Cocoriko Mpya Arusha usipime.."DC itakuza sekta ya Utalii"

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fabian Daqaro amewakaribisha wawekezaji katika sekta ya burudani ili kukuza sekta ya Utalii na kusaidia viwanda vya ndani vinavyozalisha vinywaji vikali na vilaini kuweza kuimarisha masoko yao ya ndani.

Rai hiyo ameitoa jijini Arusha wakati alipokuwa akizindua Klabu Mpya yenye hadhi ya kimataifa ya Cocoriko Anex iliyopo katika ukumbi wa Papa King zamani ikijulikana kwa jina la Triple A Klabu na kueleza kuwa ukumbi huo uwe kichocheo cha utalii katika Jiji la Arusha.

Amesema kuwa Jiji la Arusha linahitaji kumbi za starehe za kisasa ili kukidhi matakwa ya wageni mbalimbali wanaoingia katika mkoani hapa kwa ajili ya utalii ,hivyo aliwaalika wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta hiyo ili kusaidia viwanda vya ndani vinavyozalisha vinywaji vikali na vilaini kupata masoko ya uhakika .

"Kufunguliwa kwa Klabu hii ya Cocoriko kuwe kichocheo cha viwanda vyetu vinavyosalisha vinywaji vikali na vilaini kuimarisha masoko ya ndani na hivyo kwendana na Sera ya rais John Magufuli ya ujenzi wa viwanda" Amesema Daqaro

Awali Mwekezaji wa Klabu hiyo ,John Mdenye,ambaye pia ni Mmiliki wa Klabu ya Cocoriko Klabu iliyopo kijenge na Mjengoni classic Klabu Amesema kuwa uwekezaji wa Klabu hizo ameweza kutoa ajira kwa wafanyakazi wapatao 200 .

"Tumetengeneza Klabu yenye hadhi ya kimataifa na itakayosaidia kuongeza idadi za kumbi za starehe katika jiji la Arusha na hivyo kuwa kichocheo kipya cha burudani kwa wageni mbalimbali watakaofika katika Jiji la Arusha" Alisema Mdenye.

Ameongeza kuwa pamoja na ajira alizotoa kwa wazawa katika Klabu zake ,pia Klabu hizo ni chanzo cha mapato ya serikali na itachangia kwa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za nchi.

"Katika Klabu ya Cocoriko Anex usalama wa mteja na Mali yake ni wa kiwango cha juu,kwani Klabu imefungwa CCTV kamera,pia kutapatikana bendi itakayokuwa ikipiga mziki Mubashara,Mashindano kwa ajili ya kutangaza utalii,Michezo mbalimbali itakuwepo" Alisema Mdenye

Awali Meya wa Jiji la Arusha,Kalisti Lazaro alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni mbalimbali katika ukumbi huo wa Cocoriko Anex kwa kuwa umelenga kuongeza hadhi ya jiji la Arusha kimataifa katika kutoa Huduma mbalimbali za starehe.

Naye kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shanna aliwahakikishia ulinzi wa kutosha wageni wote wanaoingia katika mkoa wa Arusha na wanapokuwa katika kumbi mbalimbali za starehe kuwa ulinzi utakuwepo wa kutosha .

IMG-20190521-WA0061.jpeg
IMG-20190525-WA0086.jpeg
IMG-20190525-WA0074.jpeg
IMG-20190525-WA0003.jpeg
IMG-20190525-WA0097.jpeg
IMG-20190525-WA0077.jpeg
 
Mdenye anajitahidi sana maana hapo Cokoriko ya kijenge yenyew tu ni shida kiujumla kwa upande wa kumbi za stareh saivi hana mpinzani arusha.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom