Community Airline: Nini kiliwasibu?

Mshiiri

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
2,012
507
Hii community airline iko wapi? Au ni matunda ya pesa chafu? Ama wamefulia kabla ya kuvaa?
 
Na sikia EL ni mmoja wa wamiliki Community Airline wake kama ni kweli basi ni matunda ya pesa za kifisadi au wameziuza ukilipa madeni si tuliambiwa wapo wengi wamelipa lakini hatujatajiwa...walianza kwa fujo kweli tukajua mkombozi kashuka....
 
Nijuavyo mmiliki alikuwa Diallo wa RFA,akitumia ndege za kukodi toka turkey.Nilipanda ndege hizi dar/mwanza kwenda na kurudi.Pamoja na kuweka nauli ndogo bado ndege ilikuwa inakwenda watu hawafiki hata nusu.Nadhani aliona ni hasara ,gharama kubwa za uendeshaji wakati faida hakuna.
 
Wana jf naomba kujua hivi zilikwenda wapi maana zilipotea ghafla wakati zilionyesha kuwa na soko zuri nchini
 
pesa chafu ya epa ndo ilianzisha hii kampuni, dk.slaa alipolianzisha hili zengwe fyuuuuuuuu wakanywea....thts it.
 
pesa chafu ya epa ndo ilianzisha hii kampuni, dk.slaa alipolianzisha hili zengwe fyuuuuuuuu wakanywea....thts it.


lakini star tv walikuwa wanazitangaza bado ia zinaenda mwanza bukoba kama sikosei..
 
zilikuwa ni ndege za kukodi..Diallo akashindwana na mmiliki wa ndege maana mmiliki alikuwa anataka ndege ziwe na marubani atakaowachagua yeye kutoka huko alipokodisha. matokeo yake wakashindwana kutokana na diallo kushindwa gharama kubwa za kuwalipa marubani kutoka majuu!
 
ilikuja vizuri sana kipindi hicho, ikawasaidia watu wengi ushindani wa makampuni ya ndege yalikuwa mkubwa sana kipindi kile
tatizo sijui ni nini wamewaacha kina
michael ngereku shirima wanafanya wanavyotaka
naikumbuka ndege hii , naililia ndege hii
tatizo lilikuwa ni nini?
Nani alikuwa mbaya?
Inaweza kurudi tena?
Tuombe uzima
 
kamuulize antony dialo ulikuwa mradi wake ni kwa kiasi gani epa ilimyumbisha mpaka kuuza ndege!
 
Biashara za ujanjaujanja unadhani zinadumu basi,siku hizi kila kitu ni ujanja tu. Ilikuja kwa mbwembwe na kishindo sana lakini imekufa kibudu na kwasasa unadhani sababu zitakosekana. Nami nangoja wenye kujua haya mambo kwa undani zaidi waje watujuze wote.
 
Mimi nilisikia kuwa dialo alikuwa na ndege moja ambayo ruti yake ilikuwa mwanza kagera ila baadae watu wengine walikuja kuweka pesa zao....(Wanajulikana)
Na baada ya inshu ya Epa walipoambiwa warudishe pesa serikalini na shirika likajifia zake watu wakatoa pesa zao diallo akabaki na ndege yake ile ile ya mwanza kagera ikawa inafanya shughuli zake

Sijui bado ipo?
 
ilikuja vizuri sana kipindi hicho, ikawasaidia watu wengi ushindani wa makampuni ya ndege yalikuwa mkubwa sana kipindi kile
tatizo sijui ni nini wamewaacha kina
michael ngereku shirima wanafanya wanavyotaka
naikumbuka ndege hii , naililia ndege hii
tatizo lilikuwa ni nini?
Nani alikuwa mbaya?
Inaweza kurudi tena?
Tuombe uzima

ruzuku ya serikali iliposimama ndege nayo ikasimama.dialo ni wa kushtakiwa kwa kutumia pesa ya wa tz kuendeshea miradi yake
 
(Community Airline)Hivi hii kampuni ya ndege ya Usafirishaji iliishia wap? Mwenye taarifa zozote

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom