CMA, P Funk kukusanya data za nyimbo zote zinazopigwa

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) imekabidhiwa kazi ya kukusanya data za nyimbo zimepigwa mara ngapi kwenye redio na TVs ili muhusika aweze kulipwa.

Je unafikiri CMA itafaulu kuhakikisha wanamuziki wanafaidika na hili jambo? Je unafikiri kutakuwa na upendeleo kwa baadhi ya wanamuziki?
 
Kuhesabu nyimbo zimepigwa mara ngapi kwenye radio na TVs!! Utaratibu gani utatumika katika kuhesabu huko? Au muhusika anatega Sikion Radioni na Jicho kwenye tvs Toka Majogoo mpaka night?
 
Wasanii washaukataa CMA mpaka watakapokaa pamoja kujua CMA watawalipa vipi Wasanii maana wanaona Hiyo CMA Haina tofauti na kampuni za miito yaani mteja anakatwa 150 msanii analamba 30.
 
Hiyo ni ya NAPE. Sasa media hazipigi nyimbo zao.
... sheria hii imepitishwa lini na bunge? muziki wa kigeni utahusika pia ? muziki ulio kwenye mtandao je?...... naona dalili vituo vya redio na TV kutocheza muziki wa kibongo iwapo muziki wa kigeni hautalipiwa
 
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi na mambo ya nyimbo wapi na wapi? Tume hiyo imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Kazi na Ajira ya mwaka 2004. Haina mamlaka hiyo. Labda kama Kuna chombo kingine chenye mfanano wa jina.
 
Back
Top Bottom