Clouds FM muige mfano CBE kwa kuvaa mavazi ya heshima!!!

Watanznaia tuna mambo mengi ya muhimu ya kushughulikia zaidi ya hili la mavazi wanayovaa wanawake. Tunatumia akili nyingi mno kumchunguza mwanamke. Waacheni wavae wanavyotaka.

mkuu wazo ni zuri ikiwa wanawake wenyewe watavaa kwa kujisitiri tu na kupendeza tatizo wanavaa kwa mitego kwa maana ya ushawishi wa ngono!!
 
Kuna mdau alishawahi kuanzisha topic eti posts za pdidy huwa hazieleweki?
Kumbe anaeleweka tuu.
 
Kuna mdau alishawahi kuanzisha topic eti posts za pdidy huwa hazieleweki?
Kumbe anaeleweka tuu.
ndibalema tukiwa chuo mlimani walikuwa ngwini walikuwa wana tabia ya kukashfu jamani wanawake wa COET kama madume hivi wanachaguliwaje mwisho wa siku ndio wanaomaliza shule na kuolewa wao(ngwini's) wanaback kutafuta mume..sasa ujui hao wanaompenda didy wanaitaji gani..sio kosa lao
 
ndibalema tukiwa chuo mlimani walikuwa ngwini walikuwa wana tabia ya kukashfu jamani wanawake wa COET kama madume hivi wanachaguliwaje mwisho wa siku ndio wanaomaliza shule na kuolewa wao(ngwini's) wanaback kutafuta mume..sasa ujui hao wanaompenda didy wanaitaji gani..sio kosa lao

P didy style yako ya uandishi ni kipekee!! watakuelewa tu!
 
Eti "Mwitikio ama ushirikiano halina" P Diddy bana! teh teh teh

Nimekuuliza nane unusu mchana ama usiku mbona hujajibu?
 
MAVAZI YA KIKAHABA CHANZO KIKUU CHA ZINAA NDANI YA KANISA
Mapema kabisa nachukua nafasi hii kuupongeza kwa dhati uongozi wa Chuo cha Elimu ya biashara CBE kampasi ya DSM unao ongozwa na Athman Ally Ahmed baada ya kunzisha kampeni za kupinga mavazi ya Kikahaba chuoni hapa ,kazi ambayo makanisa yote ya kipentecosite nchini yameshindwa kuifanya.
Baada ya kulisoma gazeti la Habari leo la machi 29,2012 na tahiriri ya gazeti la Tanzania Daima la machi 31,2012 nimebarikiwa sana na mtazamo wa vyombo vya habari na hivyo kuamua kuanika ukweli tatizo la mavazi ya kikahaba na athari zake makanisani. Kwa kuwa Vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa dola,napenda kuwashauli wahariri watendaji wa vyombo vya habari waunge mkono VITA hii ya mavazi ya magharibi ,kwa kutunga kanuni za mavazi kwa waandishi wa habari kwani wapo wangine wanavaa mavazi ya kikahaba na kutia aibu kwa chombo cha habari husika .
Mimi ni mwinjirisiti na ninauzoefu mkubwa na hali la kanisa na maadili nchini ambapo kwa sasa ni viongozi wachache wanasimama katika kweli ya neon la Mungu na kulinusuru taifa.
Kwanza kabisa nifafanue kwamba kazi ya mtu inaweza kutambuliwa mapema kabla ya kumuuliza mhusika kwa kuangalia mavazi yake tu . Kwa mfano tunaweza kupambanua kuwa huyu ni askari polisi au askali magereza au askali JWTZ kwa kuangalia mavazi yao tu.pia unaweza kujua kuwa huyu ni kada wa CCM au CHADEMA au CUF kwa kuangalia mavazi ya sare zao za chama.
Halikadharika ukienda kanisani utamfahamu ni yupi ni muumini na yupi ni mchungaji kwa kuangalia mavazi. Katika shule unaweza kupambanua mwanafunzi na mwalimu kwa kuangalia mavazi. Kicha anagundulika haraka kwa mavazi yake na watu wanachukua tahadhali haraka.
Ni kwa sababu hii Kahaba naye anagundulika mapema kwa kuangalia sifa hizi za awali ambazo ni mavazi ya kikahaba.
Mungu alitahadhalisha mapema mavazi ya kikahaba kabla hayajatokeza katika ulimwengu kwa kuwa alijua mapema angalia katika vifungu hivi (Mithali 7:7-27, Kumbukumbu la torati 22:5, 1Timotheo na Mwanzo 38:14-15).


Bibilia ina sema katika kitabu cha kumbukumbu la Torati 22:5 ‘Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume ,wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke ,kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA MUNGU WAKO.’
Nguo zinazotajwa(nguo za kikahaba) hapa hata Jeshini zimepigwa marufuku,huwezi kuona suluali za kubana Jeshini lakini wapendwa wanavaa kanisani!
Katika katabu cha mithali 7:10-27, “Natazama ,mwanamke akamkuta,Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;Ana kelele na ukaidi ,Miguu yake haikai nyumbani mwake , Mara yu katika njia kuu ,mara viwanjani,Naye huotea kwenye pembe za kila njia .Basi akamshika, akambusu , Akamwambia kwa uso usio na haya,Kwangu ziko sadaka za amani;Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu; ndiyo maana nikatoka nikulaki,nikutafute uso wako kwa bidii nami nimekuona,Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri ,Manemane na udi na mdalasini.haya na tushibe upendo hata asubuhi,Tujifurahishe nafsi zetu kwa Mahaba.Maana mume wangu hayumo nyumbani,Amekwenda safari ya mbali.Amechukua mfuko wa fedha mkononi Atarudi wakati wa mwezi mpevu.Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.Huyo akafuatana naye mara hiyo kama vile ng’ombe aendavyo machinjioni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;…’
Pamoja na maneno ya Mungu kuelezea bayana mavazi ya kikahaba na Uzinzi bado Makanisa mengi ya Kipentecosite nchini wameshindwa kuzuia mavazi haya katika makanisa yao kwa kuhofia Kupoteza mapato ya sadaka na zaka. Katika vyuo vikuu vya elimu na watu wenye kipato cha juu wakiwemo wafanya biashara wakubwa nchini ndio wanao ongoza kwa mavazi hayo na ndio wanaotoa michango mikubwa kanisani .

Vigogo hawa na familia zao pamoja na kumvaa nguo za aibu wanatengewa nafasi na kukaa viti maalum vya mbele na kumupa wakati mgumu Mchngungaji anapo hubili.
Kutokana na kukithili kwa hali hii makanisani kumeathili kizazi chote cha kanisa ambapo hadi sasa mavazi ya kikahaba yametawala kwenye vikundi vya kwaya za kanisa ambapo vijana wengi huwa wanajiunga kwa malengo ya kutaka kuolewa.

Migogoro mingi ya kanisa inajitokeza katika kikundi hiki cha kwaya ambapo tuhuma nyingi zinatokana na ngona hususani kumuhusisha hata Mchungaji.
Ni kwa sababu hii nguvu ya Mungu imeondika katika makanisa ya leo na wachungaji wengi wamejikuta wanabaka waumini wao au wanafumaniwa na wake za watu.
Zipo kesi nyingi sana za Maaskofu, wachungaji na hata Wainjirisiti kubaka au kufumaniwa na nina ushahidi na hilo lakini chanzo chake ni mavazi ya kikahaba.

Nimeshuhudia kwa macho mavazi ya kikahaba kwa waimbaji wengi wengi wa nyimbo za injili ambao baada ya nyimbo hizo wanajikuta wakifanya zinaa na kuzaa watoto wakati hawajaolewa na wachungaji wakishangilia nyimbo zao kwa kuwa nao hawana ujasili wa kukemea kutokana na tatizo hilo hilo.
Kwa utafiti wangu nimepita katika makanisa mengi ya kilokole yakiwemo Kanisa la Mikocheni B Assemblizi of God ambako nilikwenda kuhudhulia semina ya wanandoa niliona mavazi ya kikahaba huku Mchungaji Getrude Rwkatare akiwa amevaa wigi anahimiza mafundisho ya kujipamba.
Zaidi ya hapo nimekwenda kanisa la Efatha ambapo nilimuona mke(Elikunda) wa Mwingira amevaa suluali inayo bana(vazi la mwanaume) na cha kushangaza wamepiga picha ya pamoja na Nabii Mwingira na kutumia katika kalenda ya mwaka 2012 na kusambaza kwa jamii.
Pia katik makanisa yote ya TAG na EAGT ambao ndio waasisi wa Upentecosite nchini kumeshamili mavazi ya kikahaba na hakuna anaye kemea.
Mwisho ninawambo viongozi wa dini waanze kufuata neon la Mungu na kuunga mkono VITA ya kubambana na mavazi ya aibu kwa kuwafukuza ndani za kanisa wale wote wenye mavazi ya kikahaba bila kujali sadaka wanazokupa kwani iposiku watakuangusha wewe katika zinaa na kutupwa katika dhambi.
Kukosekana kwa watumishi wenye nia ya dhati na neon la Mungu ndiko kumuwafanya Waingereza waangalie mavazi yetu na tuhukumu kwa kutupa mashariti ya USHOGA mwenye masikio na asikie.





 
Back
Top Bottom