Clouds FM; mbona hivyo?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Mimi huwa kuna vipindi ambavyo nafuatlia Clouds FM na nakiri ikifika muda huo huwa lazima niitafute clouds FM. Miongoni mwa vipindi hivyo ni POWER BREAK FAST, NJIA PANDA, na SPORTS.

KWa wiki mbili sasa nimekuwa nanshangazwa kwa kutosikia vipindi vya power breakfast cha Gerad Hando na Paul James wanapoeruzi magazeti na Sebastian Ndege na Njia panda.

Wadau tusaidiane, hivi watangazaji ndo tatizo au vipindi ndo vimekufa? Nakumbuka kuna wakati hata kipindi cha Sport cha usiku walikuwa wakituwekea miziki. Vipi Clouds FM? Au ndo iko safarini kufa?
 
Wako likizo ambayo to me it doesnt make sense at all! ni weakness ya management hawako tough enough kuamua nani abaki nani aende kula likizo siku izi za christmas na new year,uyo Kusaga hana ubavu huo ata kidogo lakini bila ya yeye kujua akidhania anawa please wafanyakazi wake kumbe anawaudhi wateja wake mamilioni apa nchini nadhani tatizo la darasa linamsumbua Kusaga,kama angekuwa kasoma aya mambo yasingetokea na clouds ingekuwa mbali sanaaa...Kusaga rudi shule hujachelewa ata ivo!!!
 
the way i know ni kuwa wamekwenda likizo mpaka mwanzoni mwa mwaka kesho!!!

miaka yote huwa wanafanya hivyo.
 
Acha zako wewe

Hawa Cloud's wapo likizo mwanawane mpaka mwakani tarehe za Mwanzoni.

Kuwa Mpole mambo mazuri wanakuja ndani ya Clouds. Ni radio station nzuri in Town
 
Wamechemka sana hawa jamaa.
Kama ni likizo si wangefunga na vipindi vyote ieleweke watangazaji wapo likizo.
Kuliko kututangazia vipindi half half inakuwa sio vizuri kabisa mna tuboa wasikilizaji.
 
Wamechemka sana hawa jamaa.
Kama ni likizo si wangefunga na vipindi vyote ieleweke watangazaji wapo likizo.
Kuliko kututangazia vipindi half half inakuwa sio vizuri kabisa mna tuboa wasikilizaji.
Labda itabidi wajifunze kutokana na malalamiko ya wasikilizaji!
 
Acha zako wewe

Hawa Cloud's wapo likizo mwanawane mpaka mwakani tarehe za Mwanzoni.

Kuwa Mpole mambo mazuri wanakuja ndani ya Clouds. Ni radio station nzuri in Town
the way i know ni kuwa wamekwenda likizo mpaka mwanzoni mwa mwaka kesho!!!

miaka yote huwa wanafanya hivyo.

Ingekuwaje kama Hospitali,polisi,masoko,bar etal nao wakienda likizo?
 
...acha tu wasiwe hewani, hata mpaka mwakani :(, ...Power breakfast ilikuwa highly rated enzi za Masoud Kipanya, Fina Mango, na huyo Gerrard Hando, sio sasa.
 
...acha tu wasiwe hewani, hata mpaka mwakani :(, ...Power breakfast ilikuwa highly rated enzi za Masoud Kipanya, Fina Mango, na huyo Gerrard Hando, sio sasa.
Mkuu usikariri!!!!
POWER BREAKFAST bado iko juu vibaya.
PJ, BABRA na GERALD HANDO wameziba vizuri sana gap la hao watu wako na kipindi kinazidi kunoga!!!!Na muhimu kinachijadiliwa hapa ni kitendo cha clouds kutorusha hewani baadhi ya vipindi kikiwemo hicho cha PB.
Watu wanapohoji kulikoni mbona PB hairushwi hewani ujue kuwa wanakikubali kipindi pamoja na wanaokiendesha vinginevyo wasingeulizia kulikoni?????
 
lakini huu ni utaratibu wao wa kila mwisho wa mwaka, wanakwenda retreet, si likizo kama likizo za kawaida, wanakuwa na retreet ya pamoja wafanyakazi wote kwa ajili ya kupanga mambo ya mwaka unaofuatia
 
Tatizo letu hapa mkuu ni kwanini baadhi ya vipindi tu ndivyo havirushwi hewani??au unataka kutuambia kuwa hivyo vipindi visivyorushwa ndivyo tu watangazaji na waandaaji wake wamekwenda retreet???na hao wasiokwenda hiyo retreet hawapangi mambo ya mwaka unaofuatia au hao wenzao ndio wanawapangia???au imekaaje hii???
 
Kuna baadhi ya fani huwezi kwenda likizo....

...acha upuuzi wako hapo,nani anafanya kazi non stop bila likizo? na hao Clouds waache ujinga wao wa kufunga vipindi eti wako likizo,kwani hakuna replacement? ...nilisahau kuwa ni biashara za kiswahili zinazoongozwa na longolongo tuu!
 
Acha zako wewe

Hawa Cloud's wapo likizo mwanawane mpaka mwakani tarehe za Mwanzoni.

Kuwa Mpole mambo mazuri wanakuja ndani ya Clouds. Ni radio station nzuri in Town

Kwa maoni yangu hii ni poor planning. Wanaweza kabisa kwenda likizo lakini wakahakikisha kuna Watangazaji wachache watakaoweza kutangaza vipindi ambayo vina umaarufu mkubwa kwa wasikilizaji wao.
 
Wamechemka sana hawa jamaa.
Kama ni likizo si wangefunga na vipindi vyote ieleweke watangazaji wapo likizo.
Kuliko kututangazia vipindi half half inakuwa sio vizuri kabisa mna tuboa wasikilizaji.

Wadau hii ni ishara kuwa vipindi vya Clouds ni popular lakini kwa wale wajasiriamali(entrepremeurs) ni oppurtunity ya kuanzisha Station Zenu hasa mikoani.
Many more stations coming up in the regions-model ya Clouds ni mfano just stay tuned!
 
Tatizo la Clouds ni Elimu na iko duni sana pale ndo mana Uongozi mbovu na hii imesababisha watangazaje pale ku own vipindi na hawataki wasaidizi ili wasifunikane,utakuta wako radhi kifungwe kipindi wapige mziki...Poor leadership,poor judgement,poor planning,kinachowasaidia ni ubabaishaji ambao mpaka sasa uko in their favour lakini ubabaishaji unakuwaga na mwisho...
 
Waoko retreat kama vile training fulani hivi..."kwa shangazi"waache wapewe ujuzi mwingine mpy maana mwaka mzima wanakuwa busy na same knowledge....waache wapewe zingine waboreshe vitu zaidi.....kila sehemu inatakiwa kuwa na refresher course kuongeza ufanisi kazini.....
 
Back
Top Bottom