Comment 1 kwa kina kuhusu Tiba ya Asili ya tatizo lolote, ambayo 100% unahakika nayo kwa shuhuda binafsi

Rango

Member
Feb 14, 2018
81
125
Habari wakuu,

Nimekuja gundua wadau wengi wa JF wanashuhuda za uhakika wa 100% za Tiba fulani za Asili kwa kuwa binafsi au ndugu zao wa karibu walizitumia kutatua Maradhi, Ulemavu au matatizo yaliyowasumbua na wakafanikiwa.

Hivyo nachukua fursa hii kumkaribisha yeyote mwenye kujua Tiba Asili ya jambo lolote na mwenye ushahidi Binafsi, aelezee kwa kina kwa kuandika Comment 1 tu kwa tiba au mkusanyiko wa tiba ili Tuweze kusaidia wadau wengine.

Tiba na suluhu nyingi za asili kuzipata ni mpaka uwadadisi wazee wajuvi ambao siku za hivi karibuni wamepungua na mijini hatujui kabisa wazee hao walipo, Hivyo huu ni wasaa kwa wadau tuibiane Siri za Tiba na Tatuzi hizi.

KUMBUKA: Kuweka herufi kubwa kutaja Kichwa cha Jina la Tiba au Suluhisho kabla ya kuelezea. Na pia ili kutenganisha tiba hizo endapo umeziandika kwa pamoja. Kumbuka pia kuandika maelezo ya muhimu pekee na ushuhuda mfupi kuokoa muda. UONGO, MATANGAZO YA BIASHARA na kuitana PM hakuruhusiwi.

Karibuni Wadau.
 

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,036
2,000
Tiba ya mafua na kikohozi

Kitunguu maji.
Jinsi ya kuandaa, chukua kitunguu kimoja kikubwa kata katikati chemsha kwenye maji ujazo glasi moja inatosha,unaeza kuongeza idadi ya kituu kulingana na ukubwa wa mafua na kikohozi.

Chemsha mpaka litoke povu jeupe na maji yatabadilika rangi kuwa ya zambarau upua yapoze kidogo. Matumizi, kunywa asubuhi na jioni kwa siku 7.

Matokeo,inapoza homa na kichwa, kichwa kinatulia kama sio kupona kabisa, kikohozi kinalanika na mafua yanazibuka kama yameziba.

Maumivu yakizidi muone daktari.
ANGALIZO, hii tiba itakuongezea mihemko(hamu) ya tendo la ndoa sio mzuri kwa asiye na mke au mume.
 

Rango

Member
Feb 14, 2018
81
125
Tiba ya mafua na kikohozi.

Kitunguu maji.
Jinsi ya kuandaa, chukua kitunguu kimoja kikubwa kata katikati chemsha kwenye maji ujazo glasi moja inatosha,unaeza kuongeza idadi ya kituu kulingana na ukubwa wa mafua na kikohozi...
Vizuri mkuu,

Kila unapokunywa Glass moja unarudia kukata kitunguu kingine kila awamu.

KUMBUKIZI KWA WOTE:
Unapotoa maelezo hakikisha yanajitosheleza ili kuepuka comments/maswali mengi kuhusu tiba moja na Pia Ili kutoa nafasi kwa Shuhuda za tiba nyingine ziweze kuonekana.

Unapoandika jichukulie kama ni mgonjwa anayetaka maelezo yote hii itasaidia kujumuisha majibu ya maswali tarajiwa katika maelezo yako.
 

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,036
2,000
Vizuri mkuu,
Kila unapokunywa Glass moja unarudia kukata kitunguu kingine kila awamu.
KUMBUKIZI KWA WOTE: Unapotoa maelezo hakikisha yanajitosheleza ili kuepuka comments/maswali mengi kuhusu tiba moja na Pia Ili kutoa nafasi kwa Shuhuda za tiba nyingine ziweze kuonekana. Unapoandika jichukulie kama ni mgonjwa anayetaka maelezo yote hii itasaidia kujumuisha majibu ya maswali tarajiwa katika maelezo yako.
Yeah, kila unapotakiwa kunywa basi inakulazimu ukate kitunguu kipya
Mf.ukikata kitunguu 1 ukachemsha basi matumizi yake yameisha ni kukitupa mchana au jioni ni hivyo hivyo.
 

Coolant

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
880
1,000
Mizizi ya mnazi kama tiba ya upungufu wa damu.

Chimba mizizi ya mnazi kiasi kidogo tu. Ioshe vizuri kisha ichemshe hadi maji yawe na rangi kama chai ya rangi baada ya hapo yapoze kisha kunywa kikombe kimoja tu kwa siku kwa muda wa siku tatu hadi nne.

Kila siku chemsha dawa mpya usirudie ya jana.

Baada ya hapo unaweza kwenda kuchangia damu.
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
5,905
2,000
Tiba ya mafua na kikohozi.

Kitunguu maji.
Jinsi ya kuandaa, chukua kitunguu kimoja kikubwa kata katikati chemsha kwenye maji ujazo glasi moja inatosha,unaeza kuongeza idadi ya kituu kulingana na ukubwa wa mafua na kikohozi...
Dah sasa mimi nikikaa bila dawa mafua ndani ya siku nne yanaisha.

Alafu dawa inaniambia nitumie siku saba dah.
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
5,905
2,000
Tiba ya mafua na kikohozi.
Kitunguu maji.
Jinsi ya kuandaa, chukua kitunguu kimoja kikubwa kata katikati chemsha kwenye maji ujazo glasi moja inatosha,unaeza kuongeza idadi ya kituu kulingana na ukubwa wa mafua na kikohozi.
Chemsha mpaka litoke povu jeupe na maji yatabadilika rangi kuwa ya zambarau upua yapoze kidogo.
Matumizi, kunywa asubuhi na jioni kwa siku 7.
Matokeo,inapoza homa na kichwa,kichwa kinatulia kama sio kupona kabisa, kikohozi kinalanika na mafua yanazibuka kama yameziba.

Maumivu yakizidi muone daktari.
ANGALIZO, hii tiba itakuongezea mihemko(hamu) ya tendo la ndoa sio mzuri kwa asiye na mke au mume.
Dah sasa mimi nikikaa bila dawa mafua ndani ya siku nne
Yeah, kila unapotakiwa kunywa basi inakulazimu ukate kitunguu kipya
Mf.ukikata kitunguu 1 ukachemsha basi matumizi yake yameisha ni kukitupa mchana au jioni ni hivyo hivyo.
yanaisha.

Alafu dawa inaniambia nitumie siku saba dah.
 

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,036
2,000
Mizizi ya mnazi kama tiba ya upungufu wa damu.

Chimba mizizi ya mnazi kiasi kidogo tu.
Ioshe vizuri kisha ichemshe hadi maji yawe na rangi kama chai ya rangi baada ya hapo yapoze kisha kunywa kikombe kimoja tu kwa siku kwa muda wa siku tatu hadi nne...
TIBA NYINGINE YA KUONGEZA DAMU.
kwa wale ambao wanaishi kwenye miji ambayo haina mnazi.

MAJANI MABICHI YA MPARACHICHI(avocado tree)
Chuma majani ya mparachichi kisha chemsha kwenye maji glasi 1 au 2,yapoze kunywa kutwa mara 2 kwa mda wa siku 7,hakika utaongeza damu maradufu hii inatumika pia kwa wajawazito ni mzuri huna haja kutumia vidonge.
Usirudie kuchemshia majani yaliyotumika.
 

Rango

Member
Feb 14, 2018
81
125
Nb:Ukweli uzingatiwe isije ikawa kama ushuhuda wa kula tunda kimasihara mtu anajitungia kufurahisha genge.
*****Kama Tiba hukuwahi kuitumia Wewe mwenyewe au umesikia tu kwa watu. Basi Ushuhuda wa Tiba hiyo peleka Nyuzi nyingine humu hauhitajiki na kama umeshafanya hivyo njoo Ufute mwenyewe.*****
 

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
3,385
2,000
Tiba ya mafua na kikohozi

Kitunguu maji.
Jinsi ya kuandaa, chukua kitunguu kimoja kikubwa kata katikati chemsha kwenye maji ujazo glasi moja inatosha,unaeza kuongeza idadi ya kituu kulingana na ukubwa wa mafua na kikohozi...
mkuu tunaomba ufafanuzi wa ziada kwenye hilo suala la hamu ya tendo la ndoa
 

Wang Shu

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
2,036
2,000
mkuu tunaomba ufafanuzi wa ziada kwenye hilo suala la hamu ya tendo la ndoa
Mkuu,
Umeoa/umeolewa kama haupo kwenye ndoa hii tiba itakusumbua matokeo yake, lakini kama utaitaji kuitumia kwa ajili hiyo ni sawa.

INAFAYAJE KAZI YAKUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA.
Ukitumia hayo maji ya kitunguu huzalisha NITRIC OXIDE ambayo inafanya kusimamisha UUME kama msumari ndani siku 7,21 au iwe ni desturi yako hakika nakuambia mwili wako utakuwa unasisimka kwa haraka sana yani mke/mume

akikugusa ata unywele utahisi mwili unachemka kana kwamba kuna vitu vinatembea mwilini na kuamsha hisia za kufanya tendo la ndoa kila wakati,inatokea ata ukipita mtaani ukiona mwanamke mzuri tu basi mwili unasisimka na muogo unasimama kila wakati.
Huwa ni kero na inasumbua sana hiyo hali.
 

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
8,125
2,000
Tiba ya asili ambayo binafsi nilikuwa siiamini mwanzoni mpaka nilipofanya na kuona matokeo ni mjomba kula mate ya mpwa wake ili kumsaidia tatizo la kutokwa na udenda.

Chukua udenda wa mtoto anayetoka udenda kisha changanya kwenye chakula ,nyama ,tunda nk kisha mpe mjomba wa huyo mtoto ale , uhakika wa kupona mtoto huyo ni 100% na udenda unakata muda huo huo.


Ushuhuda ni mimi mwenyewe nilitibiwa kwa njia hiyo kipindi bado nipo mdogo na nimeshamsaidia mpwa wangu ambaye alikuwa na tatizo hilo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom