Computer Yako Iko Hatarini

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Komputer yako lazima iwekewe updates za kisasa , iwekewe antivirus pamoja na updates zake bila kusahau firewall , windows xp service park 2 inakuja na service park yake ingawa haikuhakikishii usalama sana kama haina angalau vitu hivyo 3 kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa computer yako kuvamiwa au kushambuliwa kama imeunganishwa katika mtandao au hata kama haijaunganishwa .

MTANDAONI

Sasa hivi wengi tumeunganishwa katika mtandao na wengi zaidi wanazidi kuhamisha shuguli zao kwa njia ya mtandao au kutegemea zaidi mtandao kwa shuguli zao , kama kusoma email , kutembelea tovuti , manunuzi ya vitu , kuongea na mambo mengine mengi sana .
Kama nilivyosema hapo mwanzo kuunganisha computer yako katika mtandao unakuwa na nafassi kubwa zaidi kushambuliwa , katika dunia ya mtandao password pekee hazitoshi bila kuchukuwa hatua nyingine nzuri na rahisi zaidi .

UTAVAMIWA KAMA

- Ukifungua attachment yoyote ambayo hujui inahusu nini au chanzo chake .
- Kama ukiamini kila kitu unachosoma katika mtandao ni mali mfano ahadi za utajiri kama ukifungua attachement au tovuti Fulani
- Ukidownload programu ya ajabu kutoka katika mtandao kama screenserver za bure , games , picha na vingine vingi
- Kushiriki au kushirikiana na wengine data zako kwa programu za peer to peer kama kazaa , wares , au ares
- Ukishirikiana password yako na watu wengine


VITU VYA KUFANYA USIVAMIWE KWA URAHISI

- Hakikisha antivirus yako iko updated na saa zote iwe inafanya kazi
- Ujenge mazoea ya kuweka updates hizi zinapatikatika bure katika tovuti ya Microsoft au zile zinazohusika na programu unayoitumia . kumbuka lazima uwe na operating system ambayo ni genuine ili kiweka kupata updates nyingi na nzuri zaidi .
- Ni vizuri ukawa na password na account zaidi ya mbili katika computer yako moja administrator na ingine , moja ina weza kucorrupt au rafiki yako anaweza kuja kuomba compuer kwani ni lazima atumie account yako ?? unampa hiyo ingine .
- Weka firewall na hakikisha inafanya kazi katika computer yako au mtandao wa kazini kwenu .
 
thanks shy for this useful information,

Mimi ninaswali kuhusu computer yenyewe na si virus.

Mimi ni mpenzi wa kuangalia 'movie''dvd', nilichange setting ya computer kwenda kwenye region 2, ambako kwa muda ndio ninabangaiza,
nikabahatika kwenda kutembelea eneo lingine, na kama ilivyoada nikanunua dvd za eneo hilo ili kujikeep busy, nikaambiwa ili niweze kuangalia nilazima nishift kwenda kwenye region 3, nikabadili.
Sasa nimerudi kwenye region two, na kunarafiki yangu kaniambia mwisho mara tatu kubadilisha, je ni kweli?
na akaniambia ni lazima ni install windows upya
!
kinachonichanganya ni kuwa Hapa nipo region 2 na Tanzania ipo region 5. nifanyaje?

ahsante
 
Back
Top Bottom