Clouds ni sawa na Mwalimu katika tasnia ya muziki wa Bongo

rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
21,450
41,815
Katika maisha ya mwanadamu kukumbuka fadhila na msaada ambao alipata toka kwa mtu au watu akiwa hana kitu na yupo kwenye shida ni jambo wanaloweza watu wachache sana sana.

Kuna watu wanaongea kwa kufuata mkumbo kuhusu Ubaya wa Clouds juu ya wasanii wa Bongo fleva mpaka kufikia hatu ya kusema Ruge anavuna ubaya aliopanda!

Leo hii clouds iliyoibua vipaji zaidi ya 100 vya muziki kwa kupitia mkono wa Ruge inaonekana Radio ya Unyonyaji na hizo ndo fadhila za Wasanii wengi waliobebwa na Clouds... Watu wanasema Clouds ilikuwa inawanyonya wasaniii lakini wanasahau Clouds sio Charity center inahitaji Pesa kujiendesha so lazima ijilipe kwa kupitia matamasha kama Fiesta...

Hao wanaosema walikuwa wananyonywa wamejenga na kununua magari kupitia Fiesta, wameanzisha Studio zao hata Label kupitia Clouds na Fiesta

Lakini sasa wameota mapembe na kusahau fadhila zote.. Clouds haina tofauti na mwalimu anaefundisha wanafunzi na kuwalea lakini mwisho wa siku analaumiwa na kuonekana hana maana wala mchango kabisa huku wanaomlaumu wanasahau bila Mwalimu wasingefika hapo walipo..

Ruge atabaki kuwa Icon ya muziki wa Bongo milele yote Mungu amsaidie apate nafuu aje kuona unafiki wa Watanzania.

Tuungane kumchangia Ruge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom