Clouds Media, kuweni makini na kujiingiza kwenye siasa. Mtasuswa na watanzania!

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
83,975
2,000
Joseph Kusaga ukitaka kujua kwamba CCM ina wenyewe rudi nyuma miaka zaidi ya 25 iliyopita wakati ule unapiga Disco coco beach ukiwa na DJ Bonny love, ilikuwa ikifika saa 6 balozi Ammy Mpungwe anaagiza polisi kuja kuzima disco lile lilojaza vijana kibao huku wakicheza kwa amani na utulivu, Hawa ndio wenye CCM, katika kundi hilo wewe haumo, maana sisi pamoja na wewe tulikuwa tunaenda kulala baada Mzee Mpungwe kuzima disco, naamini bado hujasahau .

Chadema iliwahi kuwaamuru watanzania kuipuuza TBC na kuanzia hapo mpaka naandika uzi huu TBC imepuuzwa nchi nzima na hata watangazaji wake wakitangaza bila kuvaa nguo hakuna mwananchi atakayeangalia TBC.

Achana na Chadema jikite kwenye weledi, hawa watangazaji wanaokuja ambao hawajui hata clouds ilikotoka watakuponza, kutengeneza brand yaweza kuchukua miaka mingi lakini kuiharibu haichukui hata dk 5, kuwa makini mno!

MAJUTO NI MJUKUU, Usije kusema hatukukuambia .

 

Gebreyesus

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,684
2,000
Nilishawaonya clouds kuelemea CCM kupitia kipindi Chao Cha Clouds 360 ila naona hawajakoma .

Kusaga akumbuke alianzisha kijifundrise chake cha kipumbavu akihamasisha wenye hela kuchangia kits za COVID19 bila Magufuli kumuonea aibu alimpiga ban kwa kukataza huo upuuzi Tena akamwambia Kuna watu nasikia wameanza kuchangisha michango ya COVID19 hivi Kusaga hajui ameanza kuanguka? Alitumia mbeleko ya kumsifu Ummy Mwalimu, Kusaga kumbuka tuliokuweka hapo juu ni sisi wewe endelea kumsifu mfalme ukasahau ulikotoka

Soma aya ya mwisho Kusaga.

Clouds ni mali ya familia kumbuka ulikabidhiwa wewe toka kwa baba yako mkubwa ambae ndio alibidi apewe clouds wewe ni dogo Sana kwa sababu wewe ni mjukuu mdogo wa mtoto mdogo wa mzee Kusaga yule dogo wa Morogoro baba yake ni mkubwa kwako na Sasa wale watoto wanakuja unajua kwa nini wiki hii dogo kaenda Mbeya....???

Sasa tunakuambia hivi...

Yule mdogo wako anaevuta bangi Mafisa Morogoro na kunywa gongo sasa hivi akili imepevuka anaanza kudai umiliki wa Mali maana hiyo sio Mali yako ni ya familia endelea kufagilia upande mmoja ukaacha wa pili wanasiasa wanapita ....!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom