Colman Mboya anena: Msizibeze shule za kata. Msimamo wako wewe ukoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Colman Mboya anena: Msizibeze shule za kata. Msimamo wako wewe ukoje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAUMZA, Feb 3, 2011.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Katika taarifa ya habari TBC1 usiku huu, mwanafunzi pekee katika shule ya sekondari ya kata ya Mashujaa wilayani Songea Colman Mboya aliyepata division 1 points 15, pamoja na mama yake mzazi wametoa angalizo kwa watanzania kuwa kamwe wasizibeze shule za kata. Na mimi huo ndo msimamo wangu. Wewe je msimamo wako ni upi???
   
 2. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  He's the poster child of the so called shule za kata:clap2:
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wenzie vipi? mbona hawakushinda kama yeye? (DIV-I = 1 DIV-II = 0 DIV-III = 4 DIV-IV = 34 FLD = 69)kushinda kwake kwa juhudi za mama yake ambaye bila shaka ni mwalimu au alikuwa amemkodishia mwalimu wake special ndizo zinampa jeuri? Haya bwana!
  Nimeona shule moja ya kata huko kanda ya ziwa ina mwanafunzi ambaye baba yake ni mwalimu na sasa mtoto huyo amekuwa akisoma nje ya shule katika shule zingine na special tuition kwa muda mrefu lakini akiwa ameandikishwa katika shule hiyo ya kata. Matokeo yake yakiwa amazing tuambiwe tusidharau shule za kata?!
  Ebu atuambie alikuwa anasoma na mtoto wa mkuu wa wilaya? alikuwa anasoma na mtoto wa mbunge wa Songea? alikuwa anasoma na mtoto wa diwani wao? Alisoma na mwana wa mkuu wa mkoa au RPC wao yule mhaya?
  Hata hivyo kuna wengi tu waliopata ushindi kama wake katika shule hizo hizo za kata ambazo wengine wanaziita Yebo yebo. Sasa nadhani anatumika kupiga kampeni chafu za shule ovyo hizo zisizo na walimu, vitabu wala mahabara.
  Jamani tuache ghiriba kwenye issues za kitaifa!
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unajua hivyo ndio vinaitwa vipaji.... ila kwa wale wenzangu na mimi ambao mpaka mwalimu apige kelele na atumie viboko... shule za kata ni kaburi la elimu!!!
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hivi kweli tunaweza kuwa wajinga kiasi kwamba hatuoni kuwa zaidi ya 90% ya wanafunzi wanaosoma kwenye hizo shule wameondoka patupu? Kwa maana hiyo tushangilie kuwa angalau hao wachache wamefaulu na tusizionee huruma hizo nafsi za vijana walioondoka na mizinga zaidi ya 6 (F katika masomo 6 au zaidi)?

  Shule za kata ni jehanamu na mwanangu hawezi kwenda kusoma huko labda kwanza JK na wateule wake wakubali kupeleka watoto wao pia.

  Kuna vitu vya kutetea lakini siyo suala la shule za kata!
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hayo ndiyo maneno sahihi ya kutumia!
   
 7. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Tatizo CCM kupitia TBC1 wanataka kumtumia Colman kama mtaji wa ki Siasa na Kun justify Failure ya CCM kwenye Suala la Elimu na shule za kata ki ujumla.
  Point ya Msingi ni kwamba kama kweli amefaulu pasipo extra effort and support, Na lazimika kusema kusema kuwa Colman is Gifted,talented, smart and inteligent Boy, on the other side of the same coin,kuna Vipaji vingi sana kama Colman ambavyo vimeuliwa na shule kata,nashawishika kusema kuwa kama Colman angesemea shule zenye unafuu angeweza kupata A zoote kabisa,hajui maskinkama alitakiwa kufanya vizuri zaid ya pale ila mazingira ya shule za kata aliyosomea ndo yame mlostisha
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  inaonekana hajui asemalo! Tumsamehe!
   
 9. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #9
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hajui asemalo kwa kweli, matokeo ya shule huangaliwa kwa wastani wa shule nzima na siyo kamwanafunzi kamoja au wawili, yeye kapata point 15 wenzake wamepata nini, hata uchumi wa Taifa huangaliwa kwa kipato cha wastani kwa wananchi walio wengi na siyo kipato cha mwananchi mmoja, shule za Kata is the biggest Joke in Education System ever.
   
 10. B

  Baba Tina Senior Member

  #10
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TBC nao wakati mwingine wanakosa habari za kutuonesha. Mtu 1 anapopata div 1 halafu hakuna div 2 unategemea nini? Tbc wanajaribu kutuonesha kwamba serikali ya ccm haikukose ilipoamua kuanzisha shule za kata bila kufanya maandalizi. Shule za kata bado ni tatizo ndio maana hata wazito hawapeleki watoto wao huko. Inawezekana colman kafaulu kutokana na uwezo wake binafsi na kipaji alichonacho. Tunafahamu kwamba shule za kata zinachukua hata wanafunzi wenye uwezo na vipaji ambao hawategemei sana walimu. Ndio maana hata kwenye timu za mpira kuna wachezaji wenye uwezo binafsi na vipaji vya kuzaliwa ambavyo hawavipati kutoka kwd makocha wao, mfano ni watu kama gaucho na messi. Inawezekana hata colman yuko kwenye kundi la akina mess na gaucho ndio maana kawaacha wenzake kwa mbali.
   
 11. t

  tweve JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 696
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa mkuu,kwanza huyu dogo yawezekana alichakachua mitihani ,
   
 12. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnamaanisha nini ?kama mtu kafeli kafeli mambo ya kuzibana na kuziachia hayana msingi.ukweli ni kwamba siasa haileti tija kama haitekelezwi ipasavyo. MWAKA UJAO WANAFUNZI WA KATA WAPEWE DIV. 1 AND 2 ili iwaje?
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  all of this is bz of mixing politics and education, hawa TBC wanatumiwa kwa kila kitu hata cha kijinga, kwani wao hawajui kuwa huwezi kufanya evaluation assessment ya mtu mmoja bila ku-compare na wengine? wanafanya kazi gani hiyo?
   
 14. P

  Pokola JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wa kulaumiwa hapa ni TBC1. Kwanza tusiwajadili.
   
 15. T

  Tata JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Hakuna anayezibeza shule za kata. Kinachofanyika kwa sasa ni watu mbali mbali kuchambua upungufu mkubwa wa kitaaluma katika shule hizi ambao ndio chanzo cha matokeo mabaya ya shule za kata. Unataka watu waishangilie shule ya Colmani Mboya ya Mashujaa wakati ambapo asilimia 64% ya wanafunzi wamepata daraja la 0, asilimia 31% daraja la 4, asilimia 0.037% daraja la 3, na asilimia 0.009% daraja la 1. Kwa maana nyingine asilimia asilimia 95% ya wanafunzi wa shule hii wamepata ama daraja la nne au sifuri. Kwenye takwimu matokeo ya Colman huwa hayazingatiwi kwani hayawakilishi hali halisi ya kinachoendelea shuleni kwao.
   
 16. T

  Tata JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Duuh ndugu yangu wewe una moyo. Kwa hiyo JK na wateule wake wakipeleka tu watoto wao huko na wewe unapeleka bila kujali kama kuna mabadiliko ya msingi ya kitaaluma kwenye hizo shule. Lakini nimekuelewa kwani ni ndoto za mchana kudhani kuwa JK na wateule wake watapeleka watoto wake kwenye shule hizo. Aliyeweza kufanya hivyo ni JKN na wateule wake tu..
   
 17. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Wazo la shule za kata ni zuri - kibaya ni kushindwa kwa serikali kupeleka huduma huko.

  Kiukweli watu wanawapeleka watoto huko kutokana na kukosa uwezo wa kuwapeleka kwenye shule nyingine zenye huduma za walimu, vifaa, nk.
   
Loading...