CMA wametupilia mbali malalamiko yangu kisa sijafaili termination letter nifanyaje nikate rufaa?

daniel enocy

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
380
413
CMA wametupilia mbali malalamiko yangu kisa sijafaili termination letter nifanyaje nikate rufaa wapi,coz mshitakiwa aliweka pingamizi but alichelewa kuwasilisha ,wamefanya mamuzi mawili kukata pingamizi la mlalamikiwa na pamoja namaombi yangu
 
Pole ndugu, pili usihofu swala lako ilo ni dogo tu.

Unatakiwa ujue kwamba CMA ni chombo cha usuluhishi na rafiki, ni hatua ya kwanza ya kimahakama, kwaio usiogope ukachanganyikiwa ukajua ndio basi haki yako imepotea.

Kisheria swala lako liko hivi, ili mtu u appeal kwenda ngazi inayofuata baada ya hapo CMA kwanza ni lazima uwe haujaridhishwa na maamuzi yenyewe either yamekukandamiza na kuegemea upande mmoja au haukutendewa haki, endapo utakua haujaridhishwa na maamuzi yenyewe na ukihisi kulikua na hila au mbinu chafu kati ya upande unaoudai na ule wa Tume... Sasa unapaswa kukata rufaa kwenye mahakama kuu kitengo cha kazi,,, na nimeona hapo umeandika kua mdai alichelewa kuweka pingamizi, lakini tume nayo imekataa pingamizi la mdaiwa na madai yako wewe pia labda kwa kile ilichoona hakipo kisheria, but je nyie sasa mlienda pale kufanyaje? Kama CMA ilishindwa kuwapeni utaratibu tangu awali ilikua na nia gani mkizingatiwa nyie ni watu msioelewa sheria? Kuna haja gani ya tume kuziondoa kesi kitechnicalities while iko pale kusuruhisha kirafiki tu na ndo maana hata maamuzi yake hayapaswi kuzidi siku 30... Kwaio wewe nenda mahakama kuu kitengo cha biashara uka ombe revision ya maamuzi ya CMA kua hayakua ya haki na hayakufuata misingi ya tume yenyewe.
 
Ahsante kk nmekuelewa,Jana nilitakiwa niende high court ya mbeya but kutokana na hali ya Jana kuwa hofu police kupiga mabomu nikaamua kwenda leo
 
Pole ndugu, pili usihofu swala lako ilo ni dogo tu.

Unatakiwa ujue kwamba CMA ni chombo cha usuluhishi na rafiki, ni hatua ya kwanza ya kimahakama, kwaio usiogope ukachanganyikiwa ukajua ndio basi haki yako imepotea.

Kisheria swala lako liko hivi, ili mtu u appeal kwenda ngazi inayofuata baada ya hapo CMA kwanza ni lazima uwe haujaridhishwa na maamuzi yenyewe either yamekukandamiza na kuegemea upande mmoja au haukutendewa haki, endapo utakua haujaridhishwa na maamuzi yenyewe na ukihisi kulikua na hila au mbinu chafu kati ya upande unaoudai na ule wa Tume... Sasa unapaswa kukata rufaa kwenye mahakama kuu kitengo cha kazi,,, na nimeona hapo umeandika kua mdai alichelewa kuweka pingamizi, lakini tume nayo imekataa pingamizi la mdaiwa na madai yako wewe pia labda kwa kile ilichoona hakipo kisheria, but je nyie sasa mlienda pale kufanyaje? Kama CMA ilishindwa kuwapeni utaratibu tangu awali ilikua na nia gani mkizingatiwa nyie ni watu msioelewa sheria? Kuna haja gani ya tume kuziondoa kesi kitechnicalities while iko pale kusuruhisha kirafiki tu na ndo maana hata maamuzi yake hayapaswi kuzidi siku 30... Kwaio wewe nenda mahakama kuu kitengo cha biashara uka ombe revision ya maamuzi ya CMA kua hayakua ya haki na hayakufuata misingi ya tume yenyewe.
Mkuu, ni Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi na si Biashara. Ipo Kinondoni pale karibu na ilipokuwa Mango Garden
 
Back
Top Bottom