mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,169
- 1,072
Nasikitika kuona vyombo vinavyosimamia tasnia ya habari Tanzania vikiwa kimya kwa muda mrefu sana.
Uchambuzi na usomaji wa habari za magazeti unaofanywa na watangazaji wa Clouds FM hasa katika kipindi cha Powe Breakfast {PB} kinachorushwa mapema asubuhi kikiwa na matangazo lukuki ya kibiashara n.k ni wa kukemewa kwa sababu naamini unapunguza mapato ya wamiriki wa vyombo vya habari hususani magazeti.
Kimsingi zoezi husika lilipaswa kufanywa kwa watangazaji husika kusoma tu vinywa vya habari toka katika magazeti husika na kama ambavyo vituo vingine vya redio vifanyavyo lakini cha kushangaza na kusikitisha habari husomwa kwa kina na mara nyingi kwa zile habari motomoto habari nzima husomwa ,Mbaya zaidi watangazaji kwenda mbali zaidi kufikia hatua kukosoa waandishi wa habari husika kwa kukosoa umakini,weredi wao.
Tukumbuke pamoja na kuhabarisha jamii wamiriki husika hulenga kupata mapato ya kuwasaidia kulipa gharama kuu za kimsingi kuwezesha watafuta habari,uchapaji,mishahara,n.k hivyo basi kwa sisi wateja KWA NINI NINUNUE GAZETI AMBALO TAYARI TAARIFA ZOTE MUHIMU ZILIZOANDIKWA NIMEZIFAHAMU BURE KWA KUFUNGULIA REDIO YANGU {NYUMBANI,KWENYE GARI,KIJIWENI,INTERNET}?
Upo uwezekano wa makampuni mengi kufa kibiashara kwa sababu ya ukata na kuongezeka kwa gharama zisizolipika...Nashauri vichwa husika visomwe na si habari kamili la habari kamili zisomwe jioni ili kutoa fulsa za mtambuka kibiashara kwa wamiriki