CMA Arusha yanuka Rushwa , wafanyakazi wakosa Imani nayo,wamtaka rais Samia aivunje

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wafanyakazi zaidi ya 543 wa Kampuni ya maua ya Kili Flower ya wilayani Arusha Mkoani Arusha wamejikusanya na kuzua taharuki kwa kuangua vilio hadharani katika ofisi za Tume ya Usuluhisho{CMA} Mkoa wa Arusha wakiituhumu ofisi hiyo kuchelewesha kutoa hukumu ya madai yao ya kuachishwa kazi bila ya kulipwa stahiki zao kama sheria inavyoelekeza.

Wakiongea na vyombo vya habari wamedai kitendo hicho cha usuluhishi ni Bora kingevunjwa kwani kimeshindwa kukidhi matakwa ya wafanyakazi badala yake kujihusisha na kuchukua rushwa kwa waajiri na kuwakandamiza wanyonge.

Wamemtuhuku mkuu wa tuma hiyo hiyo Mkoa wa Arusha ,Lukumay Steven na wenzake ambao wote wanamatumbo makubwa kuwa ni vinara waa kuchukua rushwa za waajili.

Baada ya vurugu hizo zilizochukua zaidi ya masaa kadhaa uongozi wa CMA uliamua kuita polisi na walinzi wa kampuni za ulinzi ili kuwatimuwa wafanyakazi hao lakini ilishindikana baada ya wafanyakazi hao kuonyesha kutotishika nao na kuwaambia wako kwa misingi ya kudai haki na wako tayari kufa kwa hilo na hawatatoka hadi hukumu yao isomwe.


Mmoja wa wafanyakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Athumani Maulid alisema kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2019 iko katika baraza hilo na kinachotakiwa ni kutolewa hukumu lakini hukumu imekuwa kitendawili kwani imehairishwa kwa zaidi ya mara tatu bila ya sababu za msingi hali inayoonyesha kuna dalili za kutengeneza rushw aili wazurumiwe haki yao waliyoitukia kwa zaidi ya miaka 10.

Maulid alisema wananchi,wafanyakazi na wafanyabiashara wanaichukia serikali kufuatia baadhi ya watendaji katika serikali waliopewa dhamana ya kutetea haki wako kwa ajili ya maslahi hilo lazima lichukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kutupia macho CMA Arusha kwani imejaa rushwa.


Alisema kuwa kitu cha kushangaza na kusikitisha kesi ya Kili Flowers dhidi ya wafanyakazi inahirisha na kuangukia siku ya jumamosi na siku za sikukuu na kuonyesha wazi kuwa kuna njama za wazi juu ya kesi hiyo.

Naye Rose Swai yeye alisema kuwa hana Imani ten ana msuluhishi wa kesi hiyo kwa kuwa amejenga mazingira ya kuonyesha kutaka rushwa ya wazi wazi kwa viongozi wa Kili Flowers ili aweze kuwanyima haki wafanyakazi wanaozota miaka mingi kudai haki yao waliyoitolea jasho.

Swai alisema umati Mkubwa uliopo hapa mahakamani una Watoto wa shule,baadhi wanadai pango la kodi ya nyumba na wengine wanaishi Maisha magumu sana kwa sababu ya watendaji wa CMA kwa kuchelewesha kusoma hukumu ambayo haiwezi kuchukua zaidi ya saa moja.


Alisema na kuwaomba viongozi wa serikali wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha kuingilia kati kutatua tatizo hilo kwani hali za wanyonge hao ni mbaya sana kwani wanahitaji mahitaji ya kujikimu ili waweze kukithi mahitaji yao ya kila siku.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa malalamiko ya madai ya wafanyakazi hao Mtendaji Mkuu wa CMA Mkoa wa Arusha ,Stepheni Lomayani sio kesi yao tu iliyohairishwa siku ya jana kwani kuna kesi nyingi zilihairishwa hivyo wanapaswa kuwa na uvumulivu kwani hukumu yao haijaandikwa.

Lomayani alipoelezwa kuwa hukumu kesi hiyo imehairishwa zaidi ya mara tatu na hakuna majibu ya kulidhisha wanayopewa wafanyakazi,alisema kuwa atafuatilia na kusoma mwenendo wa kesi hiyo na kutolea majibu baadae.

Hata hivyo baadhi ya mawakili walioshuhudia hali hiyo walionyesha kusikitishwa sana kilio cha wafanyakazi hao na kusema kuwa watendaji wa CMA wanapaswa kujirekebisha kwani kilio cha wafanyakazi hao ni cha msingi na kinapaswa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa kutatuliwa.

Wakili huyo ambaye aliomba kutotajwa jina lake alisema wafanyakazi hao wana watu wanaowategemea iwe Watoto au wazazi na wanakaa katika nyumba za kupanga na wanadaiwa pango pia wanasomesha kuwapiga dana dana kila wakati haileti picha nzuri kwa jamii na kutoa mwanya kuwa kitengo hicho kinanuka kwa rushwa kitu ambacho sio kizuri.

‘’Kisheria hukumu haiwezi kuhairishwa kwa zaidi ya mara tatu huu ni uhuni wanafanyiwa wafanyakazi hao wanahaki ya kupiga kelele,kulia na kuzungumza yoyote wanayoyataka kwa sababu watendajiw a CMA wameyataka wenyewe’’alisema wakili huyo

Mwisho
 
Hata Mahakama kuu Arusha - Idara ya kazi ...wanapiga Tarehe kazia Hukumu ya madai ya kazi mno.

Wafanyakazi kudai haki zao inakuwa ngumu. Makampuni yanatoa Rushwa Sana.

Kesi zinapigwa Tarehe kizembe zembe mno
 
NSSF Arusha nayo wameshindwa kulipa watu mafao yao.

Watu wanapigwa Kalenda ...mpaka miezi 6 watu hawalipwi.

NSSF wanatoa vijisababu Kem Kem
 
NSSF Arusha nayo wameshindwa kulipa watu mafao yao.

Watu wanapigwa Kalenda ...mpaka miezi 6 watu hawalipwi.

NSSF wanatoa vijisababu Kem Kem
Moezi 6?wapo wengine wamesota miaka mitatu na bd kitendawili hawaishiwi sababu cjui mpk mtu ufe uwaachie madai yako!
 
CMA sio Arusha jamani Dar ndio kumejaa rushwa kubwa kuna Arbitrator anaitwa Belinda jamani aibu sana ....anachukua pesa huku na huku anavuruga kesi anadai itaamuliwa haki high court yeye anatoa ngoma juani .....muhuni sana huyo dada ni aibuuu sanaaa dada mrembo mpenda rushwa .....anaitwa Belinda
 
CMA sio Arusha jamani Dar ndio kumejaa rushwa kubwa kuna Arbitrator anaitwa Belinda jamani aibu sana ....anachukua pesa huku na huku anavuruga kesi anadai itaamuliwa haki high court yeye anatoa ngoma juani .....muhuni sana huyo dada ni aibuuu sanaaa dada mrembo mpenda rushwa .....anaitwa Belinda
Wengine wapo Tabora wanakula kotekote then kesi ni mwendo wa kuhairishwa mpaka ukate tamaa, kuna mdada pia hapo ananyodo balaa
 
Sasa kama hata NSSF wanashindwa kulipa mafao hizo Kampuni zinazoshtakiwa na Wafanyakazi hata zikiamrishwa ziliwalipe zitatoa wapi pesa?.
 
NSSF Arusha nayo wameshindwa kulipa watu mafao yao.

Watu wanapigwa Kalenda ...mpaka miezi 6 watu hawalipwi.

NSSF wanatoa vijisababu Kem Kem
Sasa kama hata NSSF wanashindwa kulipa mafao hizo Kampuni zinazoshtakiwa na Wafanyakazi hata zikiamrishwa ziliwalipe zitatoa wapi pesa?.
 
Mahakama ya kazi imezidiwa na kesi.. Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi nafikiri hawana taarifa vizuri kuhusu mahakama hii. Kesi zinaharibiwa makusudi CMA hata ukienda labour court jaji anashindwa kutoa uamuzi kwa haki
 
Hivi PCCB wapo kweli? Ili TAKUKURU wafanye uchunguzi na kukamata Wala Rushwa Ni mpaka waitwe! PCCB kamata hao CMA

NA Waziri wa Kazi Ni Nani? Hasikii hizi lawama. ...au mpaka Mabango yamfikie Rais
 
Back
Top Bottom