Clouds FM inasikilizwa kuanzia usiku, E-Fm yatawala mchana

Hearten

Member
May 17, 2016
46
54
Mambo,

Redio ya watu sasa inaburuzwa na E-Fm baada ya utafiti kuonyesha taarifa za takwimu namna ya watu wanavyosikiliza radio mbalimbali jijini Dar es Salaam.

13615087_1157816060936153_5838025627848751490_n.jpg
 
Duhh, E-FM wameanza juzujuzi lakini wamekuja juu mno. Nawapongeza na hongera sana wanaE-fm kwa kuvuta idadi kubwa ya wasikilizaji. Ni hivi punde nami nilikuwa nawasikiliza kwenye kipindi chao cha michezo. Wajitahidi kufikisha matangazo yao nje ya Dar.
 
Mimi toka nimeijua efm sikuwahi kufungulia upuuzi mwingine,kwenye michezo niko radhi hata niikose papuchi lakini sio e sports au sporta headqurter
 
Naona E-Fm wanatuchezea akili na hawa watafiti wao. hivi jahazi na ubaoni ipi inasikilizwa zaidi? plus ule muda wa amplifaya
 
Efm bonge la radio . ..wajitawanye wafike kila pande ya nchi.. Mi naisikia pia sana usiku muda wa singeli
 
Clouds Radio,bado ni kituo bora cha muda wote kwa wasikilizaji wa rika zote....Hizo tafiti zenu uchwara hazina mashiko hapa.
 
Clouds ilikuwa Bora sana,ila imeharibiwa na majungu na mipasho ya kina Dauda na Mbwiga. Mtu kama Ibrahim Masoud sio wa kumuachia aondoke. Sasa ndio anaing'arisha Efm. Na hilo Jahazi siku hizi limebaki jina tu. Kipindi pekee Clouds ni Emplifire cha millard tu. E fm wako vizuri wanachotakiwa ni kujitangaza na mikoani kwa sasa. Namimi nakubali 93.7 Huu mchezo hauhitaji hasira.
 
Mi nipo mkoa hiyo Efm haijafika bado, hebu niambieni nayo ina matangazo kibao kama clouds??? Maana ni kinyaaaaaaaa..
 
DAIMA SIJAWAHI KUZIELEWA HIZO REDIO MNAZOSHABIKI,ZIMEJAA MAJUNGU,UMBEA NA MIPASHO KUANZIA ASUBUHI HADI JIONI,BILA KUWEKA UBINAFSI,UPENDELEO WALA UJUAJI,REDIO BORA KWA SASA AMBAYO UNAWEZA KUSIKILIZA KITU UKAELEWA MANTIKI NA MAANA YA UNACHOSIKILIZA NI RFA NA RADIO ONE,HIZO REDIO ZINAKUPA REPORT KILA MUDA BILA KUSAHAU BURUDANI,HIZO NYINGINE NI WABANA PUA TU NA MA..S..GA NDIO WAMEJAZA HUKO
 
Mapenzi ya radio yanatokana na vipindi husika! Kwa mfano kama mimi, Clouds nackiliza PB, XXL na Jahazi! Amplifier ni kipindi kizuri ingawaje kinaboa matangazo yasiyoisha!

Michezo mara nyingi nasikiliza EFM! Sasa kama interest yako ni news, of coz, si Clouds wala EFM inaweza kuwa chaguo lako!
 
Clouds ilikuwa Bora sana,ila imeharibiwa na majungu na mipasho ya kina Dauda na Mbwiga. Mtu kama Ibrahim Masoud sio wa kumuachia aondoke. Sasa ndio anaing'arisha Efm. Na hilo Jahazi siku hizi limebaki jina tu. Kipindi pekee Clouds ni Emplifire cha millard tu. E fm wako vizuri wanachotakiwa ni kujitangaza na mikoani kwa sasa. Namimi nakubali 93.7 Huu mchezo hauhitaji hasira.

hicho kipindi cha EMPLIFIRE labda kinapatikana kwenye radio yako mie naijua amplifier tu aiseee
 
Efm wabaki Dar pekee at least kwa miaka 4/5 mbele...... Kilichoifanya clouds iwe hapa ilipo leo.... Watu wa mikoani wanakua obsessed nayo wakija town wanaskiza hio tu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom