Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,234
Hivi kuna watu wanaochapa kazi kama masikini? Ndugu yangu haujatembea ukajionea hapa unataka kusema masikini hawafanyi kazi ndiyo maana ni masikini?Upuuzi gani kama mtu anakuambia chapa kazi na endelea kufyatua?Au humo kichwani mwako ni sifuri?Kama unapiga kazi it means utapata kipato kitakachoweza kuendesha maisha yako vizur,sasa kwanini usizae?Au unamattz ya uzaz hii kauli ya kuzaa imekukera?
Ndugu lazima tukubali amepotoka kigezo cha kuzaa sana kisiwe kuchapa kazi bali kiwe mafanikio kama umechapa kazi haujafanikiwa huna haja ya kuzaa halafu usiangalie leo tu angalia na kesho. Kuwa na uwezo wa kulisha watoto nane leo isikupe kiburi. Angalia kama umejiwekeza vizuri kiasi kwamba hata kesho ukipata ajali ya mguu ukashindwa kufanya kazi una miradi ya kulisha hao watoto nane au ndiyo utaingia nao barabarani kuomba kwa kisingizio cha ulemavu?
Jifikirie je ukifariki leo mke wako ana uwezo wa kulea na kusomesha ao watoto nane je unaacha mali gani za kumuwezesha mkeo kuhudumia watoto nane kama ukifariki au ndiyo mkeo aanze kulaumu mashemeji na mawifi zake kuwa hawamsaidii. Unajua vile ndugu wanalia kwa uchungu mtu mwenye familia kubwa akifariki wanajifikiria mzigo walioachiwa marehemu alikuwa anawatoto 11 wote wapo shule mabamdogo na maanti wapo watatu wanalia jinsi watavyogawana mzigo.