MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Dar es Salaam na mikoa mingi sasa hivi ni kipindi cha joto kali sana. Kama wewe ni mpenzi wa kinywaji baridi aina ya Pepsi na kwenye mizunguko yako ukaona sehemu wamepanga viti vya rangi nyekundu vya coca-cola, eneo hilo si salama hata kidogo kwa kinywaji cha Pepsi, kwa maana nyingine eneo hilo vinywaji hivyo ni marufuku kabisa kuuzwa.
Yapo maelezo kuwa baada ya kinywaji cha jamii ya coca-cola kukosa soko baada ya kuchakachua vinywaji vyao na vinywaji vya jamii ya pepsi kupendeka zaidi, kampuni ya coca-cola imeingia mkataba na wauzaji wengi wa rejareja kutokuuza vinywaji vya pepsi, na kila mwisho wa mwezi coca-cola wanakulipa fedha taslimu kama faida yako uliyokuwa ukiipata ulipokuwa unauza vinywaji vya pepsi, pamoja na kupewa viti, meza na firiji.
Sina hakika kama tume ya biashara huru wanayo taarifa kuhusu huu uhuni unaofanywa na kiwanda cha vinywaji baridi cha coca-cola,au pengine tume nayo imechakachuliwa na makaburu.