CMA(Commission for Mediation and Arbitration) wanasema ni sharti niwe na mwanasheria ndipo wanisikilize

Mgimilamaganga

JF-Expert Member
Mar 31, 2019
266
257
Habari za muda huu wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada.Juzi hapa niliweka uzi unaohusu kumaliza mkataba wa kazi na niliomba kujua haki zangu.

Kuna mdau alinishauri niende CMA,Leo hii nikaamua kwenda lakini majibu niliyopata ni kwamba lazima niwe na Mwanasheria ndipo watalishughulikia hilo jambo.

Sasa naomba ushauri juu ya hilo,kwani binafsi sina uwezo wa kumlipa Mwanasheria.
 
Sio lazima ila kuna time ikifika lazima uwe naye kwa sababu ya kutafsiri sheria ila ukifika pale CMA chini utakutana na wanasheria kibao wa bei chee tu unamlipa kidogo then nyingine mkishashinda kesi 10% yake ya malipo
 
Habari za muda huu wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada.Juzi hapa niliweka uzi unaohusu kumaliza mkataba wa kazi na niliomba kujua haki zangu.

Kuna mdau alinishauri niende CMA,Leo hii nikaamua kwenda lakini majibu niliyopata ni kwamba lazima niwe na Mwanasheria ndipo watalishughulikia hilo jambo.

Sasa naomba ushauri juu ya hilo,kwani binafsi sina uwezo wa kumlipa Mwanasheria.
If you refer to the Employment and labour relation act section 86 (6) states
"In any mediation, a party to dispute MAY be represented by-
a) a member or an official of that party's trade union or employer's association; or
b) an advocate
Sio lazima kuwa represented, ndo maana wakatumia neno "MAY"
 
Sasa hawa CMA ndo wamekataa hata kunisikiliza,dah.
 
kwani kampuni husika imekataa kukulipa?
Maana kama ni kampuni loyal lazima iwe inajua huu utaratibu wa kufanya payments mbalimbali ambazo ni stahiki yako, ikiwemo leave pay, notice pay kama hawakukupa notice, transport allowances na any severance pay due. Hatua ya CMA itakuja baada ya wao kudeclare kuwa hawatohusika na malipo hayo mi nafikiri jarbu kubargain nao kwanza kuliko kuextend mchakato that far.
 
Habari za muda huu wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada.Juzi hapa niliweka uzi unaohusu kumaliza mkataba wa kazi na niliomba kujua haki zangu.

Kuna mdau alinishauri niende CMA,Leo hii nikaamua kwenda lakini majibu niliyopata ni kwamba lazima niwe na Mwanasheria ndipo watalishughulikia hilo jambo.

Sasa naomba ushauri juu ya hilo,kwani binafsi sina uwezo wa kumlipa Mwanasheria.
kakope vikoba ulipe mwanasheria
 
Mkuu ngoja nikuambie,Mimi nilikuwa nafanya kazi pale bila kuwa na kitambulisho chochote zaidi ya sare tu,Sasa jana nimeenda wakaniambia niwakabidhi nguo zao halafu wao wataamua siku na tarehe ya kunipa stahiki zangu.

Na hii imewatokea watu wengi pale na mwisho wa siku hawakupata chochote,kampuni ilikana kuwatambua baada ya kukabidhi Uniform.Hata Pay In slips,huwa wanazuia kuzipiga picha,ukipewa hela yako,Pay in slip wanaondoka nayo(Binafsi nilibahatika kuipiga Pay In slip moja kwa siri sana).

Baada ya mkataba kwisha niliwauliza juu ya malipo ya likizo,notice,mshahara wangu,pesa za sare walizokuwa wakinikata,wakaishia kucheka sana kwa dharau.

Sasa naomba kufahamishwa kama kuna sehemu yoyote inayojulikana kisheria ndani ya manispaa ya Kinondoni inayoweza kunisaidia tafadhali.
kwani kampuni husika imekataa kukulipa?
Maana kama ni kampuni loyal lazima iwe inajua huu utaratibu wa kufanya payments mbalimbali ambazo ni stahiki yako, ikiwemo leave pay, notice pay kama hawakukupa notice, transport allowances na any severance pay due. Hatua ya CMA itakuja baada ya wao kudeclare kuwa hawatohusika na malipo hayo mi nafikiri jarbu kubargain nao kwanza kuliko kuextend mchakato that far.
 
Mkuu ngoja nikuambie,Mimi nilikuwa nafanya kazi pale bila kuwa na kitambulisho chochote pale zaidi ya sare tu,Sasa jana nimeenda wakaniambie niwakabidhi nguo zao halafu wao wataamua siku na tarehe ya kunipa stahiki zangu.

Na hii imewatokea watu wengi pale na mwisho wa siku hawakupata chochote,kampuni ilikana kuwatambua baada ya kukabidhi Uniform.Hata Pay In slips,huwa wanazuia kuzipiga picha,ukipewa hela yako,Pay in slip wanaondoka nayo.

Baada ya mkataba kwisha niliwauliza juu ya malipo ya likizo,notice,mshahara wangu,pesa za sare walizokuwa wakinikata,wakaishia kucheka sana kwa dharau.

Sasa naomba kufahamishwa kama kuna sehemu yoyote inayojulikana kisheria ndani ya manispaa ya Kinondoni unayoweza kunisaidia tafadhali.
Niliwahi kufanya kazi na kampuni moja ya jamii hyo, nikaamua kuachana nao kwasbb my profession was at stake. Nilipata changamoto sana kwani mzigo wote ulikuwa unaelemezwa kwangu as an HR ila lastly wale employees walielewa mchezo mzima unatoka kwa Mkurugenzi ambapo pressing kubwa hii ya kuzurumu inatoka kwake, yaani anajua kuwa hiki kitu kinafanyika ktk kampuni ila anajikuta hajui kinachoendelea licha ya kwamba anatambua fika ya kuwa sheria iko wazi.
#resolving this katika CMA level ni vizuri ila pia resolution yake inawezekana isitoe faraja kwako kwa muda huo unaohitaji, kwani mwajiri anauwezo wa kupanga muda wa kukulipa stahiki zako na kwa mfumo gani ila pale tu nyote mtaporidhia. Kama hutoridhia na hilo utapeleka hili swala kwenye hatua nyingine ya Arbitration ambayo itahitaji solely ujitolee kwa moyo wote hususani kwa muda utaopoteza. Kikubwa haki yako iko wazi na utaipata tu licha ya kwamba inaweza chelewa sometimes. Swala la kutopewa salary slip, wala vitambulisho lisikutishe, as long as tayr Kuna relationship inayoexist kati yako na wao then ww ni employee wa kampuni husika.
 
Asante kwa maneno yako ya faraja mkuu,hapa sijui hata nifanye nini au niende wapi.
Au niende pale kwa RC Makonda?
 
Baada ya mkataba kwisha niliwauliza juu ya malipo ya likizo,notice,mshahara wangu,pesa za sare walizokuwa wakinikata,wakaishia kucheka sana kwa dharau.

Sasa naomba kufahamishwa kama kuna sehemu yoyote inayojulikana kisheria ndani ya manispaa ya Kinondoni inayoweza kunisaidia tafadhali.

Huo mkataba ulikuwa wa mdomo au maandishi?
 
Umekosaje kuwa na Nakala?.
Anzia hapo ebu kadai Nakala! Pili kadai cheti cha kufanya nao kazi! Vitu hivyo ni sehemu ya ushawishi CMA kukusikiliza kwa urahisi.
Mkuu,hii kampuni inaendeshwa kiujanjaujanja ingawa ni maarufu sana hapa mjini.Ni makusudi kabisa huwa wanakataa kutoa nakala ya mkataba kwani wanajua kuwa ni wakiukaji wa sheria na hufanya hivyo kukwepa consequences.

Ushahidi nilionao hapa ni uniforms tu pamoja na pay in slip niliyoipiga picha covertly.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom