Clouds wamedhalilisha walemavu wa ngozi

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,730
2,388
Ni sasa hv tu nipo sebuleni nafanya kazi zangu, huku nimewasha Clouds FM, wakitangaza moja kwa moja FIESTA DODOMA. Mtangazaji anasema ".......unaweza ukamwambia mshikaji wako kamata ALBINO hii hapa......" Hapo kwenye ALBINO amemaanisha NOTI YA ELFU 10.

Binafsi sijapenda hilo neno kutumika kwa jinsi lilivyotumika. Hawa ni ndugu zetu na hawajapenda kuwa na ulemavu wa ngozi. Kuwafananisha hali yao au rangi yaona noti ya elfu 10 haijakaa njema.
 
Sidhani kama ni udhalilishaji kwa walemavu wa ngozi.

Vitu vingi tu tumevipa majina kulingana na uhalisia wenyewe lakini vikileta maana iliyojificha.
 
Eti albino ukimuita zeru zeru napo ni unyanyapaa huwa nashangaa sana wakati albino ni kingereza na zeru zeru ni kiswahili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom