CMG tupeni mrejesho wa kilichopatikana Na matumizi ya michango tuliyotoa Kwa ajili ya matibabu ya ndg yetu Ruge

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,041
2,000
Naweza kuonekana mbaya Kwa kuhoji ila tutambue uungwana ni vitendo .


Wengi tulijitoa sana Kwa ajili ya kuchangia gharama za matibabu ya ndugu yetu aliyetutoka baada ya kuugua Na kutibiwa huko South Africa.

Kwa namna moja ama nyingine aligusa wengi Na ndio maana wakajitoa Na kuchukulia Kwa uzito kuchangia huku tukiongozwa Na Mh Rais Magufuli.


Tunafahamu michango ilipokelewa Kwa kupitia mitandao ya simu Na bank , tunafahamu suala la kupata records sahihi Kwa kilichokusanywa nalo siyo Jambo zito.


Tunaomba Na tunajua ni wajibu wetu kupata Statement nzima pamoja na mchanganuo mzima wa mapato Na matumizi Na kama kuna kilichobaki basi Watanzania tufahamishwe.

Huenda mmepanga kutupa mrejesho baada ya mazishi napo siyo mbaya kama mna Lengo hilo.

Hii itajenga IMANI pia kuwasaida Na wengine watakaokuja , Ruge siyo mtu wa kwanza wala wa mwisho kuchangiwa , Kwa hiyo tunaomba tuwekwe wazi katika hili Tafadhali.


Mwisho niendelee kuwapa pole wafiwa , tupo pamoja katika shughuli hii ya kumpumzisha ndugu Yetu .


R.I.P Ruge

Sent from my Iphone using Tapatalk
 

TANZANIA NCHIYANGU

JF-Expert Member
May 13, 2017
636
1,000
Michango ilikuwa inatumwa kwa mdogo wake ruge na number yake ilitolewa kwa ajili ya kumchangia...kama unataka kujua kilichopatikana wapigie familia watakwambia maana ndo waliokuwa wanakusanya michango...hii nchi bana kuna watu mmekalia roho mbaya na majungu...CMG inahusika vipi na michango ya ruge...kwanza mtu kama wewe na uhakika kabisa hukuchangia hata buku
 

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,041
2,000
Michango ilikuwa inatumwa kwa mdogo wake ruge na number yake ilitolewa kwa ajili ya kumchangia...kama unataka kujua kilichopatikana wapigie familia watakwambia maana ndo waliokuwa wanakusanya michango...hii nchi bana kuna watu mmekalia roho mbaya na majungu...
Roho mbaya ningekuwa nayo nisingemchangia mkuu

Sent from my Iphone using Tapatalk
 

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,041
2,000
Wapi nimesema SMG ,hebu soma tena

Sent from my Iphone using Tapatalk
 

mama hepache

Senior Member
Dec 22, 2018
132
250
Michango ilikuwa inatumwa kwa mdogo wake ruge na number yake ilitolewa kwa ajili ya kumchangia...kama unataka kujua kilichopatikana wapigie familia watakwambia maana ndo waliokuwa wanakusanya michango...hii nchi bana kuna watu mmekalia roho mbaya na majungu...CMG inahusika vipi na michango ya ruge...kwanza mtu kama wewe na uhakika kabisa hukuchangia hata buku
Kweli Kbs, maana watu hawana dogo hasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,507
2,000
Sio vibaya kujua ila ameuliza wakati usio sahihi,angetakiwa kusubiri kwanza mpaka baada ya mazishi...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom