Clouds tv/ radio wameamua wanachukua nafasi ya tbc?

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,429
32,173
Kwa sasa naona clouds tv/ radio wameamua kuchukua nafasi ya tbc na azam tv kila ukiziangalia interview zao wamebezi kwa watu walio ccm au wanaohama na kujiunga na ccm walimuita waitara wakaja kumuita bashiru sasa wanamuita mtatiro kuna nini clouds au tokea mkuu alipowapigia simu wameamua kumfurahisha?

Kitu kinachoshangaza kwa nini hawachukui maelezo ya pande zote mbili naona coverage kubwa inafanywa kwa viongozi wa serikali na wanachama wa ccm je wanaotoka upinzani hawatakiwi kuhojiwa hapo clouds ili habari ziwe na usawa? Huko ndo kujipendekeza au tuamini kila idara imenyoosha mikono juu kwa mkuu?

Naona vyombo vya habari vya nchi hii ndivyo vinavyoliangamiza taifa vipo si kwa ajili ya kusaidia wananchi kujua mambo kwa undani na ukweli sahihi vimechagua kuwalisha habari za upande mmoja ambao wao wanapenda moja wapo ni hiki kituo cha clouds kipo kimaslahi zaidi na kutetea tabaka fulani ambalo wao wana maslahi nalo.

Kwa mfano interview aliyofanya waitara ilitakiwa pawepo na mtu wa kutoka chadema lakini cha ajabu waitara kaachwa peke yake akijiachia na propaganda zake chafu.

Kama mnapita hapa clouds tv au radio jaribuni kufanya kazi kwa usawa hamuijui kesho..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom