiimani na kiroho niko vizuri mno. Lakini sasa naona viashiria vya kunirudisha kilingeni vinazidi kupata nguvu kila uchao.

Tafadhalini naomba msije mkanishangaa in case mkisikia nimerudi Msata Kilingeni penye shina langu. Lakini pia ukiweza na ukipenda kwa utashi wako pls niombee. Kuna shida nyingi huko vilingeni basi tuuu
 
Mathayo 12:43-45

Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
 
Mkuu kuwa makini, Konyagi za siku hizi zimechakachuliwa!

Babu yangu aliniusia, usiamini sana ahadi za wikend
Natumia hii mkuu

IMG-20210912-WA0056.jpg
FB_IMG_1631330087561.jpg
 
Brother hakuna tiba bora kama kufunguka..hukupa nafuu kubwa kiroho... Mapambano ni makubwa nimesimulia kisa kimoja tu na bado napambana!

Kutambua upo kipindi gani na unapitia wakati gani ni muhimu sana kwenye kutafuta suluhu ya jambo lolote.
Haitakua rahisi lakini kuweka wazi inakua kama unazidi kutangaza vita lakini pia inakupa ujasiri wa kuongeza juhudi kuvuka.

Kuna wakati ilikua kidogo niharibu na majaribu ya Boss, nilichokifanya ilibidi nimweleze imeadiate supervisor wangu hali nnayopitia.
Hapo ikawa kama nimejifunga kitanzi, ilibidi nichukue tahadhari zote nisidondoke, kwa sababu hata ningeharibu akaja kusikia, angeshangaa kwanini nilienda kumweleza changamoto wakati nilikua na nia ya kujiingiza kwenye hilo jambo.

Ikabidi nitengeneze mazingira ya kutoruhusu mwanya hata kidogo wa kujikuta naharibu na mkuu wa kazini. Haikua kazi rahisi lakini nashukuru nilivuka, niliamua kuishinda hiyo vita kwenye akili kabla ya kupambana nayo kwenye mwili.
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom