Clouds Media Group walia na ugumu wa biashara, Kusaga adai wanaweza kufunga hali ikiendelea hivi

Ajiunge na channel nyingine kama ITV, Channel 10 na Star TV waanzishe king'amuzi chao? Mpango wa king'amuzi cha Continental uliishia wapi?
 
sababu zako wala hazihusiani na kuathirika kwa biashara ya television nchini.

bado mainstream media ina nguvu sana... online tv na blogs sio sababu.

sababu inajulikana na inahusiana moja kwa moja na aina ya utawala uliopo madarakani hivi sasa nchini.
Kivp kaka? Sheria zilizopo ni nzuri wenye ving'amuzi wanapaswa kuwalipa content provider! Hii ita-boost ama kutoa fursa kwa wenye kutengeneza vipindi kuanzia wenye comedy mpaka wenye movie mpaka wenye kuimba.

Kwa hali ilivyo kutegemea matangazo tu haikuwa hali endelevu! Kinachotakiwa, wenye TV channels waungane waje na kisambusi/kingamuzi chao ili wapate matangazo na kuuza vipindi!

Tatizo makampuni mengi ya Bongo wabinafsi! Sidhani kama ITV, Clouds TV, Star TV, Channel 10 na other local channels hawawezi hili.

Ubinafsi wao ndo umefanya kutoa nafasi kwa Star Times na DSTV kuwanyonya maana wamefanya cartel sort of! Yaani ku-air the channels halafu kukataa kulipa watengenezaji vipindi!

BTW wakati ITV na Star TV wanajaribu kuja na visumbusi vya Continental, hawahawa wakina Clouds TV walikuwa wakwanza kukimbilia Star Times na DSTV pasijua watakuja kuwa cornered siku. Wenzao ITV wana-print pia.

Its only the day local channels watakuwa na visumbusi vyao ndipo wataona matunda. Nina uhakika Star media na DSTV watakapanda dau wataanza kugombania kununua vipindi na kutengeneza ajira za uhakika!
 
Mkuu kama usipolipia kingamuzi channel zote zinakata na ukilipia ndo zinaanza kuonesha..unadhani watashindwa kugundua kuwa mda huu unaangalia tv au laa
nikweli, mie nilijikita kwenye idadi ya watazamaji hasa mainstream media, si jinsi wanavyoweza ku control ving'amuz na wamiliki.
 
Wafunge tu coz hali imebadilika sana. Online tv zimekuwa nyingi mno,blogs, forums na vikorokoro kibao. Wakati huu unahitaji ubunifu wa hali ya juu sio mazoea. Zamani Radio kubwa zilikua Radio one, RFA, RTD. Leo hii kila kona kuna Radio na zinakimbiza. Tukubali hali imechange sana na TUKUBALI KUBADILIKA.
Ukweli ni huu.. social media zinaua radio... Millard Ayo yuko juu sana kwa sasa kuliko mwajiri wake ...
 
Bado online TV kwa Tanzania si tishio' hatuna intenet ya uhakika, na kwa gharama za Internet mtu kutegemea online TV si rahisi. Nafikiri kuna tatizo kwenye sekta ya biashara kiasi kwamba wenye stations hawapati matangazo na wadhamini. Sekta za Biashara Zinategemeana sana ni kama mwili wa binadamu tu' ukiumwa na jino sana ujue utahisi na masikio yanauma, baadae utahisi kichwa pia Kinauma, baadae utahisi hata macho hayapo sawa ukiyafungua, mwisho kizunguzungu then mwili mzima Hoi.
Social Media duniani imelenga ku replace Radio na TV station...... watz wako tayari kulala na njaa na sio kukosa bando la simu
 
sababu zako wala hazihusiani na kuathirika kwa biashara ya television nchini.

bado mainstream media ina nguvu sana... online tv na blogs sio sababu.

sababu inajulikana na inahusiana moja kwa moja na aina ya utawala uliopo madarakani hivi sasa nchini.
Unalaumu utawala kwakuwa unatanguliza siasa mkuu
Social Media ni powerful na high tech iliyokuja kuua TV na Radio stations duniani....
Tanzania matumizi ya bando/simu yako juu Africa
 
nikweli, mie nilijikita kwenye idadi ya watazamaji hasa mainstream media, si jinsi wanavyoweza ku control ving'amuz na wamiliki.
Ndo mana nimekwambia kama mtu anaweza ku control uangalie or usiangalie tv...watu wawili mnaweza kuwa na king'amuzi kimoja but jamaa wanaweza ku kuntrol we wakakupa channel flani na flani mwingine wakamnyima...watu kama hao hawawezi kushindwa kujua uliwasha tv saa ngapi na ulizima saa ngapi na uliangalia channel gani...hawawezi kushindwa kujua mda huu clouds tv tanzania inaangaliwa na watu wangapi...hiyo ndo technology mkuu
 
Kilicho msaidia Kikwete japo kidogo ni kabachelor degree kake kauchumi,akawa anaheshimu misingi na miiko ya kiuchumi.

huyu inaonekana anataka kugundua formula mpya ya uchumi itakayoingia kwenye vitabu.
 
Bosi wa Clouds Media amesema tangu kutokea changamoto ya local channels kuondolewa kwenye ving'amuzi vyombo vya habari hivo vimeathirika kwa kiwango kikubwa na hapo wanapenda kutoa ajira kwa vijana lakini wanakoelekea watakwama na kupunguza wafanyakazi.

Kusaga" wakati kupo kwenye ving'amuzi vyote zuku, startimes, Azam na DStv mfano makampuni Kama Vodacom, Tigo na Airtel walikuwa wanaona views milioni 1 wanakulipa fungu zuri kutokana na idadi kubwa ya watazamaji, lakini kwa sasa views wameshuka Hadi laki moja kwaiyo makampuni hayo yamekata bajeti zao na kukulipa kuligana na idadi ya watazamaji na huwezi kuwalaumu hata Kama wanakupenda lakini wanakulipa unachostahili Sasa kwa Hali hii wafanyakazi Hawa vijana wanafamilia tutawalipa vipi?

Maana yake hatuwezi kufika inabidi tuwapunguze japo tunawapenda". Kuna haha la kuniangalia upya suala hili.

Kusaga ameongeza hata wasanii wameathirika hawapati tena show nje kwakuwa hawaonekani Tena Kama zamani

View attachment 957913
Asiilaumu serikali bali waliofungiwa local channels kwa kutofata sheria za leseni zao.
 
Social Media duniani imelenga ku replace Radio na TV station...... watz wako tayari kulala na njaa na sio kukosa bando la simu
Labda wa Dar es Salaam. Tembelea mikoa mingine ya Tanzania uone kama uchumi wao unawaruhusu kushinda online na hayo ma bundle unayosema.
 
Nashauri serikali ibadilishe sheria yake ya ving'amuzi iwe ni lazima mtu yeyote anayetaka kufanya biashara ya ving'amuzi hapa nchini ni lazima aonyeshe hizo channel 5 za nyumbani kama anashindwa aache.!
Haya maswala ya madaraja ya lesseni ndo yanatufikisha hapa watu tunaangalia channel za kenya
Nafasi bado ipo ya kurekebisha.!
 
Back
Top Bottom