#COVID19 Clouds Media Group, kumbukeni dunia bado inapambana na Corona

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Mwenendo wa dunia bado upo katika tahadhari dhidi ya Corona. Viongozi wa siasa, serikali na dini bado wanatuhimiza tuchukue tahadhari

Kwetu Tanzania madhara sio makubwa sana Kama wenzetu tunavyoona. Na hapa kwa kweli nitamsema vibaya kwa vingine ila kwa swala la corona kongore ni kwa hayati Magufuri na vyombo vyake vya usalama na viongozi serikalini

Tunafahamu hata wao wenyewe walipingana ila hadi tulipo hapa basi pongezi kwa wote

Tukirudi kwenye mada, juzi tarehe 24.04.2021 clouds media group walikuwa na ugawaji tuzo za Malkia wa nguvu.

Katika tukio lile hapakuwa na tahadhari zozote dhidi ya corona

Watu walishikana mikono, walibadilishana mic, walikumbatiana na Mambo kadha wa kadha

Tunapokuwa na matukio Kama yale tusijisahau sana. Tutambue dunia inatutazama. Tusijichore kwa picha ya watu tusio jali.

Screenshot_20210427-193009~2.jpeg
 
Duuh bongo kweli shida ipo utadhani wale wafuasi wa kibwetere...hawataki kuambiwa chochote
 
Kwani mihadhara mingine kuna tahadhari yoyote?

Usitukumbushe, tushasahau kuhusu corona.
 
Tabia yao ya kukoleza mi blue blue colour ktk picha zao..hakika ni ya kipumbavu mnoo....
 
Kweli bana clouds hamuipendi nimeamini!!! Hivi waliwakosea Nini???

Hivi Kuna precaution yoyote ya Corona kwenye viwanja vya mpira (VPL),????

Hivi mlundikano wote ule wa msiba wa jiwe mlizungumizia precaution yyte ya Corona,????!

Mlundikano kariakoo,karume ,hivi Kuna kujilinda kkte na Corona,????

Maandamano ya bajaji iringa Kuna precaution yoyote ya Corona,?????

Hivi wasafi hawakufanya ""super woman""????

E fm na Dina Mario's hawakugawa tunzo kwa wanawake juzi juzi tu????

Maisha ya kila siku Kuna precaution yoyote ya Corona?????

Kweli clouds media hamuipendi ,hivi waliwakosea Nini???

Yaani kitu kidogo tu lazima watalaumiwa utafkili cjui wamefanya nn??
Hivi hamuipendi,?? mnawaonea wivu??, wanawafuatilia Sana?? Ni wakubwa Sana kuliko media nyingine???
 
Blue ni brand colors ya campany yao,
Na pia kwa sis web na graphics designer blue ni moja inayovutia ,na isiyoumiza macho kwa wat wengi
Ndo maana site nying hat Jf zinz blue color nyingi,

Hovyo kabisa...
 
Hawa wanaonesha imani tuliyo nayo, kuwa corona si tishio kwa Tanzania. EAC na SADC wao ndio wangetakiwa waunde tume ya wataalamu kuja kutuuliza tulifanyaje Watanzania si kinyume chake.
 
Mwenendo wa dunia bado upo katika tahadhari dhidi ya corona. Viongozi wa siasa, serikali na dini bado wanatuhimiza tuchukue tahadhari

Kwetu Tanzania madhara sio makubwa sana Kama wenzetu tunavyoona. Na hapa kwa kweli nitamsema vibaya kwa vingine ila kwa swala la corona kongore ni kwa hayati Magufuri na vyombo vyake vya usalama na viongozi serikalini

Tunafahamu hata wao wenyewe walipingana ila hadi tulipo hapa basi pongezi kwa wote

Tukirudi kwenye mada, juzi tarehe 24.04.2021 clouds media group walikuwa na ugawaji tuzo za Malkia wa nguvu.

Katika tukio lile hapakuwa na tahadhari zozote dhidi ya corona

Watu walishikana mikono, walibadilishana mic, walikumbatiana na Mambo kadha wa kadha

Tunapokuwa na matukio Kama yale tusijisahau sana. Tutambue dunia inatutazama. Tusijichore kwa picha ya watu tusio jali.

View attachment 1765819
Mbona kama sielewi elewi hivi, kama corona bado ipo ulimwenguni sasa hilo linawahusu vipi clouds?

Clouds wanafanya kile ambacho jamii ya watanzania inafanya. Watanzania wanaenda makanisani, misikitini, mashuleni na vyuoni kuna madarasa yanaendelea kama kawaida. Nyomi za Kariakoo ni kielelezo cha jamii ya Tanzania kuhusu corona.

Swali liwe je kwanini jamii ya Tanzania hailichukulii suala la corona kama kwingineko duniani wanavyolichukulia? Majibu yake ni kwamba viongozi wetu (hasa JPM) walituonyesha kwa mfano wao wenyewe kwamba maisha lazima yaendelee, na kwamba hofu juu ya corona inaweza kuwa mbaya zaidi hata ya corona yenyewe. Pili, hali ya corona kwa sasa nchini ni kama imetulia hivi. Kilichoifanya itulie kulinganisha na upepo uliokuwepo miezi kadhaa iliyopita nadhani haikuwa tahadhari kuhusu corona. Watu waliendeleza maisha yao kama kawaida na bado tukapita. Na huko duniani ambako kuna tahadhari zaidi ya corona sijaona kama wana nafuu yoyote kulinganisha na Tanzania.
 
Kweli bana clouds hamuipendi nimeamini!!! Hivi waliwakosea Nini???

Hivi Kuna precaution yoyote ya Corona kwenye viwanja vya mpira (VPL),????

Hivi mlundikano wote ule wa msiba wa jiwe mlizungumizia precaution yyte ya Corona,????!

Mlundikano kariakoo,karume ,hivi Kuna kujilinda kkte na Corona,????

Maandamano ya bajaji iringa Kuna precaution yoyote ya Corona,?????

Hivi wasafi hawakufanya ""super woman""????

E fm na Dina Mario's hawakugawa tunzo kwa wanawake juzi juzi tu????

Maisha ya kila siku Kuna precaution yoyote ya Corona?????

Kweli clouds media hamuipendi ,hivi waliwakosea Nini???

Yaani kitu kidogo tu lazima watalaumiwa utafkili cjui wamefanya nn??
Hivi hamuipendi,?? mnawaonea wivu??, wanawafuatilia Sana?? Ni wakubwa Sana kuliko media nyingine???
Mkuu binafsi mi naipenda sana clouds media, ni moja ya brand kubwa sana hapa Tanzania katika tasnia ya habari na burudani

Kama brand kubwa na Kama kiongozi kwa hizi media nyingine, hawana budi kuwa tofauti!

Wao Kama 'kiongozi" wanatakiwa kuwa mfano mzuri. Hawatakiwi kuwa Kama wengine

Naipenda clouds ndiomaana nimewapa angalizo
 
Back
Top Bottom