Clouds Wanadhalilisha Taasisi ya Urais

matasha

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
378
400
Kihistoria taasisi ya urais Tanzania inaheshimika sana. Ukiangalia utawala wa Nyerere, Mwinyi kidogo pamoja na kwamba aliichezea sana taasisi lakini Mkapa alirudisha heshima. Ukweli JK ameifanya taasisi ya urais imekuwa tu kama manager wa bendi fulani.

Nimesikitishwa na kitendo cha Clouds kumtumia JK kutangaza biashara yao. Wanaweka sauti ya JK ikiisifu Clouds kama sehemu ya tangazo la biashara kuitangaza Clouds na kiukweli kiitifika hawapaswi kufanya hivyo. Hivi itakuwaje leo Rais akitumika kutangaza Coca Cola au Azam Cola? Naiomba serikali ijue urais ni taasisi si mtu hivyo vitendo vya kudhalilisha taasisi yetu vikome mara moja. Kama JK anataka kutangaza biashara asubiri amalize kipindi chake cha urais.
 
Ni kweli kabisa, lakini kwa nini kila wanachofanya clouds fm kionekane kibaya?!!
 
Japo sijasikia hilo Tangazo lakini Sidhani kama ni vizuri kutumia Taasisi hiyo kwa matangazo. Na mkuu mwenyewe sijui hilo halioni niliwahi kusikia sauti yake kwenye DUNIA YAKO CHAGUO LAKO. Hadi kwenye Fursa nadhani yupo heunda na hisa huko.
 
inasikitisha maana kila baada kama ya lisaa unalisikia hilo tangazo la kikwete nilidhan ni mimi tu nimeona kua si sawa nashkuru mdau kwa kuleta hii hoja apa!! maaana italeta picha mbaya.... hii serikali haioni tatizo kwa vitu kama ivi si juzi tu kamanda wa kanda maalum ya dar es salaam suleiman kova alikua anatangaza biashara ya m pesa ya vodacom naona lile tangazo kwa sasa silisikii tena!!!
 
Kinachofanywa na clouds ni swala ambalo pengine serikali kupitia wizara ya kazi na vijana ingeweza kuwa imefanya. Lakini kwa wao kama private sector wamefanya uzalendo. Ndo maana Rais amewaunga mkono na kuwapongeza. Ile inayorushwa ni clip ya sauti ya rais akiwapongeza wakati wa kuhitimisha fursa. Sioni kama kuna ubaya wowote kufanya hivyo.
 
JK ameufanya Uraisi ni Kuongoza sio Utawala,hataki aonekane kama dikteta au Mfalme,JK mtu wa watu.hana majigambo wala kusujudiwa,wala Ikulu hataki ionekane kama peponi ni nyumba yetu na kila Mtu alieiletea Taifa heshma anawezakwenda,zamani hata Waandishi wa habari walikuwa Ikulu wanaiona kama Peponi.Jamaa akiondoka tutamkumbuka.
 
Uzi kama huu hauna wafuasi wa chama twawala maana ukweli 100% ,Rais anatakiwa kushauriwa kabla ya kufanya kitu !kinachofanyika anatekwa kifikra anaingia kwenye mitego na kufanya kazi za mastaa wa bongo angewaachia wakina wema ,diamond etc
 
Kinachofanywa na clouds ni swala ambalo pengine serikali kupitia wizara ya kazi na vijana ingeweza kuwa imefanya. Lakini kwa wao kama private sector wamefanya uzalendo. Ndo maana Rais amewaunga mkono na kuwapongeza. Ile inayorushwa ni clip ya sauti ya rais akiwapongeza wakati wa kuhitimisha fursa. Sioni kama kuna ubaya wowote kufanya hivyo.
kwani clouds wamefanya nini , kilichomsukuma rais kuwasifia au hata kilichokusukuma wewe kuwatetea ? huu utapeli wa maneno ndiyo unaokuchanganya ? kuna fulsa kubwa kama muziki wa kizazi kipya ? mbona wao ndiyo wanaoongoza kwa kudhulumu wasanii ? hebu fuatilia kidogo tu ugomvi wao na lady jaydee , hakuna cha fulsa wala nini ! ni kauzibe kwa kwenda mbele , isipokuwa wanasiasa wanatumika bila kujua malengo halisi ya clouds , TAFAKARI !
 
Mwl Nyerere aliwaambia ukulu si mahala pa wahuni na machekibob nyie mkamuona anawivu na chuki kwa kaka mkuu.. Haya sasa na mtashuhudia mengi
Acha jazba mkuu........hadi maneno yako unayachanganya? UKULU...........Na hata hivyo, unatuambia tulichagua wahuni na machekibobu kwenda Ikulu? Kweli?
 
Kinachofanywa na clouds ni swala ambalo pengine serikali kupitia wizara ya kazi na vijana ingeweza kuwa imefanya. Lakini kwa wao kama private sector wamefanya uzalendo. Ndo maana Rais amewaunga mkono na kuwapongeza. Ile inayorushwa ni clip ya sauti ya rais akiwapongeza wakati wa kuhitimisha fursa. Sioni kama kuna ubaya wowote kufanya hivyo.
Utaonaje wakati na ww ni wale wale
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom