Coco Beach inapojengwa wasisahau kuweka sehemu za michezo ya maji (Water Sport).

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,944
12,506
Huu ujenzi wa ufukwe wa Coco inabidi waweke sehemu za michezo ya maji kama sehemu yenye daraja la diving.

Eneo la maegesho ya boti ndogo za michezo pamoja na njia ya gari za kuvuta tela za boti ndogo wakati wa kuingia majini.

Pia wasisahau baada ya mradi kuisha kama watu wengi itakuwa ni sehemu ya kwenda kuogelea na kufanya michezo kwenye maji basi inabidi waweke walinzi wa pwani au beach ( Coast Guard Watches).

Coast Guard Watches hawa husaidia pale mtu anapozama au kupata tatizo la ghafla kwenye maji.Tumeshuhudia vifo vingi vinavyotokea beach mbalimbali na uokoaji unakuwa mdogo.
HTB1yfmKbFkoBKNjSZFEq6zrEVXaJ.jpg_300x300xz.jpg
depositphotos_21025191-stock-photo-tremezzo-town-at-the-famous.jpg


Hizo parking za boat tunaweza tumia za mbao au za kuelea ambazo ni za plastic.
 
Kwa wale wanaogelea inabidi wawekewe jukwaa( Stage) kwa ajili ya kujirusha(Diving) kwenye maji.
 
Kweli kabisa mkuu ila pia wangeweka hotel za uhakika na njia za cycling
Wakiweka jet ski itakuwa safi sana kwani sio ghali kihivyo hata vijana wanaweza kuwekeza
Kuwekeza jet ski haitaji mtaji mkubwa na hapa Tanzania uwekezaji huu bado sana.
Isingekuwa mambo ya mtaji ilitakiwa saizi niwe nimewekeza.
 
Kwakuwa nchi yetu tupo nyuma masuala ya utunzaji wa miradi ingependeza wakapeleka watu kwenye mafunzo maalumu kwaajili ya usimamizi na matunzo ya hilo eneo ili liwe sustaibable, ipo hatari baada ya awamu anzilishi kuondoka na beach nayo ikaanza kusagika taratibu
 
Back
Top Bottom