Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,403
- 1,241
Size matters!!
SteveD.
Source: JamboNetwork.comSHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limelazimia kurudisha kondomu zilizoingizwa nchini kutoka Korea baada kondomu hizo kugundulika kuwani ndogo.
Akizungumza katika ziara ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Mtaalamu Mwandamizi wa Maabara wa TBS, Mary Mlembe alisema kuwa kondomu hizo ziliingizwa nchini kutoka nchini Korea zikuwa fupi na hivyo kutofaa wa watanzania.
Mlembe ambaye alikuwa akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu juu ya ubora wa kondomu na jinsi ya kuzifanyia uchunguzi alisema baada ya kufanyiwa uchunguzi kondomu hizo ziligundulika kuwa zilikuwa hazikidhi viwango vya kimataifa vinavyokubalika kwani zilikuwa fupi.
"Kuna wakati TBS tulipokea Kondomu kutoka nchini Korea lakini baada ya kuzifanyia uchunguzi tuligundua kuwa hazikidhi viwango vya kimataifa kwa kuwa zilikuwa fupi ulikinganisha na urefu unaohitajika," alisema Mlembe.
Alisema katika kupima ubora wa kondomu hizo TBS hutumia viwango vilivyowekwa kimataifa ambavyo vinakubalika na nchi mbalimbali.
Alisema kwa sasa viwango vinavyokubalika kimataifa ni urefu usiopungua nchi 160 na kuendelea na upana wa nchi 53 wakati unene unatakiwa kuwa sentimita 0.07.
Hawa watu wanaoleta bidhaa kutoka nje wanafikiri watu wote duniani wana viwango sawa? Labda kama zingekuwa kwajili ya watoto wa shukle za msingi!!!!
SteveD.