N'jomba-N'tu
Member
- Aug 17, 2015
- 55
- 20
Ndugu wabunge
Nimeamua kuyaandika haya ili muone kwamba hapa pia kuna JIPU. Mimi ni mwajiliwa kwenye kampuni ya Coca-cola kwanza ltd iliyopo mikocheni jijini Dar es salaam. Ndugu wabunge, sisi cocacola mpinzani wetu mkubwa kibiashara ni Pepsi. Sasa mwezi uliopita muheshimiwa waziri wa kazi na ajira ( Jenister Muhagama ) alifanya safari ya kushtukiza Pepsi na kukutana madudu kibao hivyo ikapelekea pepsi kupigwa faini. lakini pia waziri huyu akaifutia leseni ile kampuni ya UWAKALA WA AJIRA ambayo yenyewe ndiyo inayowasimamia vibarua pale Pepsi jijini Mwanza ( Salama Investment )
Jambo hili limeonyesha kumfurahisha mno mkurugenzi wangu hapa Cocacola kwanza bwana Basil Gadzious ambaye ndiye Country Managing Director wa kampuni ya cocacola hapa Tanzania. Juzi kwenye uzinduzi wa bidhaa yetu fulani mkurugenzi wangu alisema kwamba Pepsi wamekutwa na makosa kibao hivyo wamechukuliwa hatua. Akaja kusema kwamba kwa hapa Cocacola yeye hana presha kabisa maana kampuni iko vizuri na kumalizia kwamba yeyote anayetaka kuja aje tu yeye hana presha.
Baadhi yetu tumejiuluza mengi sana. Hivi Mkurugenzi inamaana hajui kwamba hapa Cocacola ndo kuna madudu mengi kuliko hata Pepsi.
Mimi ni mwajiliwa lakini nikiwaangalia vibarua hapa kwakweli inasikitisha sana. Ndugu wabunge, vibarua hapa wanajituma mno ila hakuna anayewajari. Hapa kwetu kibarua akipata ajali hata akatike mguu ataambiwa tu arudi nyumbani akajitibie mwenyewe akipona ndo arudi kazini. Pepsi mtu anaosha kreti lenye chupa 24 kwa shilingi 100 lakini hapa Cocacola utakuta kreti imechanganyika chupa. Yani kreti moja ina chupa za fanta, sprite, tangawizi, tonic, soda water, Coca light n.k sasa unatakiwa uzichambue kila chupa zikae kwenye kreti lake. Hapa hawakulipi kwa kreti bali kwa parent. Pareti moja ni shilingi 400 Na pareti moja inabeba kreti 65. Hivyo kwa siku hadi upate shilingi 4000 yakupasa uchambue kreti zipatazo 650. ( tena wanaochambua ni wanawake. Hawana jinsi wanafanya tu kazi ili siku ziende tena hupewi hata chakula. )
Vifaa vya kufanyia kazi wakipewa Leo ndo hadi wanasahau kupewa tena na wengine hawana vifaa.
Kuna vibarua tunawaona humu kiwandani miaka nenda rudi lakini hawajapewa hata mkataba wa kazi.
Hata wale vibarua wenye mkataba nao hali mbaya tu. Hawana bima ya afya wala hakuna pesa ya likizo. Nenda likizo lakini utajijua mwenyewe hupewi hata senti ( kwa wale vibarua wenye mkataba.
Kuna viabarua hawapewi Overtime lakini kazi ni SAA moja asubuhi mpaka SAA moja usiku.
Vibarua wanaopewa overtime nao huwa wanakadiliwa Masaa. Ukipunjwa Masaa hakuna wa kumraumu utaambiwa wewe ni kibarua tu.
Kwa siku kibarua anayelipwa kwa kutwa hupewa 5000. Inasemekana Kampuni ya Cocacola inampa WAKALA WA AJIRA 10000 lakini yeye wakala anayokuja kumpa kibarua ni hiyo 5000.
Wale wenye mikataba wanapewa 150,000 badala ya 300,000 kwa mwezi ambayo Cocacola inatoa.
Kuna manyanyaso mengi sana kwa vibarua. Hata sisi waajiliwa tuna malalamiko lakini vibarua kwakweli wamezidi.
Vibarua wakienda HR yetu ya Cocacola kulalamika wanaambiwa nendeni mkamlalamikie CHAGUO ambaye ndiye wakala wenu wa ajira wa hapa. Wakienda kwa Chaguo wanaambiwa nendeni HR ya Coca cola mkalalamike. Kwa hiyo Chaguo na Cocacola kila mmoja anamtupia mpira mwenzake. ( Je vibarua hawa waende kulalamika kwa nani? )
Wabunge pelekeni hili swala bungeni. Serikali izimulikeni hizi kampuni za Uwakala wa ajira. Zinawanyonya sana vijana wetu. Hizi kampuni ni MAJIPU.