Conclusion (Wanawake waliosoma ni wasumbufu) ( wanaume ndo tatizo).

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,114
18,337
HUU NI UWONGO MKUBWA KABISA, TATIZO NI WANAUME

barack-obama-family3.jpgTATIZO NI WANAUME NA SI WANAWAKE.

Kwa nini wanaume wengi wanaamini huu uwongo nab ado hawataki kuelewa.

1. Hofu ya kutokuwa na sauti katika familia kitu ambacho si kweli kwani wanawake waliosoma ni wepesi kumwelewa mtu na kuishi naye kama alivyo.

2. Hawataki kuelewa umuhimu wa mwanamke aliye soma na kama ukiona ndoa inatatizo kwa sababu ya elimu YA MWANAMKE basio ujue mwanaume ndio chanzo cha tatizo kwani mwanaume wa kweli anatakiwa ajue namna ya kuwa kuongoza familia yake katika mazingira yote wakati kila mmoja akifurahia uwepo wake kama baba wa familia.

3. Ni kitu kipya machoni pa wanaume wengi kwani walilizoea kuwa juu katika kila kitu, lakini sasa dunia imebadilika na WAnatakiwa KubadilikA ama sivyo wengi tutapoteza vitu vingi vya uwakilsihi BUNGENI.

4. Wanaume wengi ni waoga mbele ya mwanamke aliye mzidi iwe elimu, pesa, akili darasani (ni mara chache mwanaume kumwuliza msichana amsaidie swali kama hajui), umri etc. na iii imeza inferiority complex.

5. Wanaume wengi si wazuri kwenye mambo ya ndoa hasa katika kujenga mahusiano ambayo yanaweka uhuru, usawa na umoja katika familia. Mawasiliano ndoo kabisa labda wakati wa uchumba. Kupenda sijafuatilia ila inasemekana wanaume hatupendi kwa moyo tunapenda kwa macho ndoo maana kumchoka mke ni rahisi kuliko mke kumchoka mume. Kipo wanacho kijua zaidi sitakitaja hapa.

6. Mitazamo hasi ya wanaume juu ya wanawake.

7. …..
8.......
 
dah umeongea maneno ya xmass...una nguo mpya baba?
umesoma?mi sjasoma so hofu ondoa ..utakuja?
 
Mna tatizo nyie akina mama, dada, wanawake, ukisoma bado unatakiwa umheshimu mumeo. Lakini hamko hivyo naturally huo ndiyo ukweli halisi Divorce rate huongezeka miongoni mwa nyumba za wasomi kwa sababu hiyo. Soma sana lakini assume position yako kama mama wa familia and not otherwise,
 
mwanamke anabakia kuwa mwanamke ata km wamesoma its just men wanaaanza kujishtukia na kuact wild wakiona wamezidiwa na mwanamke iwe elimu pesa au cheo....refer to tabutupu apo juu.....
 
Huyo mwanamke wako aliyesoma kisha akakufanya ukapoteza uaname wako mlete hapa tumpige darasa! Madarasa na ndoa/mahusiano havipaswi kuwa kama maji na mafuta vnatakiwa kuwa kama chanda na pete.
 
Idadi kubwa ya wanawake waliosoma ni ama hawajaolewa au ndoa zao zimevunjika. Na tatizo kubwa ni kwamba wanajidai wanajua sana haki zao na hivyo wanaanza kutaka wafanye mambo at the same level na waume zao. Na mwanaume atakapotafuta kudumisha nafasi yake ya ukichwa wa nyumba ndipo mambo yanapokwenda kombo. Ukitaka uishi kwa amani na mwanamke msomi wewe uwe Bushoke. Osha vyombo, fua, pika, deki, fagia uwanja nk, hapo bwana hutaona mgogoro. Lakini ukitaka ulete ile habari ya umwanaume, hiyo ndoa haitakaa isimame.
Na usiombe awe amesoma zaidi yako, na ana mshahara mkubwa zaidi yako. Haki ya mama kila siku atakwambia yupo busy na kazi za ofisini, kwa hiyo baba ni jukumu lako kulea watoto na majukumu mengine yote ya nyumbani. Nina mifano kadhaa, na hiyo imenifanya nijikute automatically nawakimbia hao watu.
 
SEMA " baadhi ya wanawake waliosoma"................
 
mwanamke anabakia kuwa mwanamke ata km wamesoma its just men wanaaanza kujishtukia na kuact wild wakiona wamezidiwa na mwanamke iwe elimu pesa au cheo....refer to tabutupu apo juu.....

Women have a wonderful instinct about things. They can discover everything except the obvious
 
SEMA " baadhi ya wanawake waliosoma"................

Yah, kweli ni baadhi. Siwezi kusema wote, maana wapo pia wenye shule zao, ni maprofessor lakini wapo kwenye ndoa raha mstarehe. But majority ya hao wasomi wana shida. Na hili si kwa Tanzania tu, hata nchi zilizoendelea 70% ya ndoa zinavunjika, sababu mojawapo ni hiyo. Wanawake wamesoma wanajua haki zao na wana majukumu ya kiofisi sawa sawa na wanaume. Kwa hiyo inafika wakati humo ndani hajulikani baba ni nani wala mama ni nani. Na mwisho wa siku wanaamua kutengana ili kila mtu awe huru kutekeleza majukumu yake ya kiofisi. Huko ndiko tunakoelekea hapa kwetu.
 
Kuna point hapo, wanaume insecurities rahisi sana kujitokeza.
 
Ningependa kusikia kutoka kwa wale wanawake ambao hawakwenda shule. Je wananyanyasika kiasi gani kwenye ndoa zao. Taabu ninayoiona hapa ni kwamba kuna baadhi ya wanaume hawajiamini. Kwa sasahivi dunia inavyokwenda mmke asiyekuwa na elimu hana soko tena. Tubadilike!
 
Idadi kubwa ya wanawake waliosoma ni ama hawajaolewa au ndoa zao zimevunjika. Na tatizo kubwa ni kwamba wanajidai wanajua sana haki zao na hivyo wanaanza kutaka wafanye mambo at the same level na waume zao. Na mwanaume atakapotafuta kudumisha nafasi yake ya ukichwa wa nyumba ndipo mambo yanapokwenda kombo. Ukitaka uishi kwa amani na mwanamke msomi wewe uwe Bushoke. Osha vyombo, fua, pika, deki, fagia uwanja nk, hapo bwana hutaona mgogoro. Lakini ukitaka ulete ile habari ya umwanaume, hiyo ndoa haitakaa isimame.
Na usiombe awe amesoma zaidi yako, na ana mshahara mkubwa zaidi yako. Haki ya mama kila siku atakwambia yupo busy na kazi za ofisini, kwa hiyo baba ni jukumu lako kulea watoto na majukumu mengine yote ya nyumbani. Nina mifano kadhaa, na hiyo imenifanya nijikute automatically nawakimbia hao watu.

Mbona mkiwa mnaishi wenyewe mnafanya hizo kazi....kuna ubaya gani kumsaidia mwenzi wako pindi ukiwa nae???Hayo mawazo ya nikishapata mwenza kazi hizo basi tena ndo zinafanya wengine wanakua na kiburi kwasababu inakua kama umepata mfanyakazi (mtu wakumtumia) kwahiyo haikuhusu tena!!Hamjui tu jinsi yakucheza na akili ya mwanamke.....kama unataka hizo kazi usifanye na bado kuwe na amani jaribu kutokumfanya ajiskie kwamba NI LAZIMA AFANYE hizo kazi ATAKE ASITAKE!!Binafsi mtu akinilazimisha kufanya kitu hata kama nilikua nimeshapanga kufanya sitafanya......yani sipendi kabisa mtu anaponifanya nijiskie kwamba ni lazima nifanye kitu fulani....nitake nisitake!!!

Na hapo kwenye kulea watoto kumbe sio jukuma la baba???Sasa siku zote kelele za nini kuhusu malezi ya baba yalivyo muhimu kwa mtoto kama sio jukumu lenu???
 
Si kweli maisha ya ubachela ya mwanume yanakuwa ya rafu sana na mara nyingi wanakula migahawani/hotelini, usafi wa vyumba vyao ni kulipua mara moja kwa wiki. Nasisitiza kama kweli Mungu yupo, kitu chochote kinyume na malengo ya Mungu kitafanikiwa kwa muda tu na baadaye kitagota tu kama mnara wa Babeli ulivyogota. Kuna msitari kwenye Bible unasema itafika kipindi mwanamke ataomba aolewe na mwanaume ili tu aitwe kwa jina lake, kutimiziwa hisia na heshima ya kuwa mke wa mtu na hapo akiendelea kujitimizia mahitaji yake mwenyewe( nimesahau huo mstari unapatikana kwenye kitabu kipi, samahani). Naamini usomi wa mwanamke na tunayoyaona ni ulimbukeni tu lakini baadaye yatajiweka sawa. Hata wanaume lazima waache kuwatesa wake zao maana si maelekezo ya Mungu.
 
Wanawake wasomi hawaolewi, kiburi,ubishi ndo maana wanazalshwa na mabos na wana2pwa!
Tatizo lipo hapo kwenye fikra mgando. Uliwahi kuwa na mwanamke msomi ukajua kiburi na jeuri yake vinasababishwa na nini? Tatizo wengi hamkubali challenge toka kwa wanawake,mnadhani kutuburuza ni haki yenu,tukihoji tunaonekana wakorofi.
Na ukisema wanazalishwa na mabosi wao halafu wanaachwa unakosea kaka!
Watu wanatafuta mbegu tu sio kusaidiwa malezi maana anajua kabisa yule ni mume wa mtu hawezi kuwa nae permanently! Za nini stress kama unaweza kuziepuka zipishe zipite.
Na hujaona bado kuna wanawake wanawazidi waume zao kipato na elimu na ndoa zao zimetulia wana amani kwa sababu wanaunganishwa na mapenzi sio social status!
Kuna wanaume kibao wanawaacha wake zao wa ndoa nyumbani wanatoka na nyumba ndogo kwenye hafla za ofisi au mialiko. Kisa...mkewe hajasoma hana hadhi atamuaibisha. Yote haya hamjayaona?
Basi tu wanawake tumekua wa kupokea lawama.
 
Si kweli maisha ya ubachela ya mwanume yanakuwa ya rafu sana na mara nyingi wanakula migahawani/hotelini, usafi wa vyumba vyao ni kulipua mara moja kwa wiki. Nasisitiza kama kweli Mungu yupo, kitu chochote kinyume na malengo ya Mungu kitafanikiwa kwa muda tu na baadaye kitagota tu kama mnara wa Babeli ulivyogota. Kuna msitari kwenye Bible unasema itafika kipindi mwanamke ataomba aolewe na mwanaume ili tu aitwe kwa jina lake, kutimiziwa hisia na heshima ya kuwa mke wa mtu na hapo akiendelea kujitimizia mahitaji yake mwenyewe( nimesahau huo mstari unapatikana kwenye kitabu kipi, samahani). Naamini usomi wa mwanamke na tunayoyaona ni ulimbukeni tu lakini baadaye yatajiweka sawa. Hata wanaume lazima waache kuwatesa wake zao maana si maelekezo ya Mungu.
Kwasababu tu ni rafu haina maana hayo hayafanyiki!!Sasa hiyo mara moja kwa wiki akaihamishia kwenye kumsaidia au hata kuonyesha tu nia yakumsaidia mwenzi wake kuna shida gani???Ndo yale yale ya nimekupata sasa siwezi kufanya kazi za nyumbani tena....get to work!!:teeth:
 
Ndugu yangu ndio maana nimesema wanaume nao waache ubabe, kinacholeta shida sasa ni ile hali ya kubeba habari za akina Annanilea Nkya Tamwa, Tawla kwa kupitiliza kiwango na kuzileta nyumbani kwa mume wako, ukweli ni kwamba katika mahusiano yoyote ili yadumu lazima mmoja ajishushe angalau kidogo( ukipata mme wa kujishusha ni bahati pia), haiwezekani katika nchi wote mkawa marais na hapo hapo wote mkawa raia.
 
Back
Top Bottom