Chanzo cha B. Dozen kuhama Clouds

Hapa B12 alifikiri Clouds ni ya babayake, ukiongezea na ile ya PKP Mapacha

1591342155679.png

By Sangu Joseph

Duuh kwanza nianze kwa kushangaa, kama ambavyo wengi tulishangazwa kuona taarifa ya kutua kwa B Dozen, Dozen ametua kwa Waswahili eFM & TVe hii taarifa kubwa kwa Wapenzi wa Media na Tasnia ya Burudani Bongo.

Kabla ya kwenda mbali uwezo wa Bdozen hakuna ambaye haufahamu, kwanza anaheshima kubwa sana kwa wasanii imefika hatua kuna wasanii hawamuiti jina lake la Dozeni wanamuongezea Brother Dozeni.

Kuathirika au kutoathirika kwa Clouds Media Group hiyo tutabonga siku nyingine, leo tumjadili Boss Francis Majizzo
Unaweza ukajiuliza kwanini huyu jamaa anasajili Giants kwenye Kituo chake, kwani haoni Watangazaji wachanga mpaka anasajili Giants, naikumbuka kauli moja ya Majizzo wakati wa kumuendeshea Mchango Boss Ruge Jasiri Muongoza Njia alisema kuumwa kwa Ruge game kwake ilikosa ushindani kwasababu Ruge alikua akimpa changamoto sana, nadhani kwasababu alishawahi kukiri Ruge ndiyo alisababisha na yeye kufungua Kituo cha Radio hivyo alikua akipita kwenye miguu yake.

Nadhani kwa sasa naweza kusema game ni kama nyepesi kwake, kwa sababu anaweza kumng'oa Mtangazaji yeyote wa Media yeyote amtakaye, hatua ambazo zilikua za Jasiri Muongoza Njia.
.
Game imekua ya kawaida kwake ndiyo maana unaona kaleta #Homa TVE na atawaleta Waimba Kwaya kwenye kipindi cha Vijana na Vijana wakatamani waimba Kwaya warudi tena.
.
Ili media iwe na impact kwanza lazima uwe na watu wasikilizaji, pili uifanye iwe media ambayo hata Mtangazaji /Mwandishi anayechipukia ahisi hicho Kituo ni sehemu ya Ndoto yake anayopaswa kuifikia, na anawezaje kuhisi hilo kwa kuvutiwa na Watangazaji wakubwa kwenye hicho kituo, Activities za Kituo, Flow ya upatikanaji wa Watu maarufu kwenye hicho kituo, ambayo kwa sasa unaiona Majizzo anaipeleka huko EFM, itawafanya Watangazaji na Waandishi Chipukizi waseme Efm ni moja ya vituo ambavyo unaweza kufikia Ndoto zako.

====

By Sangu Joseph

Kama nilivyoahidi kwenye kwenye Andiko langu lililopita kuwa ningeandika kuhusiana na kuathirika au kutoathirika kwa Clouds FM kuondoka Kwa BDozen nadhani ule wakati ndiyo leo.
.
Ukiniuliza binafsi, "Je, Sangu J unadhani Clouds watayumba baada ya kuondoka kwa BDozen?" nitakwambia BIG HAPANA ila watapata ushindani mkubwa kwa sababu hawa jamaa huwa wanakua na tahadhari ya kuwandaa Watangazaji wao wapya, wachukue nafasi pindi Watangazaji wa muda mrefu wasipokuwepo, ndiyo maana kwenye siku ambazo ni sherehe za Kitaifa mara nyingi unasikia sauti mpya, kama wakina John Jackson, Lugha Kali, Abdul Chambea na MoJ360, Broh Tei The Best, Perfect Crispin.
.
Turudi kwa Dozen na Clouds kwanini nasema hakuna Pengo, hawa jamaa walianza kumuandaa Kennedy The Lemedy, kumrithi Dozen muda mrefu ndiyo maana uliona alipewa mashavu mengi sana kwa muda mfupi Wadau tunasema waliamua kumpeleka Mjini.

Nawakumbusha kwanza Kennedy alipewa kitu kinaitwa Waziri wa Burudani kwenye Fiesta, lengo lilikua ni kumjengea heshima kama aliyokuwa nayo Dozen kwa wasanii, ili upate Shavu la kuperfom Fiesta ilikua lazima upitie Kwa Kennedy, hakuishia hapo Mara Paap akaoneka kama Mwakilishi wa Vijana kwenye Fainali ya Miss Tanzania ili kumtambulisha kwa Wadada na kumjengea kizazi chake cha Warembo, baada ya hapo akaonekana kwenye kampeni ya Kipepeo kama Balozi yeye na Meena Ally, lengo ni kumtambulisha Kennedy kwenye kizazi kipya kinachosikiliza Radio mtaani ambao wengi wao ni Vijana wa baadaye na wao ndiyo hitaji lao, unajua Taaluma ya Utangazaji huwa zina nyakati, kuna nyakati unakua juu Ila hicho kizazi kikipita utashuka, sasa utakua media kama Clouds wanalijua hilo Kwamba Dozen alianza 2000 kutangaza maana yake Vijana wa 2000 - 2010 wengi sasa ni watu wazima na kusikiliza Radio ni mara chache sana hivyo Kennedy inabidi apelekwe Mjini awachukue Vijana kuanIa 2016 - na kuendelea kwa sababu ni mwenzao na wanamuelewa.
.
Ukiangalia wakati wa kipindi Kennedy alikuwa ni mtu anayekaa karibu zaidi na Dozen kuliko Watangazaji wote XXL, na hata sasa unaona yeye ndiyo kama Main Man kwenye Show, anacontrol kila kitu.
.
So kuondoka kwa Twangalla na uwekezaji wa Clouds kwa Kennedy ni suala la muda na kusubiri, nikiri Heshima ya BDozen kwenye Burudani itabaki kuwa juu juu zaidi.

Wakati ujao nitaeleza maoni yangu juu ya namna ambavyo nadhani Boss Majizzo atamtumia BDozen Dozen Ametua pale uswahilini Efm na TV - E
.
Nicheki Instagram : Twit : FB Sangu Joseph
.
 
Mtangazaji anapotoka media A kwenda B huwa anahama na baadhi ya wasikilizaji wake watiifu, Hilo ndio pengo lenyewe. Ukiniambia hajaacha pengo nitakwambia NO! Kaacha pengo Mawingu pale. Kuna wakati unaweza kufanya usajili mbovu ukapunguza wasikilizaji fulani. Moja ya sajili zilizokuwa mbovu ni Meena Ally kwenda Amplifaya kipindi cha nyuma.
 
Uko sahihi kabisa kwa maono yako,,lakini nna wasiwasi sana na Kenedy dawa kwenye suala la Kiingredha hasa kuwa'interview wasanii wasiojua Kiswahili,,Kenedy English inamsumbua apparently,, Nilikua nafatilia interview walizowafanyia Mr.Eaz,Davido,Kizz Daniel, Skales,nk.wote hao aliyekua anawa'interview zaidi ni Twangala na Mchomvu kwa mbali lakini Kenedy kiukweli alikua kimya na kama akiuliza swali unaona kabisa Lugha anaihangaikia mno,,sasa kama main host on mic number moko inatakiwa wewe ndo uwakaribishe hao wasanii and other stuffs related to such issues,, Namuona Meena Ally sana katika jukumu hili,,lakini pia Kenedy the R'reeeeee hana uwezo wa kuwa'handle,kuwa'manage watangazaji wenzie(on the issue of time management),,Jana2 hapa kashindwa kuwa'control Wakazi,Mawenge na Nikki mbishi hadi time ikaisha na Nikki interview yake haijakamilika,,,,Kwangu udhaifu wa Kenedy ni huo
 
Kenedy bado anakua Mkuu, kikubwa muda Tu ukifika yote yatakua Historia
 
Mtangazaji anapotoka media A kwenda B huwa anahama na baadhi ya wasikilizaji wake watiifu, Hilo ndio pengo lenyewe. Ukiniambia hajaacha pengo nitakwambia NO! Kaacha pengo Mawingu pale. Kuna wakati unaweza kufanya usajili mbovu ukapunguza wasikilizaji fulani. Moja ya sajili zilizokuwa mbovu ni Meena Ally kwenda Amplifaya kipindi cha nyuma.
Mkuu huijui Clouds, kuna kitu kinaitwa Clouds na kuna Watangazaji wa Clouds, Kwa heshima na umaarufu wa Clouds hamnaga Kosa kwenye usajili wao, wewe unasema Meena ni mbovu kamsikilize Meena wa XXL ndiyo utamjua ni nani
 
Uko sahihi kabisa kwa maono yako,,lakini nna wasiwasi sana na Kenedy dawa kwenye suala la Kiingredha hasa kuwa'interview wasanii wasiojua Kiswahili,,Kenedy English inamsumbua apparently,, Nilikua nafatilia interview walizowafanyia Mr.Eaz,Davido,Kizz Daniel, Skales,nk.wote hao aliyekua anawa'interview zaidi ni Twangala na Mchomvu kwa mbali lakini Kenedy kiukweli alikua kimya na kama akiuliza swali unaona kabisa Lugha anaihangaikia mno,,sasa kama main host on mic number moko inatakiwa wewe ndo uwakaribishe hao wasanii and other stuffs related to such issues,, Namuona Meena Ally sana katika jukumu hili,,lakini pia Kenedy the R'reeeeee hana uwezo wa kuwa'handle,kuwa'manage watangazaji wenzie(on the issue of time management),,Jana2 hapa kashindwa kuwa'control Wakazi,Mawenge na Nikki mbishi hadi time ikaisha na Nikki interview yake haijakamilika,,,,Kwangu udhaifu wa Kenedy ni huo
Huyo Dozen pia ngeli haiwezi,anaungaunga tu..Ngeli ni Sam Misago..Meena pia yupo vizuri..

Hivi Babra anapohost PB akija labda Tundu Lisu yeye ndo atakua muuliza maswali mkuu?
 
Uko sahihi kabisa kwa maono yako,,lakini nna wasiwasi sana na Kenedy dawa kwenye suala la Kiingredha hasa kuwa'interview wasanii wasiojua Kiswahili,,Kenedy English inamsumbua apparently,, Nilikua nafatilia interview walizowafanyia Mr.Eaz,Davido,Kizz Daniel, Skales,nk.wote hao aliyekua anawa'interview zaidi ni Twangala na Mchomvu kwa mbali lakini Kenedy kiukweli alikua kimya na kama akiuliza swali unaona kabisa Lugha anaihangaikia mno,,sasa kama main host on mic number moko inatakiwa wewe ndo uwakaribishe hao wasanii and other stuffs related to such issues,, Namuona Meena Ally sana katika jukumu hili,,lakini pia Kenedy the R'reeeeee hana uwezo wa kuwa'handle,kuwa'manage watangazaji wenzie(on the issue of time management),,Jana2 hapa kashindwa kuwa'control Wakazi,Mawenge na Nikki mbishi hadi time ikaisha na Nikki interview yake haijakamilika,,,,Kwangu udhaifu wa Kenedy ni huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom