Kihistoria taasisi ya urais Tanzania inaheshimika sana. Ukiangalia utawala wa Nyerere, Mwinyi kidogo pamoja na kwamba aliichezea sana taasisi lakini Mkapa alirudisha heshima. Ukweli JK ameifanya taasisi ya urais imekuwa tu kama manager wa bendi fulani.
Nimesikitishwa na kitendo cha Clouds kumtumia JK kutangaza biashara yao. Wanaweka sauti ya JK ikiisifu Clouds kama sehemu ya tangazo la biashara kuitangaza Clouds na kiukweli kiitifika hawapaswi kufanya hivyo. Hivi itakuwaje leo Rais akitumika kutangaza Coca Cola au Azam Cola? Naiomba serikali ijue urais ni taasisi si mtu hivyo vitendo vya kudhalilisha taasisi yetu vikome mara moja. Kama JK anataka kutangaza biashara asubiri amalize kipindi chake cha urais.