Clouds Fm wamshukia Mnyika, wampuuza kwa kuchanganya mambo

Mkuu katika zote nimeiipenda hii, ndio maana ni muhimu kuwa na shule za kata maana tutapata hata vyuo vya tarafa, watu kama akina Gadner wasiwe wanaenda Roben Island wakidhani ukifika huko umemaliza kila kitu. Kuna watu hawajatia timu huko lakini wanajua kila angle ya ile jela, Gadner jielimishe mwanangu, suala la Biashara za siraha ni suala kubwa mno kwa hawa vijana wazee wawili (Gadner na Kibonde). kwanza sio Vijana any more nadhani waache kutangaza sasa waachie vijana wenyewe. Wakati ule akina Amina wanatangaza they were real young,

mkuu hapo nawe umeniacha hoi, hizi shule zetu za kata zisizo na walimu, hazina maabara, hazina maktaba wala vitabu halafu wewe unapendekeza tuwna vyuo vya tarafa? huoni hiyo ni sawa na kumkuta mtu amezama mtoni ila ameshikilia tawi la mti ulio inamia mtoni wewe ukaamua kuukata ili kumrahisishia safari ya kuzimu!!?? We unategemea tukiwa na vyuo vya kata wahadhiri/wakufunzi tutawatoa wapi? maabara/karakana na vifaa husika vitatoka wapi? muhimu ni kuwashawishi hao ndugu zetu "watangazaji" wa redio clouds wasiogope umande wa taaluma ya utangazaji.
 
Huyo Kibonde mwenyewe ameanza kujinadi kuwa anakusudia kugombea ubunge mwaka 2010 huko mkoani kwao Mbeya, ila hajaweka wazi atagombea jimbo gani na kupitia chama gani, sijui atakuwa mgombea huru!!??
Lakini kiufupi kwa wanaoisikiliza redio clouds asikia mengi ya upuuzi na machache ya maana. Angalau mara moja moja kwenye kipindi cha power break fast kuna baadhi ya vitu vya msingi wanaviongea hasa yule anajiita bonge na harakati zake za barabarani.

Duuuh hilo jimbo litakaloongozwa na huyu kibonde mbona litakuwa limekula kwaooooo...jamaa ni kibonde sio kwa jina bali kwa matendo pia yaani ni TOTAL LOSS IN OUR SOCIETY........hapa ndo unapoona utofauti wa wasomi wetu na wa kikenya/uganda...ours wameweka upolitics mbele plus ushabiki wa kisiasa but ZERO mukichwa.Hawana Critical thinking yaani ni upuuzi upuuzi tu na ndio maana nchi yetu iko vile.Huyo Gaderner hata sio wa kumjadili kwani mawazo yake yako kiflava flava si unajua wife ndo bread winner???UNATEGEMEA NINI UKIPANDA BANGIII.....lazima utavuna bangi ...........ndio hio.
 
Niliyasema haya... kuwa baada ya Conference hiyo ya Mnyika tutarudi hapa JF na Udaku mwingine..hoja imezaa hoja pasipo kupata suluhu.
 
Gadner na Kibonde kama mambo mengine hamyajui in details myaache kama yalivyo. Uelewa wa Mnyika na nyie ni tofauti sana. Pia huo ubaguzi wenu wa kutokusoma baadhi ya vichwa au magazeti mengine muache. Kama vipi hicho kisehemu cha kusoma magazeti mkiondoe.
 
Bob;

Hii Thread imenifanya niwaelewe wengi sana hapa JF. Sababu kubwa ni kuwa watu wanaoongelewa ninawafahamu kwa ukaribu, hivyo naona wengi wanavyochemka humu.

Mara kumuita mtu hana akili mara hovyooo wakati hata mtu mwenyewe humjui.

Jamani kazi ni kazi, kuna sheria za kazi. Unavyofikiria kazini sivyo unavyofikiria ukiwa HURU.

Ila wengi wenu humu mnaongea BS kuliko hao mnaowasema.

Mods unganisha hii na ile ya salaamu
 
Clouds???? excuse me...Gadner anajua nini mpaka kufikia level ya kuchambua alichosema Mnyika??.. iam shocked
 
Ongelea/chambua alichoongea Gadner G Habash, USIMUONGELEE GADNA as a person!!!!

siwezi kuongelea utumbo wa hao akina kibonde na gadner!! they know nothing absolute nothing..Unasema nisimuongelee in person sasa unataka nimuongelee kama JIWE au ?
 
kuna siku nilikua kwenye commuter bus, foleni ya Fire.....maneno machafu waliyokua wakiongea Gardener na huyo Kibonde kwenye uchambuzi wa magazeti, yalinisononesha sana ukichukulia ndani kulikuwa na wamama jamani...anyway, hakuna ubishi kwamba most of the guys there ni OPPORTUNISTS wa kutupwa,angalia Gardener anavyomng'ang'ania JAY DEE kisa huyu dada ana pesa...muda mwingi wanatumia kusifia BANGI na kuingiza misamiati ya maneno ya KIHUNI kwa wasikilizaji...viongozi wetu wanapenda media za hivi zinazojaza ujinga wananchi ili watawale kwa raha, no CHALLENGES from the public coz tayari jamii inakua busy na upumbavu wa vijana kama hawa...tumepoteza energy na muda kuwajadili kuku hawa!! aaagh!! @$%#&^*\"@
 
hakuna mwenye elimu clouds...they are just entertainers. uwezo wa kuchambua mambo mdogo. kina kibonde na wenzie ni ma-MC tu ndo maana wanaropoka hovyo. hata kama mnyika kakosea they dont have to take side wasome habari waiache ilivyo wananchi ndio waamuzi.
 
mi wananipa hasira sana hawa...yaani kwanza wife akiweke hiyo Clouds tukiwa tunatoka job jioni natamani nizime radio.....teh teh

Kumbe umeoa mke ambae naye anakupa hasira? Duh mzee unafukuta hapo.
 
Clouds ina watangazaji ambao uelewa wao ni mdogo sana hasa inapokuja kwenye masuala ya msingi. Ripoti inayoihusisha TZ na uuzaji wa siraha kwa majirani zetu wenye matatizo siyo ya kwanza. Zimewahi kutolewa ripoti nyingine mbili ambazo nimewahi kuzisoma.

Hawa clouds waulize fifty cent ana magari mangapi, ana mademu wangapi ana majumba mangapi watakueleza. Ila ukiwauliza mambo serious kama haya hawajui lolote. Mlimani pale tunawaita VILAZA.Gardner,Kibonde,Ruge....... na hata bosi wao Kusaga ni VILAZA TU,wako obsessed na pesa za haraka haraka.
 
Clouds ina watangazaji ambao uelewa wao ni mdogo sana hasa inapokuja kwenye masuala ya msingi. Ripoti inayoihusisha TZ na uuzaji wa siraha kwa majirani zetu wenye matatizo siyo ya kwanza. Zimewahi kutolewa ripoti nyingine mbili ambazo nimewahi kuzisoma.

Hawa clouds waulize fifty cent ana magari mangapi, ana mademu wangapi ana majumba mangapi watakueleza. Ila ukiwauliza mambo serious kama haya hawajui lolote. Mlimani pale tunawaita VILAZA.Gardner,Kibonde,Ruge....... na hata bosi wao Kusaga ni VILAZA TU,wako obsessed na pesa za haraka haraka.
wekeni CV zao hapa tuzione...
 
Hata kama watangazaji wao wanaelim ndogo, one crdit lazima tuwape ni kwamba, WAPO DOMINANT KATIKA REDIO STATION ZA TZ.

Pili wanahaki ya kutoa maoni kama JF members wengine walivyomkosoa mnyika, so me hapa sioni big deal lolote.
 
Back
Top Bottom