COCO BEACH: From City Dump to Paradise. A design proposal for a public Beach in Dar, Tanzania

untitled-jpg.313313
 
Imetoka hiyooooooooo, kuna maeneo mengi nchini wakafanye hayo

Awamu ya tano oyeeeeeeeeeeeee
 
Nadhani hawa mabinti wamedevelop hoja nzuri ila haitekelezeki kwa kirahisi hasa Tanzania. Mimi najiuliza yafuatayo:

1. Kama entry ni free kwa maana ya kupunga hewa na kuoga baharini kuna wasiwasi gani kuzuia uwepo wa facilities nyingine wakati hata sasa kuna Bar moja pale Coco ambayo sio bure.

2. Pili watu wanapinga uwekezaji wa facilities na TIB ila wanapendekeze beach ifanyiwe maboresho kwa Pesa ya walipa kodi wa Tanzania yote. Huu kwangu ni wehu, haiwezekani mamilioni ya watu wawachangie vijana wachache na wavuta unga pale Coco kusherekea raha yao wenyewe.

3. Kuna watu wanapinga uwekezaji wa beach bila kufanya utafiti. Mfano Kigamboni kuna beach ya Mikadi inajaza waswahili kibao kila weekend almost sawa na Coco na bado hawa waswahili hulipia hawaingii bure, mimi najiuliza kweli cost ikiwekwa kidogo kwa ajili ya usafi na mazingira watu watashindwa kwenda? Mbona Mikadi kuna waswahili wengi tu.

4. Huu utaratibu wa kuwabebesha watu wote mzigo wa watu wachache nadhani tuubadirishe sasa, hali ya usalama Coco na usafi vinatisha kurekebisha haya yanahitaji pesa, na si busara ikawa pesa ya watanzania wote kwani kama nchi tunakabiliwa na matatizo mengi kuliko starehe ya watu wachache.

Mwisho napendekeza hizo proposals za TIB na KMC zingewekwa wazi zijadiliwe kwa urefu na wadau na sio kuzidismiss kuwa hazifai. Naamini dawa sio kuzifutilia mbali bali kuzifanyia maboresho.
hivi land policy ya mwaka 1997 ilishabadilshwa? nakumbuka kuna sehemu inayohusu sensitive areas should not be allocated to individuals.
 
wewe unatumwa na manji nini?
arudishiwe uwekezaji wake /
mamlaka kuu za jiji ziendeshe!
Chini ya uongozi uliopo,umaridadi wake utaongezeka, na sheria Kali zikiwekwa!
Mmmh!!! Ndugu, umeelewa hoja ya hawa waandishi? Mie mbona naona hoja yao inahalalisha Manji kupokonywa hiyo project!
 
Back
Top Bottom