Comedy original (TBC) VS Comedy star search (EA tv)

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,352
3,533
EA tv wameanza kusaka comedian(s) wapya watakao chukua gepu lililoachwa na akina Joti na kundi lake ambao waliwakimbia EA tv na kujiunga na TBC kwa sababu dhahiri kabisa ya mkwanja mnono zaidi hapo TBC.

Kilichonshangaza EA tv walitumia kila hila kuhakikisha jamaa kule TBC hawatumii jina la 'ze comedy' ambalo ndilo walipatia umaarufu kule Ea tv.

Kali zaidi ilo niduwaza jamaa wa EA tv kipindi chao kipya cha comedy star search wamekiweka siku ya alhamis saa 1 usiku, muda sawa na ule wa original comedy ya TBC.
Kama vile hiyo haitoshi wameweka marudio yake ni jumapili saa 12jioni sawa na marudio ya original comedy kule TBC.

Je unafkiri EA tv kugonganisha hivi vipindi ni njama zaidi za kuwauwa comedy original wa TBC au it is just a matter of coincidence?
 
Hapo ni mashindano, sio kuuana , cheki vipindi vya USA na kwingine wanavyo chuana na ukicheza tuu show ina kua canceled. .Ila sijui kwetu rating sys kama ipo!
 
Nafikiri italeta changamoto....unajua tatizo la Tanzania ni kuwa watu wanakosa ushindani na hivyo wanajisahau sana!Nafikiri itasaidia mambo mapya kwenye mambo haya ya uchekeshaji!
 
Mi naona ni bomba tu...Walichoniudhi hawa Orijino Comedi ni kumtukana na kumuigiza mzee Mengi kama mtu wa mambo ya hovyohovyo...too childish!
Kama hakuna sheria inayovunjwa acha vipindi hivi vipandane hivyohivyo, wakorofi wa kuanza matusi wataonekana tu!
 
kwani uongo?
 
EA tv wameanza kusaka comedian(s) wapya watakao chukua gepu lililoachwa na akina Joti na kundi lake ambao waliwakimbia EA tv na kujiunga na TBC kwa sababu dhahiri kabisa ya mkwanja mnono zaidi hapo TBC.

Kilichonshangaza EA tv walitumia kila hila kuhakikisha jamaa kule TBC hawatumii jina la 'ze comedy' ambalo ndilo walipatia umaarufu kule Ea tv.

Kali zaidi ilo niduwaza jamaa wa EA tv kipindi chao kipya cha comedy star search wamekiweka siku ya alhamis saa 1 usiku, muda sawa na ule wa original comedy ya TBC.
Kama vile hiyo haitoshi wameweka marudio yake ni jumapili saa 12jioni sawa na marudio ya original comedy kule TBC.

Je unafkiri EA tv kugonganisha hivi vipindi ni njama zaidi za kuwauwa comedy original wa TBC au it is just a matter of coincidence?
Kama una kumbukumbu nzuri utakumbuka muda wanaorusha kipindi cha ze commedy star search ndio uleule waliokuwa wanarusha kipindi cha ZeCommedy. Kwa hiyo wanarudisha kipindi cha ze commedy katika muda uleule waliokuwa wanaonyesha kabla manji hajafanya ufisadi wa kuwachomoa EATV. TBC ndio waliokopi muda wa kurushwa hewani kipindi hicho mara tu walipowachukua vijana hawa.
Ze Comedy wa EATV inawaandalia kaburi la kudumu orijino komedi wa TBC. Muda si mrefu kina JOTI watafulia. Tusubiri tuone.
 
La hasha, si njama. Ni BIASHARA tu ndugu....
Nimefurahi sana hili kwani TBC wananibore sana na tabia yao ya kutokuwa consistent na vipingi vyao. Hawana ratiba maalumu... ITV wana stick na ratiba za, hili tu litatosha kuiua comedy ya tbc.
 
Nafikiri italeta changamoto....unajua tatizo la Tanzania ni kuwa watu wanakosa ushindani na hivyo wanajisahau sana!Nafikiri itasaidia mambo mapya kwenye mambo haya ya uchekeshaji!

Turuu!
Comedy orijino siku izi kwa kwel hawanichekeshi kama zamani.
Wame-run out of ideas kwa kweli, labda watastuka sasa.
 
Kama una kumbukumbu nzuri utakumbuka muda wanaorusha kipindi cha ze commedy star search ndio uleule waliokuwa wanarusha kipindi cha ZeCommedy. Kwa hiyo wanarudisha kipindi cha ze commedy katika muda uleule waliokuwa wanaonyesha kabla manji hajafanya ufisadi wa kuwachomoa EATV. TBC ndio waliokopi muda wa kurushwa hewani kipindi hicho mara tu walipowachukua vijana hawa.
Ze Comedy wa EATV inawaandalia kaburi la kudumu orijino komedi wa TBC. Muda si mrefu kina JOTI watafulia. Tusubiri tuone.

Ooh kumbe copyin imefanyika otha way round!
Haya ye2 macho na maskio tusubir mpambano.
 
Huwa napenda sana ITV/EATV wanavyokuwa creative na proffesion katika mambo yao. Huwa hawakurupuki na nadhani wanafanya tafiti nzuri kwa customers wao. Nawapa pongezi sana.
 
mbona taarifa za habari za TV zetu zinaingiliana muda? hapo napo unasema wanauana?
ni wewe mteja kuchagua unaangalia ipi, same kwa hawa Ze comedy
 
Kama una kumbukumbu nzuri utakumbuka muda wanaorusha kipindi cha ze commedy star search ndio uleule waliokuwa wanarusha kipindi cha ZeCommedy. Kwa hiyo wanarudisha kipindi cha ze commedy katika muda uleule waliokuwa wanaonyesha kabla manji hajafanya ufisadi wa kuwachomoa EATV. TBC ndio waliokopi muda wa kurushwa hewani kipindi hicho mara tu walipowachukua vijana hawa.
Ze Comedy wa EATV inawaandalia kaburi la kudumu orijino komedi wa TBC. Muda si mrefu kina JOTI watafulia. Tusubiri tuone.

Baba Chrispin BIG THANX.... hakuna maelezo zaidi
 
Je unafkiri EA tv kugonganisha hivi vipindi ni njama zaidi za kuwauwa comedy original wa TBC au it is just a matter of coincidence?
hakuna njama, EATV ndo waliokuwa wakwanza kuwa na kipindi cha Ze Comedy siku ya Alhamis saa Moja kamili, kinarudiwa katikati ya wiki na kinarudiwa tena J2 JIONI,
TBC wakishirikiana na kina Manji Yusuph, kwa kumkomoa Mengi katika shughuli zake wakawashawishi wale vijana , na wale vijana wakakimbilia TBC wakiamini watapewa na kupata pesa nyingi zaidi, ndo mara tukaambiwa wanaenda SA kujifundisha mbinu mpya za uigizaji, mara wakaenda LONDON/UK .
sasa EATV hawakuwa na jinsi ila kusitisha kwa muda kipindi ili waweze kurecruit waigizaji wapya ili kuwezesha kipindi husika kwenda hewani.
hivyo dhana ya kuwauwa commedy original haina mashiko, ila nawaona wakijifia wenyewe kwa kukosa ubunifu yakinifu kuendana na wakati.
wito wangu kwa EATV , warecruit vijana wapya kabisa katika fani, hawa kina Bambo, Mkwere, hawana jipya, watawavuruga tu.
 
mbona taarifa za habari za TV zetu zinaingiliana muda? hapo napo unasema wanauana?
ni wewe mteja kuchagua unaangalia ipi, same kwa hawa Ze comedy

Mmmh! Realy?!

Lkn mkuu zengwe hili la hawa jamaa walipelekana mpaka mahakamani.

Hivo huoni kuna kaushindani flani hapo nje ya mahakamani vilevile? Of course as a viewer i have a choice.... thats 4 sure.
 
ushindani upo .
na sakata lile lilitokana na haki ya EATV kutaka kubakia na kipindi kile hata kama kina Joti wakiondoka, maana msanii ama mtangazaji hana haki ya kipindi unless awe analipwa kwa kukodisha kwa kipindi chake kama walivyo kina Oprah, TYRA BANKS, etc.
 
Mi naona ni bomba tu...Walichoniudhi hawa Orijino Comedi ni kumtukana na kumuigiza mzee Mengi kama mtu wa mambo ya hovyohovyo...too childish!
Kama hakuna sheria inayovunjwa acha vipindi hivi vipandane hivyohivyo, wakorofi wa kuanza matusi wataonekana tu!

PakaJimmy hata mie hapo ndo wameniboa vya kutosha napenda kuwacheki lakini vijana wanaonekana wanapenda ligi..pia muongozaji wa kipindi chao naona kama yupoyupo tu ,,kwa sababu kipindi kabla ya kurushwa inabidi kipitiwe kama hakijakiuka maadili lakini hicho chao sijui kama huwa wanafanya hivyo...
Ila kuna methari moja isemayo mla ndizi husahau lakini mtupiwa maganda ..vijana wajirekebishe wasione kama wamefika wakati bado wanasafari ndefu sana
Pia masanja sasa anaongea sana na utoto umekuwa mwingi !!
 
Tupo kwenye kipindi cha biashara huria ambapo biashara yako itadumu tu kama itahimili ushindani. KUMBUKA KIZURI KINAJIUZA NA KIBAYA KINAJITEMBEZA. watazamaji wataamua wapi ni pazuri kuangalia
 
EATV nao wanahitaji kusonga mbele...mafanikio sio kuwapiku kina Masanja!
 
Back
Top Bottom