Community airlines ni ya nani?

Maseke ya Meme

JF-Expert Member
Jul 11, 2007
1,679
2,975
WanaJF kuna rumours hapa mtaani na vijiweni kwamba kampuni mpya ya ndege ya "COMMUNITY AIRLINES" ni ya Anthony Diallo naomba mwenye kufahamu atumwagie tupate ukweli. Kama ni yake kapata wapi pesa ya kununua Boeing 737-800 ambayo hata serikali haijawahi kumiliki? Kama kiongozi wa serikali kwa muda mfupi aliokuwa madarakani anaweza basi siasa utakuwa ni mradi unaolipa sana!!! Tupeni ukweli wenya data najua JF hamna kinachoshindikana
 
Pia niskia rumours hizo huku na kule,but the little that i know ni kuwa wamiliki wa Community airlines ni pamoja na Mh.Diallo na Matson Chizi(alikuwa M/kiti CCM Dar...kama sijakosea),wenye taarifa za kina watatusaidia
 
WanaJF,

Mimi sijui kama ni ya Dialo- mimi nampongeza kama Mtanzania, ni kitu kizuri kweli sisi tukawa na wazawa na kuweza kuwa na masirika makubwa. Pia Precison Air ni ya Mtanzania.

Je ni bora aje mzungu ndo aonekane mwekezaji mzuri?

Hao wanoiba pesa na kujenga Ulaya ni kipi bora? Community Air pia sii inaajiri Watz na kulipa kodi?

I commend this initiative kuanzisha Community Air- itasaidia kuamsha ATC iliyolala!
 
Ndege sio yao,wamekodi...lakini ni kweli Diallo yumo na jamaa wengine kutoka Mwanza,sina uhakika na huyo Chizi
 
Mmiliki wa Community Airline ni Diallo sasa sijui kama kuna wengine.

Mlio karibu na Mh huyo naomba mmshauri aweke watu wenye proffesion zao ofisini sio kuweka ndugu, branch ya hapa kwetu kajaza ndugu tu wengine hata uwezo wa kazi hawana,kisa mtoto wa dada n.k
 
Nilikuwa Juzi likizo bongoland, nimeitumia hiyo ndege Dar Mwanza, nimeona kuna waturuki wanafanya kazi mle kama wahudumu sasa nashindwa kujua hata kazi za kuhudumia nazo zifanywe na wageni...niliongea na moja wa wafanya kazi alidai ndege ile ni ya Diallo na Karamagi ana hisa kubwa.

Naweza amini hilo maana Radio free Africa na Star TV kila baada ya sekunde chache kuna tangazo la community airlines....Dar-Mwanza 119,000/=!!! too much matangazo hadi inakera
 
WanaJF kuna rumours hapa mtaani na vijiweni kwamba kampuni mpya ya ndege ya "COMMUNITY AIRLINES" ni ya Anthony Diallo

Si tetesi tu. Ni mmojawapo kati ya wadau wakuu wa Community Airlines. Uzuri wa huyu jamaa si kama amepata ngawira toka kwenye siasa. Acha kumpaka matope. The guy seems to be clean. Hana mi-skendo ya kipuuzi.

Pia Star Tv hawaishi kuitangaza kila baada ya sekunde kadhaa huku wakionyesha na viwango vya nauli. Ni sawa na Radio One wanavyokuwa wanalitangaza gazeti lao kila siku 'lenye habari motomoto na zenye utafiti' Alasiri.

Nampongeza Diallo kwa jitihada zake na wazalendo tuko nyuma yake.

mNyOo
 
Actually hatumpaki matope lengo ni kupata ukweli tu!
 
Nauliza,
Hiyo 119,000 Nauli Dar-Mwanza kwenda na kurudi? Au ni one way? Sijasarifia hii route mda mrefu sasa! Je wana ndege ngapi na zinaenda wapi Tz?
 
Nauliza,
Hiyo 119,000 Nauli Dar-Mwanza kwenda na kurudi? Au ni one way? Sijasarifia hii route mda mrefu sasa! Je wana ndege ngapi na zinaenda wapi Tz?

119,000 Tshs ni one way, nafikiri inakwenda na Kilimanjaro nauli yao ni Dar - KJO 99,000/= kwa kweli amejaza ndugu zake wanakera kweli unapokata ticketi, wabeba mizigo guyz are not competent at all watoto wa mjomba...binamu etc...huduma zao ni fake kweli ndani ya ndege..wanagawa maji na juicy tuu no bugger nothing...hwakawii kukwambia soda zimekwisha na hatugawi kakinywaji maana bei zetu ni chini we provide basic services...kwa mtizamo wangu ATC wako juu wakiacha ubabaishaji na ujinga ujinga...nilisha safiri nao some yrs back route hiyo Dar -Mwanza, msosi ulikuwa wa kutosha na kanywaji ka kumwaga...
 
Hiyo 119,000/= ni one way, return ticket ni 238,000/= kama una muda we angalia Star TV au sikiliza Radio Free utajua fare zote.

DAR-MWZ-JRO-DAR
 
119,000 Tshs ni one way, nafikiri inakwenda na Kilimanjaro nauli yao ni Dar - KJO 99,000/= kwa kweli amejaza ndugu zake wanakera kweli unapokata ticketi, wabeba mizigo guyz are not competent at all watoto wa mjomba...binamu etc...huduma zao ni fake kweli ndani ya ndege..wanagawa maji na juicy tuu no bugger nothing...hwakawii kukwambia soda zimekwisha na hatugawi kakinywaji maana bei zetu ni chini we provide basic services...kwa mtizamo wangu ATC wako juu wakiacha ubabaishaji na ujinga ujinga...nilisha safiri nao some yrs back route hiyo Dar -Mwanza, msosi ulikuwa wa kutosha na kanywaji ka kumwaga...

Ushirombo,

Yaani wewe ukisafiri ni hadi upate msosi wa nguvu???? Kwi kwi kwi! Hii si cheap Airlines na ni short distance?

Well kuajiri ndugu ktk kampuni binafsi -inabidi wawe competent- laa sivyo atafukuza wateja! Kusema kweli ni vigumu sana kama mjomba wangu ana kampuni la ndege -mimi nikiomba hata kazi ya ulinzi- aninyime! Kuondoa ajira za ndugu 100% mashirika binafsi ni ngumu!
 
Heheheh....mjomba angekuwa Gavana wa BOT je?
 
Tangia nimerudi hii Nchi nimepanda ndege mno ila zake ni ghali sana . Nashindwa kujua hesbau yake kwa kweli. Sijapanda community wala ATCL ila nimepanda Precision ni ndee ambayo kwa kweli hata chooni kunanuka kama choo cha Public mnazimmoja . Pia they never keep time .Na hasa Route za Musoma , Dar Mwanza na KiA Dar kila siki nachelewa .
 
Nilikuwa Juzi likizo bongoland, ... nimeona kuna waturuki wanafanya kazi mle kama wahudumu sasa nashindwa kujua hata kazi za kuhudumia nazo zifanywe na wageni...

Kama Wahudumu ni Waturuki nahisi ndege hiyo si ya WaTz bali ni shirka la ndege la nchi moja ya nje linalofanya kazi Tz pia. Haiyumkiniki kuwa ni Shirika la Kibongo wakati Wahudumu ni raia wa Kigeni.

Sijawahi kuona hata kusikia Shirika la ndege lililosajiliwa nchini likiwa na Wahudumu wa kigeni. Nadhani hilo linawezekana hapa kwetu Tanzania tu! Yasiyowezekana nchi yoyote yanawezekana Tanzania-kweli hii ni Bongo!
 
119,000 Tshs ni one way, nafikiri inakwenda na Kilimanjaro nauli yao ni Dar - KJO 99,000/= kwa kweli amejaza ndugu zake wanakera kweli unapokata ticketi, wabeba mizigo guyz are not competent at all watoto wa mjomba...binamu etc...huduma zao ni fake kweli ndani ya ndege..wanagawa maji na juicy tuu no bugger nothing...hwakawii kukwambia soda zimekwisha na hatugawi kakinywaji maana bei zetu ni chini we provide basic services...kwa mtizamo wangu ATC wako juu wakiacha ubabaishaji na ujinga ujinga...nilisha safiri nao some yrs back route hiyo Dar -Mwanza, msosi ulikuwa wa kutosha na kanywaji ka kumwaga...

Watanzania mnapenda kulishwa na mnafikiri nauli ndio malipo ya chakula! Ndo maana mkipelekwa kwenye "all you can eat buffet" mnarukwa akili na kusaini mikataba kipumbavu shauri ya tamaa!

Nenda Marekani au ulaya uone, cha bure ni kopo moja la soda, kikombe cha chai au kahawa, Joisi na maji. Ukitaka kifuko cha karanga au biskuti ni $3, kipande cha "baga" $5-10 na hiyo ni safari ya masaa manne!

Otherwise pale jirani na airport si kuna kibanda cha chipsi dume, kwa nini usiende ukashindilia pamoja na mshikaki, ndipo ukakwae pipa?

Get on the plane make you prayers and enjoy the trip.
 
Kama wahudumu ni wageni basi inawezekana ni ndege ya kupangisha. Ni jambo la kawaida kabisa duniani kwamba ukikodisha ndege unaweza kutakiwa iendeshwe na wafanyakazi wa kampuni ulikoikodisha.

Kuhusu kuajiri ndugu, hilo nalo ni la kawaida kwenye kampuni binafsi. Hata Rupert Murdoch amemwajiri mwanae awe mkurugenzi wa Fox News. Mengi akiajiri nduguye IPP mtashangaa?

Hilo la usafi nalo linatokana na hali halisi ya kisomo na maendeleo ya Watanzania. Haiwezekani vyoo vya ndege vikabaki visafi wakati watumiaji si wasafi.

Tuwapongeze Watanzania wanaothubutu kuanzisha biashara zaidi ya ile ya kuwa na baa au daladala.
 
Kwani ndege siku hizi hazitu pale Itigi? kwenye "kuku" wengi kwa msimu wote 24/7/365?

Anyway, mambo mawili ya kuangalia. Umiliki wake na pili huduma zake. Kwenye umiliki sidhani kama kuna mtu atakuwa na tatizo kama Mtanzania kwa kutumia alichonacho kwenda kupata mikopo benki au mashirika ya nje n.k . Tukumbuke kuwa Bw. Diallo alikuwa ni mfanyabiashara maarufu tu pale Mwanza kabla ya kuingia kwenye siasa na anazo mali nyingi ambazo zinaweza kuwa rehani katika kutafuta mikopo.

Unless kuna mtu anaweza kutuonesha kuwa Bw. Diallo ametumia ofisi yake na cheo chake kupata mkopo wa Benki pasipo njia ya haki basi mengine ni wasiwasi usio na msingi. Sidhani kama tunaweza kulinganisha uwekezaji wa Daniel Yona, Ben Mkapa na huu wa Diallo.

La pili ni huduma. Katika ile mada ya "kipi kikureketacho" mojawapo ya mambo mengi yanayowekera watu ni huduma kwa wateja na kama ni kweli yanayosemwa kuhusu Community air sidhani kama ni ya pekee kwenye ndege hiyo (kama suala la mahujaji lilivyotuonesha).

Bado katika Tanzania wazo la huduma bora kwa wateja halizama sana licha ya kuimbwa sana. Huduma kwa mteja siyo kumpatia kile anachostahili tu bali kwenda na kuzidi wito wa kazi! Yaani, ni pamoja na ukarimu, heshima, kujali n.k

Wakati wafanyakazi wengi wanajitahidi kutoa ile huduma au bidhaa, ni vigumu wakati mwingine kumuona mtu anakuwa mkarimu, mwenye kumwaga tabasamu na kuwa mcheshi kwa wateja.

Ndio maana watu kama kina Imani Kajura wamekuwa na mafanikio sana katika masoko kwa sababu wanawakilisha dhana ya "huduma bora inaleta tabasamu!" (M. M. Original)...
 
Hongera diallo, na wengine waige. huduma kwa wateja itaboreka tu pole pole. Rome was not built in a single day.
 
Namfahamu Mhe. Anthony Ng'wandu Diallo toka miaka ya 80,Ni mmoja ya wafanyabiasha walikokuwa na kampuni na viwanda binafsi toka kipindi cha Mwalimu,kuwa na pesa ya kukodi hizo ndege si jambo la kuuliza
1.Kwa asset alizonazo anaweza kukopa Benki ili kuweza kufanya biashara aliyonayo.
2.Sahara Communication kwa mwaka ianlipa kodi zaidi ya sh. Million 150,wanaojua Accounts wanaweza kujua ni faida kiasi gani aningiza kwa Mwaka.
3.toka kipindi cha majiko ya sahara mpaka sasa ,Mhe Diallo hawezi kukosa pesa ya kukodi ndege.
4.Kuhusu suala la kuajiri ndugu zake,Nimekuwa nikifuatilia Biashara za Bwana Diallo,na amekuwa akiweka ndugu zake katika Biashara zake ila zimekuwa na mafaniko makubwa na ndio maana anaendelea na hiyo hulka yake.Mfano Mdogo wake Samwel Nyara ameweza kuiendesha Radio free africa kwa mafanikio mapaka ikazaa Kiss Fm apamoja na Televison ya kwanza kuonesha Live ijadala ya Bunge(Star Tv).

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom