Clouds: Ruge kama yule mwalimu aliyewagomea askari wa kikaburu waliomfata darasani katika SARAFINA

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Hili sakata limenifanya niikumbuke filamu hii maarufu ya SARAFINA.

Katika filamu hii,askari wa kikaburu walikuwa wakifanya jitihada kudhibiti maudhui ya masomo katika shule huko afrika kusini.

Walifanya kila njia ikiwamo kujificha na kusikiliza yanayofundishwa,na mwisho wa Siku wakiamua kulivamia darasa lililokuwa likifundishwa na mwalimu huyo,hapo ndipo moto uliwaka.

Mwalimu kagoma kuelekezwa mambo ya kufundishwa na wale askari,wanafunzi wakamuunga mkono.

Nalifananisha na sakata la Ruge kugoma kuelekezwa nini cha kutangaza ili kufurahisha watawala.

Kugoma kwa Ruge sasa kumewafanya clouds media wawe na Uhuru,maana kila dakika simu zinapigwa hiki tangazeni hivi,mara nampongeza diamond,mara shilawadu .....watangazaji wenyewe bado vijana mpaka wakaanza kuonekana wazee.

Hakika
Freedom is coming tommorow

Sasa ni mwendo wa kuwagomea tu.

Hatudai risiti mpaka makonda aondoke
 
Mwalimu aliitwa Madam Masambuka...kuna wakati walipelekewa Mwalimu mwingine baada ya Madam Masambuka kukamatwa na askari wa kikaburu yule mwalimu akaanza kuwafundisha kwa kuwapotosha, alikula kichapo kutoka kwa watoto wale hadi raha, alipigwa na madaftari, kalamu, viatu na kwa chochote kile walichoweza kukiokota wale watoto!
 
Usimfananishe madam Mary Masembuko na vitu vya kijinga!! Mwalimu masembuko alikuwa hatumiki na hakuwahi kutumika na makaburu yeye kazi yake ilikuwa ni moja tu ya kutoa elimu ya ukombozi, tofauti na ruge ambaye alitumika kwanza kukandamiza watu na kueneza propaganda ila kibao kilipombadilikia ndio akabadili gia angani..!!
 
Mwalimu aliitwa Madam Masambuka...kuna wakati walipelekewa Mwalimu mwingine baada ya Madam Masambuka kukamatwa na askari wa kikaburu yule mwalimu akaanza kuwafundisha kwa kuwapotosha, alikula kichapo kutoka kwa watoto wale hadi raha, alipigwa na madaftari, kalamu, viatu na kwa chochote kile walichoweza kukiokota wale watoto!
Hahahaaa....watoto walitembeza kichapo
 
Back
Top Bottom